Mambo yamewekwa wazi

I like this Pamaoja na vitisho vyote wanavyojaribu kuvitumia kunyamazisha watu zinaelekea kushindwa umma unazidi kufahamishwa yale yote ambayo hayakuwahi kusemwa!Time will tell
 
Mohamed Said kahadithia humuhumu JF kuhusu kina Hanga na wengineo watu wakampinga sana, sasa haohao wanachukuwa hizo data na kuzipeleka bungeni.

Kwa hakika Mwenyeezi Mungu ana mipango yake. "Baniani mbaya kiatu chake dawa"
 
yaani ile Hotuba ya Tundu Lissu lime print na kuigawa kwa wanzanzibar kama 28 hivi na wameniona mimi bonge la Shujaa mpaka na mimi wananiita Mwana Uamsho, ile hotuba ilikuwa na nondo kali
mkuu tuewekee hiyo hotuba
 
Salaam kwa wote,

Tundu Lisu ameweka mambo waizi.Siri zote ziliokuwa zikisemwa semwa mitaani ameweza kuzitaja hadharani tenda ndani ya bunge la Tanzania.Huko nyumba tulikuwa tukisikia tu kutoka kwa wazee wetu kwanba kuna watu walitiwa ndani baada ya mapinduzi na hawakuonekana tena maishani kama kina Kassim Hanga na wenziwe.Haya hayajawahi kusimuliwa kwenye vyombo vya serikali kama bungeni.Nani aliyatarajia kwamba kuna siku bungeni kutatajwa mauaji yaliyofanywa na serikali? Hakuna hata mmoja wetu.Na pia kuuliwa kwa Karume kiongozi aliye unganisha nchi mbili hizi kaambiwa kuwa pia kauliwa.Hiyo hatuoni haja ya watu kuhoji sasa na kuchunguza tuhuma hizo nzito zinayoihusu Serikali? Iweje zitolewe tuhuma nzito kama hizo ndani ya bunge na serikali ikae kimya? Waandishi wa habari na wanasheria wako wapo kuhoji na kudadisi mauaji haya? au hayajawafurahisha haya? Kama wanatafuta habari za kuandika basi waanze kuhoji tuhuma hizi kwa walio husika.Na pia kesi ifunguliwe mahakamani na waliohusika wafikishwe mahakamani kama wapo waliobaki bado.Serikali lazima itoe tamko lake kama tuhuma hizo si za kweli.Venginevyo kukaa kimya ni kukubali yaliosemwa.
Nampongeza Mheshimiwa Tundu Lissu kwa kuweka mambo hadharani kwani wengi walikuwa hawafahamu nini kimetokea tangu kuundwa kwa Muungano huu ambao unalazimishwa uwepo hata kwa kutoa roho za watu..
Tumeona faida za Muungano kwamba damu zimemwagika ili kuunusuru hata kwa yule kiongozi muasisi nae pia katolewa mhanga.Haya yote ya nini? Kama watu hwataki kwanini walazimishwe? kuna ajenda gani ya siri hapa? Waandishi wako wapi wakuandika haya? Tundu Lissu kishafungua njia ya watu kuhoji kulikoni? Serikali itwanbie.Wabunge na Wawakilishi wetu kuna haja ya kufuatilia kilichosemwa bungeni na kukifanyia kazi la sivyo roho za watu zitaendelea kutoweka kwa JINAMIZI hili la Muungano.

TUNATAKA KUONA MAGAZETI YAHOJI MADAI HAYA YALIOTOLEWA NA TUNDU LISSU KTK BUNGE.

Samahani Mkuu,

Sikutazama Bunge siku hiyo. Lissu alitoa madai gani?
 
Je kwa kauli hii ya Utundu Lisu imekuongezea tsh ngapi? wote hawa wanasiasa lao moja hawana lolote whether Upinzani o C C emu
 
yaani ile Hotuba ya Tundu Lissu lime print na kuigawa kwa wanzanzibar kama 28 hivi na wameniona mimi bonge la Shujaa mpaka na mimi wananiita Mwana Uamsho, ile hotuba ilikuwa na nondo kali

wacha weeee! kumbe hata wazenji wameipenda, nadhani hiyo imekaa vizuri na ipo siku wataipata zanzibar yao na ASP yao iliyozamishwa na kifo cha tanganyika!
 
Je kwa kauli hii ya Utundu Lisu imekuongezea tsh ngapi? wote hawa wanasiasa lao moja hawana lolote whether Upinzani o C C emu

mara nyingi mgonjwa anayekaribia kufa huwa hapendi kabisa hata kutumia dawa ingawa anajua dawa ndiyo inayotibu magonjwa!
 
CCM inakufa kifo kibaya kila mahali inakabwa koo .Sasa mwisho wake ni kitu gani
 
Back
Top Bottom