Mambo ya ndoa: Yawezekana naibiwa?

CHANG'OMBE

Member
Jul 22, 2012
19
6
Habari wanajamii

Mwenzenu naleta hoja hii. Inanihusu mimi mwenyewe na simzungumzii mtu mwingine kama ilinavyofanywa na wengine.

Nina mke na watoto, kwa muda mrefu tuliishi vizuri japo mikorogano midogo midogo haikukosa. Lakini mwaka huu mwenzangu kabadilika sana na nimeingiwa na hisia kuwa huenda kuna mahali mama watoto ana-cheat.

Kwa kawaida tukishaoga usiku asubuhi yake huwa haogi mwili mzima lakini usiku wa juzi kwanza alijifanyia usafi akafyeka NYWELE ZAKE kila mahali zilipo ukiondoa za kichwani (NADHANI NAELEWEKA). Jana kaamka saa 10.00 alfajili akaenda nje kuchemsha maji ili aoge (hii siyo kawaida yake).

Mimi nilibaki ndani kwa muda lakini alipoingia ndani akakuta najiandaa kutoka nje akasema nibaki ndani kwanza yeye atakuja kunistua muda mwafaka ukifika - huenda alitaka aoge na kujufuta maji mwilini huko huko nje bila mimi kujua. Alioga hivyo hivyo na kujipuliza pafyumu nzuri nzuri, kajivika cheni za dhahabu, lipstick, nk tofauti na nilivyomzoea. Kama kawaida tuliongozana kwenda kazini japo hatufanyi kazi sehemu moja.

Jana jioni au tuseme usiku kuna shughuli nilikuwa naifanya nje, akaja kuniuliza eti nafanya nini kwa kuwa yeye alitaka kulala, hapo chakula cha usiku (dinner) hakijaliwa bado. Lakini nilipoenda dinning yeye alikuwa anahangaika na simu yake tu.

Wazoefu wa mambo haya mnijuze tafadhalini. Je kwa mazingira hayo yawezekana tayari kuna mahali amepata 3rd party?

KILA MARA MWENYEWE HUDAI KUWA YEYE NI MSAFI SANA NA KWAMBA KAMA NI KUCHEAT LABDA ITAKUWA MIMI NDIYE NAMCHEAT NA SIYO YEYE, LAKINI NYENDO ZAKE ZINATIA WALAKINI.
 
Yeye sikisha kuwambia yeye msafi sana hana mambo ya kucheat, sasa yanini unataka kumlazimisha awe cheater.

Mwanamke hachungwi baba utajiumiza tu, na mwanaume yule mwanaume haswa, mara nyingi sana huwa hana wasi wasi na mke wake.

Sasa mwanamke kujipilizia perfumes na kupaka lipstick ndo lazima awe anagawa tunda lake tu nje, kazi unayo si mchezo.
 
Mhhhhh! Yahitajika busara sana kutatua hilo jambo! Kwanza kabisa wewe usimuulize, mlie cobis tu, wala usioneshe kuwa una wasiwasi nae, ila kumuumiza roho na kumfanya roho imsute wewe mkumbushe jinsi gani unapenda sana na hutaki kumpoteza! Mweleze unavomthamini na alivo wa muhimu kwako kila mara. Ila at the same time fanya uchunguzi wa kina wa matukio yake, mpitie kazini bila taarifa mda kutoka mwambie muongozane home ( Kama ana kidate utaona atavojitahidi kukukwepa) chunguza chunguza tu taratibu kwa mda, ili upate uhakika na wkt huohuo umpe mda wa kutambua mistakes zake, huenda akajirudi. Unaweza kuta nae yamemkuta kama yangu ana crash kwa bosi wake mpya! LOL! Ila akizoea utakuta anajielewa na kurudisha heshima na upendo zaidi. Cheating inahitaji roho ya chuma! Wengi wanajaribu wanahcemsha!
 
Mkuu Changombe, una papara, hayo mambo unafatilia taratibu kama zuzu na mwisho wa siku kama anacheat utajua tu, ukishakuwa mkali ma maswali basi na yeye anakuwa makini kwa kila hatua anayopiga, hiyo simu jifanye wala hauna habari nayo na mwisho wa siku atajisahahu na kuiacha ambapo utapata muda wa kuipekua kwa siri bila yeye kujua.......................Wivu muhimu hasa kwenye chako
 
mbona sioni kigezo hapo cha kukufanya upate mawazo na labda kuhisi anakucheat jamani?? nways usiwe negative kwenye ndoa, u will always be hurted!
 
Mpe muda wa kulichunguza hili jambo, dalili zipo lakini sio strong enough to make conclusion. Mlie chabo hasa hizo simu, hasa ukipata muda muafaka jaribu kusoma txt zake au incoming and outgoing calls.

Unaweza hata ukaweka siku umfatilie nyenendo zako baada ya kazi.
 
