KERO Mamlaka ya maji Mwanza (MWAUWASA) watuambie kama kuna mgao wa maji Nyakato

KERO Mamlaka ya maji Mwanza (MWAUWASA) watuambie kama kuna mgao wa maji Nyakato

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Upatikani wa maji safi katika jiji la Mwanza maeneo ya Nyakato umekua usioridhisha kwa muda wa wiki mbili sasa.

Kuna siku maji hayapatikani hata siku tatu. Kuna siku yanakuja asubui na kukatika mchana. Kipindi hiki cha sikukuu maji yamekuwa yakija na kukatika.

Tangu jana siku ya Eid maji yamekatika mpk leo jumapili hayajarudi na hakuna taarifa rasmi kutoka kwa mamlaka husika.

Nikiwa mmoja wa wateja ninaomba idara ya maji (MWAUWASA) watupe taarifa rasmi kwa nini maji hayapatikani maeneo ya Nyakato? Na kama kuna mgao basi watujulishe na watupe ratiba ya huo mgao wa maji.

Kutokuwepo kwa maji na mamlaka husika kukaa kimya ni sawa na kutudharau wateja wake hasa kipindi hiki cha sikukuu ambacho maji yanahitajika zaidi.
 
Back
Top Bottom