Mambo ya kuyaepuka ukitembelea nchi hizi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
Utamaduni ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kuhifadhi hadhi na heshima ya mtu na kumfanya atambulike kila mahali. Mbali na hayo, lakini zipo tamaduni ambazo zinabaki kuwa za sehemu moja pekee na haziwezi kusambaa sehemu nyingine.


1: Usiache kusalimia uwapo Ufaransa
156008609f558c5ab946376b46a80c70.jpg

Kila unapotembelea nchi ya Ufaransa kumbuka kusalimia. Neno “Bonjour madame, monsieur” lazima liwe la mwanzo kutoka kinywani mwako, vinginevyo utachukuliwa kuwa unawadharau watu.


2: Usipige honi wakati unaendesha gari ukiwa Norway.
ea64521b3076806ce5ef9dad69a46112.jpg

Kama kuna jambo unalotakiwa kuwa makini uwapo Norway ni hili, kutopiga honi ukiwa unaendesha gari. Katika nchi ya Norway honi hutumika wakati wa dharura tu, hivyo kupiga kwako honi kutasababisha taharuki.


3: Usitumie mkono wa kushoto ukiwa India.
ca9ca6a94f9e33e628262c03613b15dd.jpg

Kwa mujibu wa utamaduni wa India ni kuwa mkono wa kushoto si salama. Hivyo jitahidi kila mara uwapo katika nchi hii kutumia mkono wa kulia kusalimia watu.


4: Usimalize chakula kwenye sahani ukiwa China
22b2643f296f3826fd7ff7b0cc1369e1.jpg

Nchini China, wageni waungwana hawamalizi chakula chote kwenye sahani. Kufanya hivyo hutafsiriwa mwenyeji wako hakukupa chakula cha kutosha. Sanjari na kubakisha chakula kwenye sahani, unaruhusiwa kubeua kama heshima kwa mpishi.


5: Usizungumze na mtu mikono ikiwa mfukoni uwapo Ujerumani
0676a1d86cf2329684fc17c8335b6ee6.jpg

Unapanga kutembelea Ujerumani? Jihadhari na kuzungumza na mtu wakati mikono yako ikiwa mfukoni, kitendo hicho kuchukuliwa kama jeuri. Pia ni utamaduni wa nchi hiyo kuweka mikono juu ya meza wakati wa kula.


6: Marufuku kutabasamu mbele ya mgeni ukiwa Urusi
a532bbd95c55b319858186d1272d4e1e.jpg

Upo usemi unaosema; “Tabasamu, na ulimwengu utatabasamu nawe” . Uwapo nchini Urusi usemi huu hauna maana yoyote. Warusi wanaona kutabasamu ni ishara ya karibu, ikionesha mshikamano baina yao. Kama utatabasamu mbele ya mgeni hukuchukulia kama mnafiki.


Chanzo : Nyani Ngabu
 
Back
Top Bottom