nilipoangalia username tu niligundua hii itakuwa ni comment nzuri kwa ajili ya kuisoma, niliwahi kukwambia ya kwamba
lee empire una maarifa makubwa sana ya kutathmini mpira wa miguu na kinachonivutia zaidi ni kwamba huna upendeleo na imenichukua muda mrefu kufahamu ni timu gani unashabikia na kama sijakosea unashabikia timu ambayo ilikuwa na mshambuliaji nisiempenda
jimmy floyd hasselbaink (chelsea fc).
kiukweli mimi pia nashangazwa sana na matokeo wanayoyapata everton msimu huu ila anayepaswa kulaumiwa ni Ronald Koeman kwa kufanya usajili wa kitoto,naamini utumiaji mkubwa wa kifedha aliyoufanya koeman laiti kama angeliufanya robert martinez kipindi kile ndio manager wa everton basi tungelishuhudia everton ngumu sana msimu huu.
- timu kama everton haikupaswa kulipa pound million 30 kwa ajili ya kumsajili goal keeper ambaye ni jordan pickford wakati walikuwa na uwezo wa kulipa angalau pound million 10 kwa ajili ya usajili wa Joe hart au kuwapa arsenal pound million 10 kwa ajili ya kumsajili wojciech szczesny ambaye amesajiliwa na juventus.
- wamemundoa gareth barry mchezaji ambaye anaongoza kwa kucheza mechi nyingi za ligi kuu ya uingereza ambaye msimu uliopita alikuwa anacheza vizuri sana na tom davies pamoja na idriss gueye kwenye deep midfielder na wamemsajili kiungo bishoo davy klaassen kwa pound million 25 kutoka ajax amsterdam, klaassen anacheza vizuri ila gareth barry alikuwa ni kiongozi.
- pound million 28 kwa kumsajili mlinzi wa kiingereza michael keane ambaye hana tofauti na rob holding wa Arsenal ni nyingi sana na ronald koeman alikuwa na uwezo wa kumshawishi davinson sanchez kutoka ajax amsterdam au inigo martinez kutoka real sociedad.
- kama wanavyohangaika manchester united kwenye upande wa kushoto na wao everton wana tatizo kubwa upande wa kulia tokea apate majeraha seamus coleman.
- pia nikubaliane na wewe ya kwamba everton wanammiss mno romelu lukaku na mwili wake mzito uliowapa magoli 28 msimu uliopita, huwa najiuliza ingelikuwaje kama lukaku angelikuwa na uwezo wa kuwapiga chenga mabeki kama anavyofanya alvaro morata na washambuliaji wengine, lukaku angelikuwa hatari zaidi ya ugonjwa wa kisukari.unapomuuza lukaku basi unapaswa kumsajili angalau carlos bacca ambaye amekwenda villareal kwa mkopo na kama atashirikiana na rooney huyu wa sasa hivi asiyeweza kukimbia tena na amebaki kujificha eneo la kiungo mchezeshaji basi atafunga magoli mengi tu.ila kitendo cha koeman kumtegemea rooney ampe zawadi ya magoli 30 kwa msimu ni jambo lisilowezekana labda amsomee Ahl albadri kama waliosomewa watu wasiojulikana.
- kituko chengine cha koeman ni kulipa pound million 40 na ongezeko la pound million 5 kwa ajili ya gylfi sigurdsson pesa ambayo walitakiwa walipe manchester united kwa ivan perisic na walikataa,jaribu kufikiria olympique lyon wamelipa pound million 9 kwa chelsea kwa ajili ya bertrand traore aliyekuwa ajax kwa mkopo ambaye ana maajabu makubwa ya kimpira kuliko sigurdsson.
- bado ligi ni ndefu sana ila mwenendo wa everton kutokana na usajili walioufanya haufurahishi, wanaweza kupigana na wakatengeneza mechi ya ushindani ya kuwania nafasi ya 5 dhidi ya jahazi asilia (liverpool fc), timu ambayo mara ya mwisho kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya uingereza paul scholes alikuwa ndio kwanza anaanza kuota ndoto za kulala na mwanamke mzuri usiku wa manane kumbe yupo peke yake na akiamka lazima akoge (alikuwa na miaka 15).