Mkuu wa chuo
JF-Expert Member
- Feb 3, 2011
- 7,626
- 5,346
Saa nyingine inaudhi sana mkuu, Kwa mfano yule Falcao ametanguliziwa fresh halafu anapiga nje... yaani anakosa sana zaidi ya kufunga sana ana kiwango kama cha Welbeck tu Toka atue Manchester United... Man U hata akicheza na timu ipo namna gani, game yake inakuwa ngumu...Jana baada ya Big Sam kukosa point 3 zote kuna uchambuzi niliuona ktk mtanadao namna ManU walivo wabovu....maana jamaa anahoji haiwezekani mbele ukawa na RVP na Falcao nyuma kidogo ukawa na Di Maria, Rooney na Januzaj alafu unahangaika kufunga au kupata draw, yani unakuja kupa sare dakika za mwisho kwa shida....kweli ni shida hii timu aisee.
Manu sio wabovu sana tatizo ni team selection na tactics mbovu za kocha
Saa nyingine inaudhi sana mkuu, Kwa mfano yule Falcao ametanguliziwa fresh halafu anapiga nje... yaani anakosa sana zaidi ya kufunga sana ana kiwango kama cha Welbeck tu Toka atue Manchester United... Man U hata akicheza na timu ipo namna gani, game yake inakuwa ngumu...
Kikosi ukiangalia kwa macho ni kikali, lakini kiwango chao cha uchezaji hawana tofauti na zile timu cha chini yake... Van Persie ni striker mkali lakini kwenye top ile ya wafungaji hayumo... Wanamwangalia mtu anapiga danadana halafu anatupia, jana waliniudhi kama wale wa Ghana walivyokosa penati pamoja na kipa wao ambae hakupangua hata penati moja...
kwa kikosi hicho cha Man U ilitakiwa wawe wanasumbuana na chelsea pale juu... lakini eti wanagombea nafasi ya 3 na 4...
Sawa wataalamu...
Siyo kazi ndogo kuvaa viatu vya SAF kama tunavyofikiri humu...
Hadi sasa leo la kurudi UCL mwakani bado lipo...uwezekano wa kumaliza top 4 bado upo...na hii ndiyo realistic target ya timu....hayo mambo ya kusema LvG alichukua makombe msimu wa kwanza katika timu alizopita, siyo ya kuyafikiria katika EPL...
Pamoja na mapungufu yake ya kibinaadamu, bado namwaminia LvG...tukianza fukuzafukuza ya makocha, timu haitokuwa stable kwa misimu 10 ijayo...
Tulizoeshwa raha sana na SAF, sasa tuonje shubiri kidogo ili tupate utamu misimu miwili ijayo..
Yangu ni haya tu..
Selection ipi mkuu unayotaka? Uko na RVP, Falcao, Di Maria, Januzaj na Rooney? mkuu mi nakubaliana na mdau mmoja hapo juu kwamba kwa kikosi cha ManU jinsi kilivyo ilikua inapaswa awe anatifuana na Chelsea lkn sasa ndo kwanza anagombania no3 na Soton! hii inashangaza kwa kweli km ilivoshangaza jana mmeweka full mkoko lkn mnashindwa kupata goli! Mnapata goli kwa taabu kweli..........nini shida iliopo kwa ManU? Hebu nisaidieni jamani maana haiwezekani na kamwe haitowezekana unakua na watu wazuri alafu unafanya vibaya!
