Luqman mohamedy
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 899
- 1,232
Mjini bwana binadamu ni wabaya kuliko majini usipofuata principal zilizopo utaangukia pabaya. Moja kati ya mambo unayohitajika uepuke kwenye matembezi yako usiku ni:
1. Epuka kutembea kwa vikundi hasa vya watù wachache 3-5 usiku, mjini bwana mob yenu inaweza kufananishwa na kikosi kazi kilichovamia maeneo fulani alafu wote mkamiminiwa risasi au kusekwa ndani. Mwendo wa solo ni wa kioga ila unaweza kukuokoa.
2. Epuka wakati wa kuongea na simu kuweka simu sikio lililoangalia barabarani, bodaboda wataipitia ndugu yangu wavuruge matumizi ya mshahara wako ujao.
3. Epuka kupita sehemu za madada poa wanaojiuza kwani huko polisi hupita mara kwa mara kubeba watakao watuliza njaa, mitaa kama ya Sinza midnight iepuke. Pia madada poa wa kuzidiwa njaa wanakuitia mwizi wanakupiga tukio, huko nyuma watu wanakuua.
4. Epuka kukimbia kimbia bila sababu utaunganishiwa kelele za mwizi aliyejificha sehemu, wananchi mpaka wajue sio wewe utakuwa umeivaa.
5. Epuka kutembea bila kitambulisho aise, hii itakusaidia ukikamatwa na mamwera, ukipata ajali usiku au tatizo lolote ni rahisi sana kuhudumiwa na ndugu zako kupewa taarifa.
Chunga sana pindi inapofika usiku!! Usiku!
Nipe tahadhari nyingine hapa!!
===

1) Ukitembea usiku kuwa Mwenye Malengo sio kwenda kwa kuranda randa. Mara usimame ushangae ..mara urudi njia hii mara ile. Usiku sio mzuri
2) Tembea mwendo wastani. Isiwe upesi sana wala kawaida kabisa. Not to draw attention.
3) Constantly tunza Kumbukumbu ya maeneo yanayokuzunguka, nini umeona nani umemuona vyote vinavyokuijia mbele yako. Inaweza kuwa ya msaada hata ukidakwa na mamwela na ukaweza kutoa account ya matukio vyema wakaweza kupinpoint muda ulipopita ikawa alibi.
4) Epuka kuonesha vitu vyako vya thamani, Kama Simu, Tablet, Saa maana wakati mwingine unavianika ndio kuwatia watu ushawishi.
Jenga utamaduni wa kufanya mambo yako mapema na kuingia ndani kabla usiku haujawa mkubwa.