James Martin
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 1,206
- 1,509
Hivi karibuni kumekuwa na matukio mbalimbali yakikiuka au kuchochea ukiukaji wa haki za binadamu.
Mifano hai ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani kumlazimisha askari kuitikia salamu za chama chake. Halafu kumwambia mshahara wake unalipwa na serikali ya CCM. Sasa huyu kada wa CCM akitaka twende kwa kina zaidi ni kwamba serikali ya CCM imepewa dhamana tu ya hizo fedha lakini pato la serikali pia linatokana na kodi za Watanzania wote wakiwemo na wapinzani.
Halafu haikatazwi kutembelea taasisi za serikali na kufanya tathimini ya huduma zinazotolewa na kutoa maoni yake kwa kufuata ngazi za chama chake au mtu mwenye dhamana hiyo serikalini. Kuingilia moja kwa moja kwenye maamuzi na utendaji siyo sahihi. Sasa hivi inaonekana kila kada wa CCM ana uwezo wa kutembelea taasisi ya serikali na kutoa amri kitu gani kifanyike huku akipuuza watu wa ngazi za juu waliopewa dhamana ya kuongoza taasisi hizo.
Mfano mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi kushinikiza watumishi wa serikali kuchanga fedha zao binafsi kununua kifaa cha ultrasound.
Kama hiyo haitoshi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anasema watu wasiosifia mafanikio ya serikali ya awamu ya tano wachapwe viboko.
Kwa kuhitimisha natoa rai kwa wanaoguswa na upuuzi huu kusambaza hizi clips na tafsiri yake kwa Kiingereza kwa mabalozi wa nchi za nje na wadau wa haki za binadamu wa kimataifa ili wajionee wenyewe vioja vinavyoendelea.