Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Daah man u tunaitaji beki moja katili mwenye roho mbaya kama Ramos ili aweze kukaa na muhuni rojo pale kati ...pia left back ya inaitajika
Rojo na Baily tayari wameshatengeneza combination moja itakayokuja kutisha sana kwenye EPL next season tupate wa kuwasaidia pindi kutakapotokea majeruhi au uwepo wa Red card,ila Mou atazifanyia kazi hizi kufuli na next season tutakuwa na Ukuta pale nyuma wa aina ya Vidic na Rio,kumbuka tayari Vidic amesema kwa mchezo wa Baily pale United basi amepatikana mrithi wake,Rojo kama tulivyoona soka lake halina tofauti na mchezo aliokuwa anacheza Rio,shughuli anaiweza kweli kweli na kingine ni mtoto wa mtaani,soka la mtaani na la ubabe pia analiweza haswaa, sasa subiri Mou amtie ndimu na misimamo atakuja kuwa katili kama Ramos tatizo mguu anaotumia kama beki wa kati kuna faida na hasara nyingi pia kwa washambuliaji aina ya Leo Mess.
 
baada ya kufungwa na Chelsea kwenye mechi ya FA nakumbuka nilitoa mawazo yangu kuhusiana na mwenendo wa timu yetu na miongoni mwa mambo niliyoyazungumzia ni kwamba hatuwezi kuifunga Chelsea mechi ya ligi kuu kama tutashindwa kumdhibiti eden hazard na pia nilisema ya kwamba hatuwezi kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu kwa hivyo ni bora tupiganie kombe la Europa ambalo tumebakisha mechi 5 tu ili tuwe mabingwa na kujihakikishia nafasi ya kushiriki UEFA kuliko kupoteza nguvu nyingi kwenye ligi kuu ambapo tulikuwa tumebakisha mechi takribani 14.

kiukweli hili suala la kutokuwa na uwezo wa kupata nafasi ya nne lilikuwa ni gumu sana kwa baadhi ya washabiki wa humu ndani kulikubali nahii ilitokana na kuwa mashabiki wengi wao waliamini mechi bado ni nyingi na timu inaweza kufanya vizuri na timu pinzani kama Liverpool zinaweza kupata matokeo mabaya na ikawa ni faida kwetu.

naamini jose mourinho thread hii hajawahi kupita nawala haifahamu ila nashukuru mawazo yangu aliyafanyia kazi kwa sababu alitafuta dawa ya kukabiliana na hazard na pia alizidisha nguvu kwenye mapambano ya kuwania kombe la Europa na kilichotokezea kila mshabiki wa Manchester united kimemfurahisha.

wapo mashabiki wanaomkosoa mourinho kutokana na mbinu zake ila mimi naamini ndani ya mwaka mmoja wa utawala wake amerudisha ubora wa timu kwa 60% na naamini 40% zilizobakia atazikamilisha msimu huu.mimi binafsi nilipokuwa naangalia mechi za Manchester united hususan kwenye round ya pili nilifika wakati nilikuwa sina presha yoyote kwa sababu nilikuwa nayafahamu matokeo tutakayoyapata inawezekana tutapata ushindi au tutatoka draw ya goli moja. nilikuwa naamini hakuna timu yoyote yenye uwezo wa kutufunga goli Zaidi ya moja kwenye mechi na kumbukumbu zangu zinaniambia ukitoa mechi ya arsenal na tottenham ambazo kwangu mimi nazichukulia kama ni mechi za kirafiki sifikirii kama kuna mechi nyengine ambayo tuliruhusu bao Zaidi ya moja kwenye round ya pili na kiukweli haya ni mafanikio makubwa sana.

tatizo kubwa ambalo lipo ndani ya timu yetu ni umaliziaji wa mechi na hili ndio lililosababibisha tufanye vibaya kwenye ligi kuu,laiti kama tungelikuwa makini kwenye ufungaji basi mechi zote tulizotoka suluhu ndani ya old Trafford tulikuwa na uwezo wa kushinda wastani wa mabao (3-1).tunahitaji mshambuliaji ambaye ana uwezo wa kufunga magoli 25 kwa msimu,

wapo baadhi ya mashabiki wanamuona belotti anatufaa kwenye timu yetu, mimi sijawahi kumuona akicheza kwa sababu sijawahi kuangalia mechi ya torino ila napatwa na mashaka na wachezaji wa ligi ya Italy wanapokuja uingereza wanapata wakati mgumu sana kwa mfano Crespo, veron, Shevchenko, jovetic, savic, ballotelli wote viwango vyao havikuwa vizuri kama mashabiki walivyotegemea.

mimi naamini wachezaji hawa tulionao basi tuna uwezo wa kucheza robo final msimu ujao kwenye uefa na si kwasababu ni wachezaji wazuri sana ila sababu kubwa tuna mwalim bora ambaye anafahamu jinsi ya kuzitumia mechi mbili za mashindano ya uefa, Mourinho ndiye mwalimu pekee ambaye ana uwezo wa kuondoa huu utawala wa timu 3 uliopo kwenye uefa ambapo nawazungumzia real Madrid,Barcelona na Bayern munich. tunahitaji kufanya usajili kwa kuziangalia timu hizi ambazo ndio bora kwa kipindi cha miaka 6 mfululizo na si kuwaangalia timu kama Arsenal, Liverpool,Chelsea, Manchester city na tottenham wamefanya usajili gani, mimi hawa nawachukulia kama ni majirani zetu na si wapinzani wetu kwa sababu ni wachezaji wachache sana wanaozichezea timu hizi ambao wanaweza kupata namba kwenye vikosi vya real Madrid, Barcelona na Bayern munich.

