kipindi cha kwanza game ilitaka imkatae ila nadhani ni nafasi aliyokua anacheza alikua shimoni sana, that's why hata kiungo chetu kilibwana, alivoingia bastian dogo alituonesha Herrera tunae mjua, ile pasi ile dah sijui kama sitaiota.
Herrera huyu wa leo sio yule ninayemfahau....Especially first half
Herrera alikuwa shake sana first half kipindi anacheza kama CM....
CH14 Ofcourse kuna chance amekosa za wazi ila penati simlaumu sana alipiga vizur sema kuslip ndio kumemfanya kukosa
1st half alikuwa anacheza deep sana na alikuwa na mchecheto kiasi, sema alivyo ingia bastian ikawa simple kwake kucheza free, ila LVG inabidi ajifunze huyu dogo kila akichezaga timu inakuwa bora sana kuliko akikosekanaga, sijui ata watumiaje wote maana kila kiungo ana taste tofauti na mwenzake..
Kuna kipindi niliandika humu juu ya mfumo wa 4-5-1, ambapo nikasema kama pale kati: CMs wakiwa Morgan na Carrick, au Morgan na Bastian, au Bastian na Carrick; na AM akiwa Herrera huku AWs wakiwa Depay na Mata, huku Mata akiwa huru kuhama kwenye wing na kuwa kama AM, basi ushindi unapatikana kwa asilimia kubwa.
Na hicho ndicho kilichofanyika jana: Herrera kipindi cha kwanza hakuwa kama AM, alicheza na Carrick. Baada ya kuingia Bastian, Herrera akaenda kuwa AM, huku Mata akiwa na uhuru mkubwa kwenye midfield. Ukitaka kumfaidi Mata mwache awe huru.
Naamini LvG atakuwa kajifunza jana, namna ya kujenga timu pale mbele kupitia Herrera na Mata. Hili lipo wazi mno kwamba hawa viumbe wawili wana uwezo wa kuibeba timu, wakipewa msaada na CMs.
Ile inaitwa pasi ZEGEZA mkuu, wanapiga watu wachache sana katika sayari ya 3 kutoka jua😀😀
Pasi ya Herrera siyo? Ilikuwa balaa, lakini je ile ya Bastian? Ile Herrera angeshindwa kufunga, angepaswa apewe adhabu ya kufua nguo za Bastian msimu mzima! Maana ile pasi si ya sayari hii kabisa, tena hata siyo galaxy hii. Kwa ujumla haielezeki!
Hahahahaha mkuu umeona eee?? Sijui km atacheza tena yule
Chicharito mimi bado namuona anatufaa sana. Ila utampenda zaidi kwenye games ambazo bado matokeo ya ushindi hayajahakikishwa. Kwa mfano, score line iwe 1-1, hapo Chicharito anakuwa na moto sana kama super sub. Kumwingiza kwenye game ambayo mnaongoza 3-0 au 4-0 ni kumwonea tu.
Naomba sana aendelee kubaki na awe anatumika kama super sub. Kama alivyokuwa Ole Gunnar, ambaye naye alikuwa anaboa kwenye games ambazo matokeo tayari yamekaa poa.
Kuhusu jana: nilifurahishwa sana na uchezaji wa kitimu. Shaw na Darmian shikamoo zao. Shaw ka-improve sana; anapanda na kushuka tofauti na mwaka jana. Naona baada ya kuitwa sana 'fatso' na washabiki kaamua kuwaonyesha kuwa hata kama una mwili wa ukibonge unaweza fanya mambo. Darmian kwa kweli United iliwaibia Torino, wanapaswa waidai zaidi United.
Romero anazidi kuwa-prove wrong critics wake. Huku Smalling akizidi kukua na kuonyesha kwamba SAF hakukosea kumsajili kutoka Fulham. Naamini wakirudi Jones na Rojo, backline itatulia zaidi.
#WasagaSumu wataendelea kuchonga huku timu iki-keep clean sheets tu. Backline inayosemwa mbovu ndiyo imefungwa magoli machache sana kuliko timu zote EPL 😳
Inabidi performance ya jana, hususani katika kufunga ihamie EPL sasa kwa kuanza na Swansea.
#ggmu #let'sdoit