Mambo ya muungano na yasiyo ya muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo ya muungano na yasiyo ya muungano

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shoo Gap, Dec 22, 2011.

 1. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimesikia mara nyingi kauli hii "kuna mambo yasiyo ya Muungano na yaliyo ya Muungano",. Kwa uelewa wangu Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tz walipaswa kushughulikia yale mambo ya Muungano tu, wakati ambao Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilipaswa kushughulikia mambo ya yasiyo ya Muungano kwa upande wao tu. SWALI: Mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanganyika chombo gani kinayashughulikia?  ORODHA YA MAMBO YA MUUNGANO
  1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
  2. Mambo ya Nchi za Nje.
  3. Ulinzi na Usalama.
  4. Polisi.
  5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
  6. Uraia.
  7. Uhamiaji.
  8. Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje.
  9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
  10.Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,
  ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa
  nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
  11.Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na
  simu.
  12.Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya
  malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja
  mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;
  fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika
  na fedha za kigeni.
  13.Leseni ya viwanda na takwimu.
  14.Elimu ya juu.
  15.Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya
  motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo za
  mafuta au bidhaa, na gesi asilia.
  16.Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote
  yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
  17.Usafiri na usafirishaji wa anga.
  18.Utafiti.
  19.Utafiti wa hali ya hewa.
  20.Takwimu.
  21.Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
  22.Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengine
  yanayohusiana navyo.
  ONGEZA MENGINE KAMA YAPO
   
 2. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Aisee mengi nilikuwa siyajui....

  Nimeuchoka wimbo wa muungano ambao sioni faida yake kama Mtanzania...!
   
 3. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Ardhi sio jambo la muungano.

  elimu sio jambo la muungano.

  n.k
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  sioni uhusiano wowote na kuchoma makanisa nikisoma baadhi ya hayo mambo ya Muungano na nikilinganisha na kero za muungano.
   
 5. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Zanzibar imeshakiuka nyingi kama sio vyote kwa mtindo kujaribisha kidole kwanza
   
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  May 29, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,206
  Likes Received: 3,771
  Trophy Points: 280
  Muungano batili, na yaliyoongezwa batili!
   
 7. SONGOKA

  SONGOKA JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 1,710
  Likes Received: 877
  Trophy Points: 280
  una uhakika hayo mambo ndo nyerere na karume walikubaliana?ebu tupe hiyo hati ya muungano kama ina hiyo orodha...HAMNA MUUNGANO HAPO MKUU ni kufaamiana tu na urafiki...
   
Loading...