Mambo ya kuzingatia ukiwa unachagua vigae vya kusakafia kwa ujenzi wa jengo lako

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280

Habari za wakati mpedwa msomaji! yaweza kuwa mpaka sasa unajiuliza ni vigae gani unataka kutumia kwenye sehemu/vyumba vya jengo lako mfano sebuleni, jikoni, vyumba vya kulala, stoo, chooni, bafuni, nk. Basi majibu yake yapo hapo chini.

Aina za vigae

Kuna aina mbili za vigae
1. Kutokana na malighafi/material iliyotengeneza mfano ceramic, marble, slate, porcelain, granite,carpet , nk.

picha ya vigae vya ceramic

2. Kutokana na umbile (texture) – hapa kuna aina mbili vinavyokwaruza(grazed) na visivyokwaruza (ungrazed)

picha ya vigae vinavyokwaruza (grazed)

Mambo ya kuzingatia ukiwa unachagua vigae vya kusakafia

1. Matumizi ya eneo husika – Sehemu zenye majimaji hazihitaji vigae vinavyoteleza (ungrazed) mfano chooni, bafuni, na jikoni ukilinganisha na sehemu ambazo hakuna matumizi makubwa ya maji mfano sebuleni, sehemu ya kulia chakula na vyumba vya kulala

2. Upatikanaji – kwa kawaida inaweza kuwa aina ya kigae unachotaka ukawa uliangalia kwenye mtandao na ukakipenda lakini kumbe bado katika mazingira yako haijafika basi ni vyemba kutafuta aina nyingine iliyopo karibu na wewe au kufanya mchakato wa kuiagiza.

3. Uwezo wake na muda wa kuaribika – vigae vinatofautiana uwezo na muda wa kuaribika kutokana na malighafi/material iliyotengeneza hivyo ni vizuri kuchagua vile vinavyokaa muda mrefu ili usipate shida ya kurekebisha/maintenance mara kwa mara.

4. Gharama (mfuko wako) – ukiachana na sababu zilizoelezewa hapo juu, pia ni lazima uangalie na bei ya vigae hivyo ili uweze kufanya upembuzi yakinifu kulingana na kiwango cha fedha ulichonacho, usijiumize sana kwa sababu ya weza kuwa vipo vingine vyenye bei angalau na vinafanana na hicho unachotaka.

Zingatia: sababu hizi ni za msingi(basic) kwa yule anayehitaji vigae. kwa msaada zaidi onana na wataalamu husika kama wasanifu majengo(architect) au wakadiliaji ujenzi (quantity surveyor)

Ujenzi elekezi blog
 
KWA MARA YA KWANZA NDIO NASIKIA UWEPO WA "VIGAE KWAAJILI YA KUSAKAFIA" LABDA NI BIDHAA MPYA SOKONI ANYWAY. NINACHOJUA KAMA ULIMAANISHA "TILES" BASI KISWAHILI CHAKE CHAPASWA KUWA "MARUMARU". VIGAE NI KWAAJILI YA KUEZEKEA NYUMBA NA SI KWA AJILI YA KUSAKAFIA.
 
Marumaru ni marble mfano lile la jikoni hutumia kwa ajili ya kuwekea vitu ni marumaru na kuna sakafu za marumaru zinang'aa na vijiwe jiwe....

Vigae ni tiles...
Vigae vya sakafu
Vigae vya ukuta
Vigae vya kuezekea
Vigae vya chooni

Wasaalam wote huko mkoani...
 
Back
Top Bottom