BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Kwa muda wa takriban miezi miwili kumekuwa na malalamiko mfululizo ya Wananchi kuhusu wamiliki wa Mabasi kupandisha nauli bila kufuata utaratibu ingawa sababu wanayoitaja ina umuhimu kwakuwa ni kweli bei za mafuta zimekuwa zikipanda kila wakati huku nauli zikibaki palepale.
Pamoja na hilo bado Mamlaka zinapaswa kuingilia kati na kupanga jinsi suala hilo linavyopaswa kuwa kwasababu bila hivyo mambo mengi yataenda bila utaratibu na kuathiri mfumo wa maisha na hali za Wananchi pamoja na uchumi wa Nchi
Lakini cha kushangaza hadi sasa Mamlaka hazijachukua hatua stahiki zaidi ya kutoa matamko ya kuonya watakaopandisha nauli, jambo ambalo halijaleta matokeo chanya kwasababu upandishaji nauli bado unafanyika na wananchi wanaendelea kuumizwa na hali hiyo.
Ni wakati sasa Mamlaka zioneshe uwajibikaji katika suala hili kwa kuchukua hatua ikiwemo kufungia mabasi yanayopandisha nauli blla kufuata utaratibu lakini pia liharakishe uamuzi wa namna ya kukabiliana na gharama za uendeshaji kwa wamiliki wa mabasi