We akili zako sometimes zinachekesha vipi ukae unamchunguza mke wako/mme wako kama humuamini unaishi naye ya nini....Pls refer Qur'an 49:12
O ye who believe! avoid suspicion as much (as possible): for suspicion in some cases is a sin: and spy not on each other nor speak ill of each other behind their backs. Would any of you like to eat the flesh of his dead brother? Nay ye would abhor it...but fear Allah: for Allah is Oft-Returning Most Merciful.
 
Jamani, sasa hivi haji hali yake tete, Je akijuwa what NEXT? Oba mungu hata kama anafanya usijue wewe timiza wajibu wako kama baba.
 
Mhhhhh! Yahitajika busara sana kutatua hilo jambo! Kwanza kabisa wewe usimuulize, mlie cobis tu, wala usioneshe kuwa una wasiwasi nae, ila kumuumiza roho na kumfanya roho imsute wewe mkumbushe jinsi gani unapenda sana na hutaki kumpoteza! Mweleze unavomthamini na alivo wa muhimu kwako kila mara. Ila at the same time fanya uchunguzi wa kina wa matukio yake, mpitie kazini bila taarifa mda kutoka mwambie muongozane home ( Kama ana kidate utaona atavojitahidi kukukwepa) chunguza chunguza tu taratibu kwa mda, ili upate uhakika na wkt huohuo umpe mda wa kutambua mistakes zake, huenda akajirudi. Unaweza kuta nae yamemkuta kama yangu ana crash kwa bosi wake mpya! LOL! Ila akizoea utakuta anajielewa na kurudisha heshima na upendo zaidi. Cheating inahitaji roho ya chuma! Wengi wanajaribu wanahcemsha!

Huu ushauri safi kabisa!
 
Wala usipate taabu badilisha ratiba ya kuwa naye kimwili, ikiwezekana dozi ya kila baada ya massa 8 kidonge
 
We akili zako sometimes zinachekesha vipi ukae unamchunguza mke wako/mme wako kama humuamini unaishi naye ya nini....Pls refer Qur'an 49:12

Kama kuna dalili zinaonyesha hivyo kwanini nisichunguze na hiyo verse imekwambia suspicion in some cases and in future stop insulting my intelligence kama haukupendezewa potezea.
 
loh yqani nyie mkishaoga usiku asubuhi mnanawa mnaenda kazini? Khaaaaaaaaaaaaaaaaa

mpe mkeo hongera kwa kujua kuwa mwanamke anapaswa awe msafi........
Mwanamke anukie......
Mwanamke asiwe na vichaka huko kunakofunikwa nguo
 
Mimi naona kapiga story na wenzake, wakamwambia mwanamke anatakiwa aoge atleast 2 times a day; na kuwa tunapaswa kujiremba muda wote ili waume zetu wasizshobokee wadada wanaokuwa nusu uchi mitaani!!

Usiwe na negative mind, utacreate negative images na mwishowe utaona negative things peke yake!
 
Mhhhhh! Yahitajika busara sana kutatua hilo jambo! Kwanza kabisa wewe usimuulize, mlie cobis tu, wala usioneshe kuwa una wasiwasi nae, ila kumuumiza roho na kumfanya roho imsute wewe mkumbushe jinsi gani unapenda sana na hutaki kumpoteza! Mweleze unavomthamini na alivo wa muhimu kwako kila mara. Ila at the same time fanya uchunguzi wa kina wa matukio yake, mpitie kazini bila taarifa mda kutoka mwambie muongozane home ( Kama ana kidate utaona atavojitahidi kukukwepa) chunguza chunguza tu taratibu kwa mda, ili upate uhakika na wkt huohuo umpe mda wa kutambua mistakes zake, huenda akajirudi. Unaweza kuta nae yamemkuta kama yangu ana crash kwa bosi wake mpya! LOL! Ila akizoea utakuta anajielewa na kurudisha heshima na upendo zaidi. Cheating inahitaji roho ya chuma! Wengi wanajaribu wanahcemsha!

Huyu kasema yote...
 
Kaka kaungane na shigongo kitabu kitauzika ila ukae chini ufanye kazi vizuri
 
usiwe na hofu na Mkeo, Labda amegundua kuoga asubuhi na kujipamba kunakuvutia wewe mumewe. So ondoa shaka na pia jitahidi kumridhisha mkeo kunako 6x6 hii itamuongezea upendo kwako na wala hatokuwa na uwezo wa kuangalia wanaume wengine.
 
Kama kuna dalili zinaonyesha hivyo kwanini nisichunguze na hiyo verse imekwambia suspicion in some cases.
Na hii thread inaongelea nini kama sio suspicion in some cases, angekuwa hamuamini mke wake yanini anaishi naye.

in future stop insulting my intelligence kama haukupendezewa potezea.
The more you act hurt, the more the insults will continue...BTW if someone insults you as being someone you're not...Yanini ukasirike :bounce:
 
Na hii thread inaongelea nini kama sio suspicion in some cases, angekuwa hamuamini mke wake yanini anaishi naye.

The more you act hurt, the more the insults will continue...BTW if someone insults you as being someone you're not...Yanini ukasirike :bounce:
fazaa naomba tu ukae mbali na post zangu, I dont see myself coming to peace with you labda ifike UN :)
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom