Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Na spurs nae tayari ameshampiga Bodo goli 2, Fainali Man Utd tukikutana na Spurs mechi itakua ngumu sana, maana wote kwenye ligi tumezingua, hivyo wote tumewekeza nguvu zote kwenye Europa ili tupate nafasi ya kushiriki Uefa msimu ujao.
 
Maisha yanaenda kasi sana, siku hizi Maguire anapiga chenga na ukija kijingajinga anakufinya au anakupiga tobo kabisa.
Amorim kumchezesha kama foward imesaidia sana kumuongezea confidence huyu mwamba.
 
Wanangu mnawajua bolibao?


Huyu kocha valverde nilimpenda toka akiwa Barcelona

Huruma manchester united zikipungua sana leo mnakula tano uku bruno akila umeme
Kanji unajua sana kutabiri kinyumenyume.
Kipindi cha kwanza tayari huyo Bilabao wako kashachezea goli 2 na ile kadi nyekundu uliyoitabiri pia wameshapewa kama kifungashio, tunasubiria kipindi cha pili tumalizie hizo goli 3 ili utabiri wako uende sawa.
 
Hawa jamaa hawajakosea kabisa kujiita Bilabao.
Ila wachezaji wetu na wenyewe hawajui kabisa kutumia fursa vizuri, hii mechi ilikua ya kushinda zaidi hata ya goli 5 halafu second leg inakua ni mechi ya kukamilisha ratiba tu, mechi ya marudio utakuta yanajirudia tena yaleyale ya Lyon, kipindi cha kwanza tu Bilabao wanarudisha goli zote 3 halafu mashabiki tunaanza kuteseka na high blood pressure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…