Manabii wasifumbiwe macho wanapotukana mamlaka

Manabii wasifumbiwe macho wanapotukana mamlaka

Unajua maana ya neno nabii?
Nabii umwambia mtu ujumbe toka kwa Mungu. Mara nyingi viongozi wengi hawapendi na wengine huwageuka manabii na hata kuwaua.
Haisaidii. Kubali ujumbe au subiri cha moto.
 
Kwani kakobe alikosea wapi jamani? Soma mithali,28:1--20
Mithali,29:12---
Inasema mfalme akisikiliza uongo watumishi wake wote watakuwa waovu.
Askofu Kakobe yupo sahihi sana maana amesimama kwenye nafasi yake kama wakili wa siri za Mungu.
1wakorintho, 4:1----
halleluya halleluya kumbe wanatuibia sadaka wameacha kukemea uzinifu wanakazi ya kuhubiri siasa ya kaisari muachie kaisari
 
Habari wakuu,

Tunaomba Serikali isifumbie macho manabii wote wanaotukana mamlaka ambazo zimewekwa na watu wengi kwani chaguo la wengi ni chaguo la mungu.

Kumeibuka na tabia mbaya ya viongozi wa dini kutafuta kiki kwa kutukana mamlaka ili wapate watu kwenye ibada zao ili kuongeza sadaka kwan watanzania wengi wanapend umbea.

Juzi tumeshuhudia kiongozi mmoja wa dini akimtukana na kumkebehi Mh rais. Naomba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimchukulie hatua kali kwani kitendo cha kumdhalilisha rais ni sawa na kutukana watanzania wengi tuliomchagua kwa kura nyingi za upendo pia ni sawa na kuitukana nchi yetu.

Naomba ninukuu maneno ya bibilia Mith 14:12 “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti”
Mathayo 7:15-16 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali, mtawatambua kwa matunda yao”.
Mathayo 24:11-13 “Na manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi na kwasababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka”.
Ungesema manabii wa uongo, maana nabii wa ukweli hawezi kutukana mamlaka iliyowekwa na Mungu.
 
....... Serikali isifumbie macho manabii wote wanaotukana mamlaka ambazo zimewekwa na watu wengi kwani chaguo la wengi ni chaguo la mungu.
ni kweli kabisa... chaguo la 2015 lilikuwa chaguo la huyo uliyemtaja hapo juu. ndiyo maana mambo yapo shaghalabaghala.
tusubiri 2020 labda sasa tunaweza kupata chaguo la Mungu wa kweli.
 
Mleta hoja usijidanganye na kuwadanganya wengine kuwa tawala zote zatoka kwa Mungu! Sio kweli hata kidogo kutokana na ushahidi huu wa herode na waisrael enzi za utumwa alivyokuwa anashindana na Mungu kuhusu kuwaachia waisrael ili waende nchi ya ahadi. Herode alikuwa mfalme na hakuwa chaguo la Mungu. Na mifano ipo mingi tu. Hivyo usimtumie Mungu kujustify na kuhalalisha dhuluma juu ya watu wa Mungu.
Kwa taarifa yako hata wanasiasa ni manabii na wanahubiria wafuasi wao habari za uongo nao uwakatae pia.
Umebonyeza buttons zisizo sahihi boss wangu. Ni buttons za FARAO siyo HERODE. Tupo wote.
 
Umejua hayo baada mshika akili zako kuambiwa ukweli? Aliposifiwa kinafiki (Zimbabwe ) ukafurahi mpaka ukatokwa machozi, leo kawapa za uso mmekuwa kama umekatwa mkia bila ganzi (sorry mkia wa binadamu ulishaga perish )
Punguza kumchapa makofi ya macho huyo bendera. Utamuua kwa jakamoyo.
 
"chaguo la wengi ni
chaguo la mungu" sasa leo nimeelewa. Umekili kwa kinywa chako kuwa huyu ni chaguo la mungu na sio Mungu ndio maana mambo yake kila siku yanaibua maswali. Mwambieni akatubu. Afu siku nyingne unaposema fulani katukana dola ebu jaribu kuorodhesha na matusi ambayo ametukana. Kwahyo naomba uorodheshe japo matusi manne (4) aliyotukana kakobe.
 
Unaaibisha nickname yako, programmers hua hawana thinking capacity low namna hii.
 
Toka lini chaguo la Mungu kukawa na kampeni na rushwa na mapigano hadi watu wakabaki vilema.
Huyo ni chaguo la tume.
kwani huyu jamaa kasema chaguo la Mungu au la 'mungu' ? Soma vzur post yake afu tafuta tofaut ya haya maneno.
 
Habari wakuu,

Tunaomba Serikali isifumbie macho manabii wote wanaotukana mamlaka ambazo zimewekwa na watu wengi kwani chaguo la wengi ni chaguo la mungu.

Kumeibuka na tabia mbaya ya viongozi wa dini kutafuta kiki kwa kutukana mamlaka ili wapate watu kwenye ibada zao ili kuongeza sadaka kwan watanzania wengi wanapend umbea.

Juzi tumeshuhudia kiongozi mmoja wa dini akimtukana na kumkebehi Mh rais. Naomba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimchukulie hatua kali kwani kitendo cha kumdhalilisha rais ni sawa na kutukana watanzania wengi tuliomchagua kwa kura nyingi za upendo pia ni sawa na kuitukana nchi yetu.

Naomba ninukuu maneno ya bibilia Mith 14:12 “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti”
Mathayo 7:15-16 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali, mtawatambua kwa matunda yao”.
Mathayo 24:11-13 “Na manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi na kwasababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka”.
Unatofauti gani na gaidi???
 
Back
Top Bottom