Mamonita mnaotusumbua sana madarasani

Mamonita mnaotusumbua sana madarasani

Smartbeing

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2014
Posts
323
Reaction score
426
Umofia kwenu,

Leo nipende kuleta kero ya baadhi ya mamonita madarasani. Hii inahusisha mamonita wa shule za kata hadi zile za private ambao kwa kweli wanatumia nafasi na madaraka yao vibaya. Tunafahamu kuwa ninyi ni viongozi wetu wa madarasa lakini tunaona kuwa kuna mambo mnahitaji kujua.

Mosi, mmekuwa mamonita sio kwa sababu mna akili kuliko wote darasani au mnajua sana kuongoza, hapana wengine ni kwa sababu tu mmeteuliwa na mwalimu wa darasa kutuongoza na wengine ni watoto wa walimu tu na pengine angeweza kuchaguliwa mwingine kama tungepiga kura vizuri sema tu mara nyingine tunakuwa hatuna option ya kuchagua.

Pili tabia yenu ya kutuziba midomo hatupendi. Mara nyingine somo darasani linakuwa zuri tunapenda kujibu maswali au kumuuliza mwalimu lakini hampendi tufanye hivyo mnapenda muulize wenyewe na mtuulizie hata yale ambayo mnadhani ndo maswali yetu kumbe sio.

Tatu kutulazimisha tuwafanyie majukumu yenu mfano kuwaandikia notisi ambazo ni jukumu lenu, kuwahi namba kwa ajili yenu halafu hamna shukrani.

Finally niwaombe viongozi wa madarasa muache kunyanyasa wenzenu, na tukiwaeleza ukweli muache kutuandika kwenye listi ya wapiga kelele. Have a good day

NB: Sio viongozi wote wa madarasa ni wabaya wengine, huwa wanakubali hata kuchapwa kwa kosa letu ili mradi wasitutaje tukizingua darasani.
 
Ukute mwalimu mwenyewe ndiye anawaagiza vilanja na mamonita wake wawe wanafanya hivyo.
Angalia tu wanavyo hamishwa hamishwa madarasa na wengine kunyang'anywa u-monita!!
Nimecheka kweli, inaonekana wewe umekaa shuleni muda wa kutosha hivyo unafahamu yanayoendelea ktk madarasa mengi
 
Unamaanisha ambao hawajaelewa huu uzi au?
HAPANA hawa ni watoto kabisa tena wa primary
sijui nani kawapa smartphone
wanashusha hadhi ya jukwaa
story haina fasihi / wala fumbo, wala kilijojificha
tafadhali katika maboresho ya jamii Forums haya yaangaliwe na
kitufe cha "Dislike' kiwepo tuwe tunachuja Mada ziinazojazwa jukwaa
 
nimekuja haraka nimjue huyo mamonita nilijua ni mchuchu mkali kumbe unazungumzia Monitor c2pdy
 
HAPANA hawa ni watoto kabisa tena wa primary
sijui nani kawapa smartphone
wanashusha hadhi ya jukwaa
story haina fasihi / wala fumbo, wala kilijojificha
tafadhali katika maboresho ya jamii Forums haya yaangaliwe na
kitufe cha "Dislike' kiwepo tuwe tunachuja Mada ziinazojazwa jukwaa
Bronze member, hope mawazo yako yatafanyiwa kazi, maana sio lazima kila kitu kieleweke kwa kusoma haraka, vingine vinahitaji kufikiria zaidi
 
Back
Top Bottom