Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Summer transfer window tunahusishwa na Matt Hummels na Paul Pogba...pia beki wa Southampton Nathan Clyne, tukimpata Pogba na Hummels tutakuwa vizuri sana!
 
Mkuu we are not top 4 contender, we are th title contender. nafikiri utakuwa unatufananisha na ze goonerz

Atalinganishaje bunduki na Shetani huyo, anadhani anaweza kumuua Shetani kwa bunduki. Shetani anaibukia sehemu yoyote na wakati wowote hatabiriki....
 
Siwezi jipa ban sababu mlishinda mkitumia loopholes ya Majogoo kuwa pungufu

11 kwa 11 hunifungi Anfield

Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 13 wakati huo loserpool wakiwa 11 na likadumu mpaka mapumziko, swali kwanini hamkurudisha hilo bao moja?

Kama ingekuwa kuwa pungufu ndiyo kigezo kwanini bao la kufutia machozi lilifungwa mkiwa 10 uwanjani au unataka kutuambia lile goli la Sturridge mlipewa zawadi na David De Gea ila hamkustahili?

Isitoshe mimi nahesabu loserpool ilifungwa bao 3, ni Rooney tu aliamua kuwaondolea aibu ya kufungwa bao 6 na kugawa point 6 kwa msimu mzima.
 
Mkuu we are not top 4 contender, we are th title contender. nafikiri utakuwa unatufananisha na ze goonerz

Atalinganishaje bunduki na Shetani huyo, anadhani anaweza kumuua Shetani kwa bunduki. Shetani anaibukia sehemu yoyote na wakati wowote hatabiriki....


Maneno yote haya yanatoka baada yakuifunga LFC au vipi? Mbona mnaanza kutukosea adabu Chelsea kabla hamjaja darajani na tukayageuza hayo mashetani na kua vibwengo.... Nzi na everlenk na RRONDO siongei na nyie mpite tu juu km mashetani mekundu.....niachieni hawa waliojisahau kwa tips kidogo ya ushindi kwa LFC nisuguane nao.....lol.
 
Last edited by a moderator:
Jamaa ana excuse za kimawenge....Liver alishaingia kwenye mashine ya kuchinjia....it wasn't about red card but about tactics

Sipati picha wangefunga goli wakiwa 11 kisha red card then tuka-draw.....mane lno ingekuwa mingi mtaani

Anashindwa kufahamu kuwa kucheza rafu za kijinga mpaka kupewa kadi nyekundu ni dalili ya kuzidiwa kimchezo, mbinu za nahonda zilikwisha akaona heri ya lawama kuliko fedheha. Vijana wa OT walikuwa wanateleza kama samaki majini utamlaumu Gerrald bure timu nzima ilizidiwa...
 

Mkuu sijaiona
 
Last edited by a moderator:
Ha ha! Hao wanazi jembe lao kila msimu linawaangusha....mwaka jana liliwaharibia matumaini ya ubingwa, mwaka huu inavyoelekea, limeshawaharibi matumaini ya top 4....

Katika yoote hili jamaa sitasahau "lilivyompa" back-pass Drogba iliyowapa Chelsea Kombe kutoka mikononi mwetu
 
Mkuu sijaiona

Mkuu hivo vilikua ni vikosi vilivoumana kukamilisha msimu wa Champions league mwaka 1998/1999. Fainali ilifanyika ktk jiji la Barcelona mnamo tarehe 26 mwezi wa tano mwaka 1999 ktk uwanja wa Camp Nou na watu 90,245 waliingia uwanjani kutizama mpambano huo...Huku Manu viungo wake nguli wa kati Paul Scholes na Roy Keane wote wawili wakiwa suspended kwa hiyo fainal....Munich walipata goli la mapema sn mnamo dakika ya 6 lililofungwa na Mario Basler na kudumu kwa muda wote mpk mpira ulipotaka kuisha.


Katika dakika ya 67 mzee wa bahasha ya kaki alianza kufanya sub za nguvu kwa kumtoa Jasper na kumuingiza mchezaji mwenye sura ya kitoto Teddy Sheringham, na mnamo dakika ya 81 alimtoa Andy Cole na kumuingiza Ole Gunnar Solskjaer...na dakika 90 zilikwisha ManU akiwa kalala na ktk zile dakika za nyongeza 3, Teddy Sheringham aliisawazishia ManU goli ktk dakika ya 90+1 na dakika ya 90+3 Ole Gunnar Solskjaer akaipataia ManU goli na pili na la ushindi na ManU kua bingwa wa Ulaya. Mwamuzi wa mchezo huu alikua babu upara toka Italy, Pierluigi Collina.

Mchezo huu unanikumbusha kitendo cha Samuel Kuffour aliekua akitengeneza ngome ngumu ya B Munich kulia sn uwanjani baada ya kufungwa.


Wengi hawawezi kusahau miujiza ya mpira huo na mpira ni dakika 90 siku zote, zingine zote hua ni mbwembwe tu.
 
Kama namuona kuffor siku hiyo baada ya game alipiga piga mkono chini uwanjani mpaka akatengeneza kashimo! kiukweli tulipora coz kuna shuti alipiga basler ikala mtambaa panya duh utumbo ulikuwa unapanda na kushuka.
 
Mmoja wa wachezaji jaap stam akihojiwa akisema hivi: ki ukweli hili kombe hatukuchukua, tumefanya kupora!

Kama namuona kuffor siku hiyo baada ya game alipiga piga mkono chini uwanjani mpaka akatengeneza kashimo! kiukweli tulipora coz kuna shuti alipiga basler ikala mtambaa panya duh utumbo ulikuwa unapanda na kushuka.


Ni kweli mlipora aiseee......maana Munich walijua kazi imeshakwisha na wakaanza kutoa majembe yao nje....nakumbuka Mario Basler alitolewa katika dakika za 90 huku akijua kua kombe letu na ngoma imekwisha.....alivo kaa tu chini Teddy Sheringham akatupia goli moja fasta....hajakaa sawa goli la pili bench lote la Munich likazimia...... Kweli huo ulikua ni uporaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…