ukiondoa tatizo la ushambuliaji pia tuna tatizo la upande mzima wa kushoto kuanzia beki tatu na winga, wapinzani wetu wako vizuri kwenye upande huu, real Madrid wana carvajal, bale, asensio ,isco.hivyo tunahitaji mlinzi bora wa kushoto kama rose wa tottenham na winga kama perisic wa inter milan na naamini kama atajikaza mourinho wote anaweza kuwasajili.

pia tunahitaji viungo wa kati ambaye atakuwa na uwezo wa kukabiliana na wachezaji kama modric,isco,vidal,rakitic,bosquet na wengineo na nafikiri bakayoko anatufaa kutokana na umbile lake na hata matuidi japokuwa ana miaka 30, kama tutaongeza viungo itakuwa ni faida kubwa sana kwetu kwa sababu tutapata kumtumia pogba na Herrera kwenye namba zao za asili.

Tafadhali jose mourinho turudishie heshima yetu na pia tuondolee huu utawala ninaouchukia wa timu za Hispania kwenye ligi ya mabingwa na yote hayo yanawezekana kwako wewe kwa sababu wewe ni:

bingwa wa tactics na uwezo huu umeuonesha kote ulipofundisha kuanzia porto, intermilan, Chelsea, na hata real madrid
 
World football rich list

1) Manchester United - $3.69 billion

2) Barcelona - $3.64 billion

3) Real Madrid - $3.58 billion

4) Bayern Munich - $2.71 billion

5) Manchester City - $2.08 billion

6) Arsenal - $1.93 billion

7) Chelsea - $1.85 billion

8) Liverpool - $1.49 billion

9) Juventus - $1.26 billion

10) Tottenham Hotspur $1.06 billion
 
The club, owned by the American Glazer family, is also substantially the most profitable, posting operating income of $288 million -- more than fellow English clubs Arsenal ($122 million), Chelsea ($52 million, Liverpool ($29 million) and Tottenham Hotspur ($68 million) combined.
 
Maoni yangu Juu ya Kipa wetu David De Gea.

Akili huwa na tabia ya kuchoka au kuzoea mazingira hivyo kuhitaji mazingira na changamoto mapya.

Akili ya David de Gea imeshachoka na kuzoea mazingira na changamoto za pale Old Trafford na hivyo kuhitaji mazingira mapya,ndio mana unaona katika match za mwisho wa msimu alianza kuwa nje ya mchezo na kufikiria uhamisho wake hasa baada ya Real Madrid kutaka kumsajili na Juu ya Mafanikio ya Real Madrid katika misimu hii miwili.

Hii inatokana na kuwa katika kiwango kuzuri pale Old Trafford lakini tatizo tuliokuwa nalo la kutokuchukua makombe katika misimu hii minne baada ya kustaaf kwa Kocha wetu mwenye mafanikio Sir Alex Fegurson ndio lililomfanya David de Gea kuyachoka na kuyazoea mapema mazingira ya Old T na hivyo kuhitaji changamoto mpya katika ligi nyingine.

Ni ukweli usiojificha katika misimu hii ambayo hatukuwa tukifanya vizuri ndio kipindi pekee ambacho De Gea alifanya kazi ya ziada kuzuia timu kutokupata matokeo mabaya Zaidi licha ya matokeo tuliyokuwa tunayapata lakini kwa kiasi kikubwa David De Gea alikuwa Imara langoni na kuchomoa mikwaju na michomo ya maana, ndio mana haishangazi kuona akichaguliwa kuwa mchezaji bora katika misimu hiyo ndani ya kikosi hiii ni kutokana na wachezaji wa ndani kutokufanya kazi yao ipasavyo/kutokuwa na wachezaji Wenye njaa na mafanikio pamoja na ubovu wa mbinu za makocha.

Kwa kiwango chake alichokionesha na kama tungebahatika kufanya vizuri katika misimu hii hasa kombe la ligi kuu na Uefa champion leo hii tusingesikia madai yake ya kutaka kuhama kwenda Madrid.

Now tuna Kocha wa Dunia anayejuwa mahitaji ya Timu na ni Kocha wa Makombe,Falsafa ya Mou ni kushinda Mataji popote anapokuwepo.

Mourihno anachotakiwa kufanya sasa ni kumjenga kisaikolojia David De Gea na kutengeneza mazingira ya kumuhakikishia juu ya kurudi kwa zama za makombe ndani ya Old T chini yake,kuja kwa wachezaji wa kiwango cha Dunia na ikiwezekana kumuongezea mshahara.

Nitafurahi kumuona David De Gea akiendelea kuwa nasi Next season hasa kipindi hichi tunachotakiwa kurudisha heshima Yetu kipindi hichi ambacho tumeanza kukisuka upya kikosi chetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…