Manara Akanusha Taarifa za Kurejea Simba, Asema Moyo Wake Upo Yanga

veyra

Member
Joined
Aug 31, 2025
Posts
19
Reaction score
29
Mkurugenzi Mtendaji wa Manara TV na mwanachama wa Klabu ya Yanga SC, Haji Manara, amekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni zikidai kuwa anatarajia kurejea kufanya kazi katika klabu ya Simba SC.
Akizungumza kupitia Manara TV, Manara alisema kuwa taarifa hizo si za kweli na kwamba bado anaendelea kuwa mwanachama na mshabiki wa Yanga SC.
“Nimeona na mimi nimetumiwa mitandaoni kwamba naenda tena kufanya kazi Simba, na watu wengi mmeniuliza. Jawabu langu ni uongo, sina mpango huo kwa sasa. Mimi naendelea kuwa mshabiki na mwanachama wa Yanga, nalipa ada za uanachama na moyo wangu uko Yanga,” alisema Manara.
Aliongeza kuwa aliwahi kufanya kazi Simba lakini hawezi kurudi tena, huku akiwataka wanachama na mashabiki wa Yanga kupuuza taarifa hizo ambazo zina lengo la kumchafua, hasa kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba ambako anagombea nafasi ya Udiwani Kariakoo.
Aidha, Manara amewasihi wanachama na mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kushiriki kilele cha Wiki ya Yanga pamoja na kununua jezi za klabu hiyo akibainisha kuwa zina ubora wa hali ya juu.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…