Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Msanii wa muziki singeli Man Fongo amesema anakumbuka alipoanzia muziki wake kwa kuimba nyimbo za vigodoro uswahili na ipo siku atarudi uswahilini kuwaimbia mashabiki zake.
Akiongea kupitia eNewz amesema singeli ni muziki wa watu masikini na watu wa hali ya chini na umetokea uswahilini.
Amesema anakumbuka mwanzo alipokuwa akiimba uswahilini alikuwa analipwa hela ndogo hadi elfu ishirini pia kulikuwa na misukosuko mingi ikiwemo kushikiwa mapanga na kuwekewa mawe aimbe hadi asubuhi.
Hata hivyo Man Fongo anasema zamani alipokuwa anaimba muziki wa singeli alikuwa anakuwa na watu mbalimbali wa uswahilini waliokuwa wakimfuata nyuma hali iliyopelekea mpaka watu kuhisi kwamba ni vijana wa panya road japo walikuwa mashabiki.
Mambo hayo amesema akiyakumbuka anatamani siku hiyo ifike arudi uswahilini na kuendeleza show zake za kwenye vigodoro.