Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Nadhani hii game ni ya Arsenal.....Karata yangu nawapa Arsenal.
 
KUELEKEA MCHEZO KATI YA MANCHESTER UNITED NA ARSENAL MZEE WENGER ASEMA HANA TATIZO NA MOURINHO NA ATAMPA MKONO!.

~Kuelekea mtanange mkali wa kukata na shoka kati ya Manchester United na Arsenal utakao fanyika Tarehe 19 siku ya j mosi (kesho), mambo yameanza hii ni baada ya Kocha wa klabu ya Arsenal kusema ana uhusiano wa kawaida tu na kocha wa Manchester United Josee Mourinho na Amesema atampa mkono kuelekea mchezo huo!.

~Itakumbukwa Kocha Arsene Wenger hakuwa na mahusiano mazuri na Kocha Mourinho baada ya kuonekana wakitoleana maneno na kusukumana hadi kumlazimu mwamuzi wa Mezani kwenda kuwa achanisha kwenye muendelezo wa michezo ya Epl Wakati arsenal walipo menyana na Matajiri wa Jiji la London Chelsea mnamo Mwaka 2014!.

~Kocha Arsene Wenger baada ya kuulizwa kuhusu kumpa mkono Mourinho alisema '' Sidhani kama ninaweza kuelezea kuhusu uhusiano wetu, atapambana kwa ajili ya Timu yake na Mimi ntapambana kwa ajili ya Timu yangu nadhani hili ndo la msingi, nitampa mkono namheshimu kama mwalimu!.

~Kocha Wenger hajawa na matokeo mazuri pindi wanapokutana na Josee Mourinho kwenye michuano ya Premier League kwani wamekutana Mara 11 Josee Mourinho kashinda Mara 5 wakiwa wametoka sare Mara 6 huku mzee Wenger akiwa hajashinda hata mchezo mmoja!.

~Arsenal Mara ya mwisho kuibuka na ushindi katika dimba la Old Trafford ilikuwa ni Mwaka 2006 Goli la Emmanuel Shekh Adebayor kunako dakika ya 86 kwenye ushindi wa goli 1_0 tangu hapo arsenal hajawahi kupata ushindi kwenye uwanja wa Old Trafford!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…