Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Msijidanganye kuwa mna timu ya kugombea ubingwa, hizi ni nguvu za soda tu

Teh teh teh!! Muda mwingine ni heri kuzuia jazba na kukubari yaishe maana ukijikakamua unaweza toa maneno ya kushangaza sana...kwani team zinazozidi fanya vibaya hazihitaji hizo nguvu za soda au kitu gani kinawashinda kupata hizo nguvu za soda?
 
Reactions: Nzi
Welcome back,
Tatizo letu kubwa ni beki na kila wiki beki anaumia sidhani kama tumeweza kuchezesha same back four kwenye game 3 mfululizo.I hope kama tusingepata majeruhi mabeki wangeelewana

Welcome back? nipo hapa siku zote, nimepunguza kucomments tu mkuu. Anyway, tukizingatia sababu ya majeruhi basi hata sisi tunaweza kurudi juu na maybe kugombea ubingwa kama majeruhi 10 wote wakirudi. Lakini kama unavyojua akirudi wetu mmoja wengine 2 wanaingia wodini. Kama vile kuna mkono wa " Manyaunyau" kambini kwetu
 
Dah! rubaman anatia huruma :becky::becky::becky:

Kuna jambo uwa linanishangaza sana, haswa kwa pundits wa UK.

United ikishinda games bila kucheza vizuri, basi utawasikia wanavyopondea na kusema eti siyo United's way of playing; oh, timu haina identity, oh, inacheza kama timu ya walevi (a pub team) n.k. Wanasahau 'winning ugly' ilikuwa ni moja ya philosophy ya timu hata chini ya SAF.

Lakini mpiga domo Maureen akipaki basi na kushinda games, anaonekana master tactician:A S 13::A S 13::A S 13: Wenger akishinda kwa kucheza vibaya, utawasikia eti hivyo ndivyo inapaswa kuwa wakati mwingine siyo kucheza tiki-taka kila mechi.

Yaani kwa UK, nafikiri United ni timu inayoongozwa kuchukiwa na waandishi wa habari na pundits wengi..

Ni ajabu na kweli...
 

Manchester United ni timu inayochukiwa UK ? Utakuwa unatania ama unajisahaulisha. Manchester United ni timu ya FA administration,mnabebwagwa hata msipostahili.Timu inayochukiwa England ni Arsenal tu, rekodi haisemi uongo.
 
Manchester United ni timu inayochukiwa UK ? Utakuwa unatania ama unajisahaulisha. Manchester United ni timu ya FA administration,mnabebwagwa hata msipostahili.Timu inayochukiwa England ni Arsenal tu, rekodi haisemi uongo.

Bado mna mengi ya kusema.
Endeleaaaaaaaaa...........!.
Bado wachezaji wanaochukiwa
Kocha anayechukiwa
Uwanja unaochukiwa
Wakurugenzi wanaochukiwa
............
...........
............
.........
Endeleeni jama orodha isiisheeee ili sababu zikubalike!.
 
Reactions: Nzi
Magoli ya kuvizia ... ... khe he khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Manchester United ni timu inayochukiwa UK ? Utakuwa unatania ama unajisahaulisha. Manchester United ni timu ya FA administration,mnabebwagwa hata msipostahili.Timu inayochukiwa England ni Arsenal tu, rekodi haisemi uongo.

Kama hujui jambo uliza ufahamishwe, ... kwanza ujue ndani ya FA kuna uingereza sana (ubaguzi) ndio maana Rio ferdinand amesema ye akimaliza career yake basi anataka aingie kwenye administration.
Unaposema Man utd inabebwa huo ni ushabiki wa vijiweni. ...katika vilabu ambavyo vimekutana na adhabu zisizostahili kutoka FA basi man utd kakutana nazo nyingi sana...mpk Rio alishawahi kusema kuwa fine wanazopigwa man utd players wakifanya kosa ni kubwa tofauti na mchezaji wa timu nyingine akifanya kosa kama hilo.
Pia fahamu kuwa man utd haipendwi sana hapa uingereza kama inavyopendwa nje ya UK na hasa bara la ASIA, tofauti na vilabu kama Madrid na Barcelona ambavyo vinapendwa sana huko kwao, na hii ni kwa sababu ya FA walianzisha campaign ya 'support ur local team'..na ujue tu mji wa Manchester una team tatu kubwa unazozijua wewe ambazo ni man utd, man city na Wigan lkn timu ya wakazi wa pale wanayoishabikia miaka yote na yenye wapenzi wengi Ktk mji ule (local team) ni man city, hivyo usifikiri man city ni team ya juzi.
Arsenal mchawi wenu ni meneja wenu na sera zake ambazo mpk yule shareholder wa kirusi kazichoka. ...mara ngapi wenger anapewa pesa lkn hataki kununua wachezaji wenye majina kwa kuogopa gharama?....
 
Reactions: Nzi
Manchester United ni timu inayochukiwa UK ? Utakuwa unatania ama unajisahaulisha. Manchester United ni timu ya FA administration,mnabebwagwa hata msipostahili.Timu inayochukiwa England ni Arsenal tu, rekodi haisemi uongo.

Mimi nimeongea kwa kuangalia nini pundits na waandishi wanaongea dhidi ya United.

Unavyoleta stori zako za vijiweni eti United ni timu ya FA, ina maana David Dein (aliyekuwa mmiliki wa goons na kigogo wa FA hadi mwaka 2007) naye alikuwa anaisaidia United kushinda makombe ama?!?
 

Dah! Chifu asante sana kwa kuliweka hili jambo sawa.

Niseme jambo dogo tu, ni kuwa unaongelea the Greater Manchester. Maana kuna wajuaji humu wanaweza kupinga kuwa Wigan haipo Manchester


Watu wanaleta stori za vijiweni kwa Mtogolo kuongelea nini kinachoendelea UK!!! Mimi nimewaambia kuwa United ni timu inayoongeza kuchukiwa na UK Media, yeye analeta stori za kwa Mtogolo!! Mfano mdogo sana, angalia tu platforms za social media za United (Twitter, Instagram na Facebook) uone jinsi watu walio UK wanavyoiponda United, huku mashabiki wengi wa United wakiwa toka nje ya UK. Mfano mwingine mdogo, kuna siku nilienda kuangalia game kwenye Irish pub katika mji mmoja, kulikuwa na game ya United vs. Everton, jamaa wasivyoipenda United, waligoma kuonyesha game eti kisa kulikuwa na Rugby match :becky::becky:

Halafu kinachowauma na kuwaumiza zaidi mashabiki wa Shitty timu yao siku zote inajaribu kujifanya ni kubwa zaidi ya United. Walivyoshinda EPL (kwa goli la dakika za mwisho la Aguero) Manchester kulikuwa kama kumechizika. Ila Shitty siku zote watabaki kuwa Minnows tu kwa United. Hizo Arab monies zitakatika baada ya mwarabu kupata hobbies mpya...sasa waarabu hobbies zao ni kumiliki timu za mpira. Inaweza fika siku wakapata hobbies za kusafiri kwenda Mars n.k. Hapo ndipo Shitty watakasaga meno :becky::becky:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…