Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Either wachezaji wanamgomo na kocha au kocha ana mgomo na maboss kwa kufundisha mbinu za kufungwa

Ukiachana na fact ya kuwa nyumbu hakuna team
Kwa jicho la haraka utagundua wachezaji wana mgomo na hari ya uchezaji imeshuka sana. Kwa mtazamo wangu nadhani matajiri wa timu wamechangia na m Carrick pia kachangia.

Ikumbukwe mwaka jana utd ilianza upya kusukwa kwa kununua wachezaji wapya hasa safu ya ushambuliaji na Amorim alifanya kazi kubwa sana ya kuwaondoa wazembe na wachezaji wasio na impact kwenye timu. Ule muunganiko wa Sesko, Mbeumo, Cuhna na Amad ulishafanya kazi vizuri tu na ulielewana. Leo INOES wakaamua kumrudusha Rashford haikuishia hapo Carrick naye kaamua kumuanzisha kikosi cha kwanza huku akiwaweka bench wachezaji waliomopigania msimu uliopita. Kikawaida tu nilazima wachezaji morali yao ishike kwa vyovyote vile.

Hao wachezaji sio wajinga. Ni nani asiyejua kuwa utd ilikuwa inaharibiwa na wachezaji kama Pogba, Martial na Rashford? Hawa wawili walishaondoka akabaki Rashford, alipokuja
Amorim akamhmuondoa eti leo Carrick anakuja kumuanzisha kikosi cha kwanza kila mechi kwa impact ipi aliyonayo?

Binafsi naamini utd hatutashinda mechi yeyote kuanzia sasa na hata tukileta kocha mwingine hatuwezi toboa shida yetu ni Morali ya wachezaji imeshuka sana baada ya baadhi ya wenzao kula bench ili muingereza acheze.

Huu unaweza kuwa msimu mbaya wa utd kuwahi kutokea na huenda tukashuka daraja ikiwa Carrick hata ongea na wachezaji wake na ikiwa hatomuweka Rashford bench. Kwa sababu ili Rashford aanze ni lazima kati Mbeumo, Cuhna au Seski aanzie bench hii inawakatisha tamaa kwa hawa vijana waliopigania timu.
 
Unazunguka tatizo badala ya kulisema.

Timu mbovu.

Sesko tangu asajiliwe anakaa benchi haiwezi kuwashangaza leo.

Maino ailkua anawekwa bench siku hizi anaanza kwanini wachezaji wasimpende kocha badala yake mgomo uje kisa Sesko? Ambaye kuanzia benh ni kawaida yake.

Na angalau Carrick anamuanzisha baadhi ya mechi.

Hii timu ni mbovu mkipata matokeo mnasahau ukweli. Kama umeangalia mechi ya jana na hitimisho ni wachezaji wana mgomo basi na mashabiki mnachangia hii timu kutoenda mbele
 
Either wachezaji wanamgomo na kocha au kocha ana mgomo na maboss kwa kufundisha mbinu za kufungwa

Ukiachana na fact ya kuwa nyumbu hakuna team
Hivi ukiangalia mechi zao hawa watu unahisi kuna mgomo?

Uwezo ndiyo umefika mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…