Mambo ya kuzingatia ili kuishi muda mrefu

BenKaile

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
443
373
Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa wakazi wa maeneo mbalimbali wanaoishi maisha marefu zaidi duniani kama vile Japani, Italia na Marekani, pamoja na mambo mengine, wanajiepusha na matumizi ya vileo, tumbaku na kupunguza ulaji wa nyama nyekundu.

Nyama yenye shida kubwa ni ile yenye mafuta mengi, nyama choma iliyoungua na ile iliyosindikwa. Nyama ya namna hii huchangia kutokea kwa magonjwa ya moyo, kiharusi, kisukari na saratani ya utumbo. Hii inasababisha uzalishaji wa kemikali zinazodhuru afya.

Pia kuvuta hewa safi ya kutosha na kupata mapumziko ya kutosha baada ya kazi ngumu kila siku. mazoezi na kula chakula asilia cha mimea kama vile mbogamboga na matunda kwa wingi.
Vyakula vya asili vineelezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa matokeo ya watu kuishi miaka mingi kuliko wale ambao hawazingatii utaratibu huo.

Wataalamu wa masuala ya afya ya jamii wanaongeza kusema kuwa, uhusiano bora na mtazamo chanya katika maisha huongeza urefu wa maisha kwa miaka saba na nusu.


Hali ilivyo Afrika Mashariki
Umri wa kuishi kwa wananchi wa Tanzania hautofautiani sana na wananchi wa nchi nyingine za Afrika Mashariki. Kwa Burundi wanawake huishi hadi miaka 62 na wanaume miaka 58, huku Kenya miaka 65 kwa wanawake na wanaume (62).

Kwa upande wa Uganda, wanawake (56), wanaume (54) na Rwanda inakaribiana na Kenya ambapo wanaume huishi kwa wastani wa miaka 58 na wanawake (61).

Licha ya umri wa kuishi kati ya mwanamke na mwanaume kutotofautiana sana kwa wananchi wa Afrika Mashariki, bado kuna watu wanaishi hadi miaka 80 na wakiwa na nguvu wanafika miaka 100.

Kwa Tanzania, idadi kubwa ya wanawake wanaishi hadi miaka 63 na wanaume miaka 61, ambapo umri huo wa kuishi umeongezeka kutoka miaka 57 kwa wanawake na 54 kwa wanaume kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi, 2012. Tofauti inayojitokeza ni kuwa wanawake wanaishi muda mrefu kwa zaidi ya asilimia 2 kuliko wanaume.

Licha ya wanawake kuishi muda mrefu lakini inatajwa katika tafiti mbalimbali kuwa wanawake wa Afrika hufariki zaidi wakiwa katika umri wa miaka 15 na 34 kutokana na matatizo ya uzazi na huduma duni za afya.
 
Back
Top Bottom