Mamlaka ya mapato Tanzania na mfumo wa internet

Mamlaka ya mapato Tanzania na mfumo wa internet

Mwenekaya Nkulu

Senior Member
Joined
Jul 16, 2014
Posts
143
Reaction score
170
Mamlaka ya mapato Tanzania yaani tra ni chombo cha serikali cha kusimamia ukusanyaji wa kodi na mapato ya serikali, ni mamlaka ambayo kwa jicho fulani hivi inayojitahidi kuhimiza watu katika kulipa kodi kwa njia na mifumo halali.
Mamlaka hii imetoa idhini kwa baadhi ya watu au taasisi binafsi kujenga mifumo ya utoaji wa risiti baada ya mauzo na huduma mbalimbali. Jambo la kushangaza na kusikitisha ni kwamba karibu kila siku au masaa kadhaa mfumo wa kutuma taarifa za risiti kwenda tra ili ziweze kutambuliwa unakua na hitilafu na wakati mwingine ni zaidi ya siku nzima au mbili na zaidi, je ni kwamba mamlaka haina wataalam wa masuala ya mitandao ya internet au kuna namna ya uzembe tu watu walio kwenye hizo nafasi wanafanya hivyo kusababisha hali hiyo? Katika ulimwengu wa sasa wa sayansi na teknolojia ni jambo la aibu kwa taasisi nyeti kama tra kuwa na uwezo wa chini kiasi hiki kushughulikia masuala kama haya. Ni mara nyingi tunasikia watu wanashindwa kufanya malipo kwa sababu mfumo upo chini na hilo limekuwa tatizo la kudumu, ina maana serikali haioni kwamba kuna uwezekano wa kuruhusu mapato kuvuja kwa watu kuamua kufanya biashara bila risiti kwa kisingizio cha mfumo upo chini? Toka tarehe 20 ya mwezi huu wa 7 kuna watu kadhaa wamefanya mauzo na kutuma taarifa zao tra lakini z report mpaka leo tarehe 22 bado ipo pending Na bado tunategemea mwisho wa mwaka tuje kujisifu kisiasa kwamba tumekusanya matrilioni kuvuka lengo wakati huu uchochoro wa makusanyo unaonekana kuwa wazi kiasi hiki? Naamini wahusika wapo humu jukwaani hebu fanyeni kazi bhana
 
Back
Top Bottom