Wachezaji wanachezeshwa out of position (Di Maria,Rooney) then Ander Herrera huyu ndio best creative midfielder tuliye naye huyu ndio anapaswa kucheza kiungo Rooney acheze no 10 au striker RVP/Falcao mmoja aanze benchi.Tulivyoanza ligi Di Maria alicheza winger,Rooney no 10 na Herera alicheza kiungo wote Di Maria,Rooney,Herrera walishine tulikuwa tunafunga magoli na kutengeneza nafasi nyingi tatizo lilikuwa defence now defence iko stable Rooney anachezeshwa kiungo,Di Maria forward,Herrera benchi kabisa
Mkuu nakubaliana na wewe kabisa ktk maelezo yako lkn nashindwa kuelewa kwanini Nzi hayaoni haya? Bora ya RRONDO kaona lawama zote atupiwe Van Gaal na mimi naona Van Gaal au bench la ufundi linashida. Kabla ya mchezo wa jana niliona nafasi kwa ManU kua ktk nafasi ya pili kumekaribia maan km wangeshinda jana basi pengo la points kati ya Man City na ManU lingekua ni 3, alafu Tarehe 1 mwezi ujao City anakwenda kwao Liverpool huo mchezo nahisi city atapoteza na hapo ManU na City wangekua sawa kwa points na ukumbuka kua huyu City bado hajaja hapo OT. kitu amabacho akija hapo lazima City afungwe maana mchezo wao wa kwanza ManU akiwa ktk kiwango kibovu, City alimshinda ManU kwa makosa ya beki Chris kitu ambacho km ManU wangekua wote kamili uwanjani City alikua anapoteza ule mchezo....kwa hiyo nilivoona hivo nikaona ManU wana nafasi kubwa ya kua nafasi ya pili....lkn baada ya hapo naona vijana wa Big Sam wanamuabisha tena Van Gaal....ni shida mkuu. .
hizi timu zinatakiwa kujifunza kwa chelsea km zinataka kufikia hatua nzuri.
Mkuu Rooney kucheza nafasi ya kiungo ni jambo zuri sn km anamudu kufanya hivo na ni kweli Rooney ata wakati wa babu Alex alikua anacheza km Striker lkn alikua anashuka chini na kuchukua mipira na kuipeleka mbele na wakati mwingine huwachezesha wenzake na ndivo huyu Van Gaal anatumia uwezo wa Rooney kumpanga ktk hiyo nafsi kwasbabu anamudu vzr.
Kwa game ya jana Di Maria alicheza nafasi ya kiungo ingawa alipangwa katikati lkn hakucheza km forward kwasababu mbele yake kulikua na Falcao na RVP. Sioni km kwa kupanga hivo ni makosa kwasababu hii inasaidia sn timu ikiwa na wachezaji wa aina hii wakiwa wanashambuliua wanakua na ujuzi na uwezo mkubwa kwasababu ni nafasi ambazo ndio wanauzoefu zaidi.
Antonio Valencia ktk taifa lake alikua anacheza Striker wa katikati, alipokuja ManU Mzee Alex alimpanga kucheza winger wa pembeni na alifanya vzr tu na siku hizi Van Gaal anampanga huyo Valencia beki wa pembeni kulia na anafanya vzr anakaba na anapanda mbele anaingiza klosi nzuri na amewaweka bench kina Rafael. Mbona hili haulizungumzii? Kuna shida ingine mkuu na wachezaji hawajitumi huo ndio ukweli.
Acha unafiki...sasa downfall ya United wewe inakuuma nini? Si unapaswa ufurahie kukosa wapinzani ili uchukue ubingwa ama?!?
LvG ni binaadamu; hata SAF alichemsha mara nyingi kupanga timu...
Pamoja na kiburi chake, LvG ni mtu sahihi kuiweka timu sawa...hayo mengine ni mapito tu...
Ati nini?!? Doh! United ijifunze kwa rentboys? Acha masihara chifu...
Kuongoza ligi mnaanza kujiona mpo on top of English football?!
Yaani nyiye bado sana, labda miaka 200 ijayo...United itarudi mahala pake pa siku zote...
Rentboys zaidi ya kuongoza ligi, haina chochote cha kuishinda United! Sasa unataka United ijifunze nini kwa rentboys?!? Kuongoza ligi?!? Been there, done that..
