Mambo ya kukera/kutia kinyaa ambayo hufanywa na baadhi ya watu

kilambalambila

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
9,290
8,611
Wananzengo naomba tujadili mambo ambayo mimi binafsi nayachukia yanayofanywa na baadhi ya binadamu. Mambo haya naonaga kama yanatia kinyaa na yanapunnguza heshima kwa anayeyafanya hasa anapokuwa kwenye kadamnasi.

1. Kuingiza kidole puani na kukomba yale mauchafu ya kamasi kuyatoa nje. Hapo mtu atayapekecha na vidole na baadaye anayapaka kwenye kitu kilichopo karibu yake.

2. Kutoa ule uchafu wa machoni/tongotongo na vidole na kupaka sehemu.

3. Kupiga chafya bila kufunika mdomo na vi-moisture kuruka kwa wenzako.

4. Kuongea kwa jazba mpaka mate yanaruka nje ya kinywa, wengine yanajikusanya pembezoni mwa lips yanafanana na yale ambayo zamani tunayakutaga polini tunaambiwa ni mate ya nyoka.

Mambo haya na mengine ya aina yake yanakera sana na unakuta anafanya mtu mnayeheshimiana unaamua kumuacha bila kumsemesha.

Wahusika kama unasoma bandiko hili jirekebisheni tafadhali.
 
Mungu atusaidie, nimekuja kugundua kuwa "dhambi" inatia kinyaa na ni chafu kuliko chochote tunachoamini kuwa kichafu. moyo wenye dhambi ni moyo mchafu sana mbele za Mungu ndio maana ukigundua una dhambi au umeteleza ukafanya dhambi au umefanya dhambi makusudi, kimbie mbio kwa Yesu, piga magoti tubu ili akusafishe haraka kwasababu unanuka na kutia kinyaa. Mungu akusaidia, Mungu anisaidie na mimi niishi kwenye utakatifu.
 
Back
Top Bottom