Kucheza kiungo Rooney kuna hasara kubwa kuliko faida,mpange kiungo kama huna option but tuna Herrera ambaye mwanzo alicheza vizuri,Rooney alicheza vizuri akicheza no 10 na alikuwa anafunga magoli.Falcao/RVP wanakosa magoli ambayo Rooney angeyafunga.Ukicheza na Stoke/West Ham ni timu zinazocheza mpira wa nguvu sana but kocha anampanga Januzaj while Mata na Fellaini wanakaa benchi.Game ya jana kocha alichemsha sana,kama tungefungwa mashabiki wangemzomea
Haya ndio matatizo ya mashabiki wa humu Jf. Pale mtu anapotoa mawazo yake kwa uhuru km mpenzi wa mpira mnaanza kumuita mnafiki mara sijui nini....ndio maana mnajifungia ktk thread zenu kwasababu sio wapenzi wa mpira.
Baadhi ya Wachambuzi wa soccer baada ya matokeo ya Man City na ManU na Arsenal na Liverpool wengi wamesema ili hizi timu zifikie hatua nzuri na nafasi nzuri msimu huu lazima wajifunze kutoka kwa Chelsea. Maana huwezi mchezo huu ukapata matokeo mazuri alafu mchezo ujao ukaboronga mbaya.
Haya ndio matatizo ya mashabiki wa humu Jf. Pale mtu anapotoa mawazo yake kwa uhuru km mpenzi wa mpira mnaanza kumuita mnafiki mara sijui nini....ndio maana mnajifungia ktk thread zenu kwasababu sio wapenzi wa mpira.
Baadhi ya Wachambuzi wa soccer baada ya matokeo ya Man City na ManU na Arsenal na Liverpool wengi wamesema ili hizi timu zifikie hatua nzuri na nafasi nzuri msimu huu lazima wajifunze kutoka kwa Chelsea. Maana huwezi mchezo huu ukapata matokeo mazuri alafu mchezo ujao ukaboronga mbaya.
Wachezaji wanachezeshwa out of position (Di Maria,Rooney) then Ander Herrera huyu ndio best creative midfielder tuliye naye huyu ndio anapaswa kucheza kiungo Rooney acheze no 10 au striker RVP/Falcao mmoja aanze benchi.Tulivyoanza ligi Di Maria alicheza winger,Rooney no 10 na Herera alicheza kiungo wote Di Maria,Rooney,Herrera walishine tulikuwa tunafunga magoli na kutengeneza nafasi nyingi tatizo lilikuwa defence now defence iko stable Rooney anachezeshwa kiungo,Di Maria forward,Herrera benchi kabisa
Kuwa mpenzi wa soka na kutoa mawazo huru hakuna mahusiano yoyote....
Kwa sababu kiukweli United haina cha kujifunza kutoka kwa rentboys...rentboys washukuru timu nyingi haziko vizuri msimu huu..ila mpira wao wa kawaida sana...mpira wao umezidiwa hata na uliokuwa ukipigwa na Liverpool msimu jana...
Na hakuna mahala popote panaposema ni lazima mtu kuchangia kwenye majukwaa yote..nitachangia jambo ambalo nalitaka mimi...sina haja ya kuchangia mahala ili nionekane ni mpenzi wa mpira ebo!
Hao wachambuzi wa soka ni binaadamu kama sisi, hawana authority ya kuwa quote kama wao ni miungu watu...waliyoyasema ni mawazo yao kama yangu na yako...
Ndiyo maana nilisema haya na mawazo yangu...sasa kama hukubaliani nayo ni sawa kabisa...lakini siyo kuniambia sijui wachambuzi wa soka!!! Wachambuzi wenyewe kina Merson, Jamie na Chogo?!?
Nilipita kuwasalimu tu humu ndani lkn naona mnajaa upepo kweli. Mtasubiri sn safari hii zama zenu kwishiney.....shaja na mongo gwa le Simiyu. Babu Alex wamchezo
Nilipita kuwasalimu tu humu ndani lkn naona mnajaa upepo kweli. Mtasubiri sn safari hii zama zenu kwishiney.....shaja na mongo gwa le Simiyu. Babu Alex wamchezo
Paddy McNair kasaini mkataba hadi 2017...
Afadhali sisi tulikuwa na zama sasa zimeisha nyinyi hamjawahi kuwa na zama wala enzi....no history,no class...plastic fans damn rentboys!