Mambo ya hovyo yafaa kuripotiwa kwa mataifa makubwa na wadau wa haki za binadamu

James Martin

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
1,206
1,509
Hivi karibuni kumekuwa na matukio mbalimbali yakikiuka au kuchochea ukiukaji wa haki za binadamu.

Mifano hai ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani kumlazimisha askari kuitikia salamu za chama chake. Halafu kumwambia mshahara wake unalipwa na serikali ya CCM. Sasa huyu kada wa CCM akitaka twende kwa kina zaidi ni kwamba serikali ya CCM imepewa dhamana tu ya hizo fedha lakini pato la serikali pia linatokana na kodi za Watanzania wote wakiwemo na wapinzani.

Halafu haikatazwi kutembelea taasisi za serikali na kufanya tathimini ya huduma zinazotolewa na kutoa maoni yake kwa kufuata ngazi za chama chake au mtu mwenye dhamana hiyo serikalini. Kuingilia moja kwa moja kwenye maamuzi na utendaji siyo sahihi. Sasa hivi inaonekana kila kada wa CCM ana uwezo wa kutembelea taasisi ya serikali na kutoa amri kitu gani kifanyike huku akipuuza watu wa ngazi za juu waliopewa dhamana ya kuongoza taasisi hizo.

Mfano mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi kushinikiza watumishi wa serikali kuchanga fedha zao binafsi kununua kifaa cha ultrasound.

Kama hiyo haitoshi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anasema watu wasiosifia mafanikio ya serikali ya awamu ya tano wachapwe viboko.

Kwa kuhitimisha natoa rai kwa wanaoguswa na upuuzi huu kusambaza hizi clips na tafsiri yake kwa Kiingereza kwa mabalozi wa nchi za nje na wadau wa haki za binadamu wa kimataifa ili wajionee wenyewe vioja vinavyoendelea.
 
Attachments

  • VID-20190815-WA0002.mp4
    1.6 MB
  • VID-20190815-WA0001.mp4
    15.2 MB
Hawa viongozi wanahitaji semina elekezi.

Naamini ujumbe utawafikia viongozi wa Viongozi hawa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tusisahau pia kusifia na wanayofanya mazuri ili tunaowataka wasikie yanayoendelea Tanzania wafanye tathimini nzuri.

Sina maana mabaya yasisemwe au kukemewa la hasha tuyakemee ila pia tuyasifie na mazuri wayafanyao.
 
Siyo vibaya kusifia lakini tunategemea viongozi kufanya mazuri kwasababu waliapa kufanya mazuri na si mabaya.
 
Hakuna mkoa wa bariadi kuna mkoa wa simiyu alitaka wafanyakazi wachangie sio mkuu wa mkoa ni mkuu wa wilaya mtake radhi mkuu wa mkoa wangu Anthony Mtaka
 
Hivi karibuni kumekuwa na matukio mbalimbali yakikiuka au kuchochea ukiukaji wa haki za binadamu.

Mifano hai ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani kumlazimisha askari kuitikia salamu za chama chake. Halafu kumwambia mshahara wake unalipwa na serikali ya CCM. Sasa huyu kada wa CCM akitaka twende kwa kina zaidi ni kwamba serikali ya CCM imepewa dhamana tu ya hizo fedha lakini pato la serikali pia linatokana na kodi za Watanzania wote wakiwemo na wapinzani.

Halafu haikatazwi kutembelea taasisi za serikali na kufanya tathimini ya huduma zinazotolewa na kutoa maoni yake kwa kufuata ngazi za chama chake au mtu mwenye dhamana hiyo serikalini. Kuingilia moja kwa moja kwenye maamuzi na utendaji siyo sahihi. Sasa hivi inaonekana kila kada wa CCM ana uwezo wa kutembelea taasisi ya serikali na kutoa amri kitu gani kifanyike huku akipuuza watu wa ngazi za juu waliopewa dhamana ya kuongoza taasisi hizo.

Mfano mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi kushinikiza watumishi wa serikali kuchanga fedha zao binafsi kununua kifaa cha ultrasound.

Kama hiyo haitoshi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anasema watu wasiosifia mafanikio ya serikali ya awamu ya tano wachapwe viboko.

Kwa kuhitimisha nataka rai kwa wanaoguswa na upuuzi huu kusambaza hizi clips na tafsiri yake kwa Kiingereza kwa mabalozi wa nchi za nje na wadau wa haki za binadamu wa kimataifa ili wajionee wenyewe vioja vinavyoendelea.
Takataka ,mavi ya nguruwe,.badala ya kuzungumza ndani unategemea wazungu wakuamulie,kifuatacho uwape tigo kama ujira
 
Wewe ni mpumbavu kama wapumbavu wenzio sasa hao ma balozi wakusaidie nini pia hatuna mkoa unaitwa bariadi punda ww
Amesema wilaya ya Bariadi sio mkoa. Acha kukimbilia mambo usioyaelewa. Ndio tusambaze kwa mabalozi ili waione ile kauri ya muuza bar Chalamila.
 
Tusisahau pia kusifia na wanayofanya mazuri ili tunaowataka wasikie yanayoendelea Tanzania wafanye tathimini nzuri.

Sina maana mabaya yasisemwe au kukemewa la hasha tuyakemee ila pia tuyasifie na mazuri wayafanyao.
Na hili ndio tatizo la watu wengi, hayo mazuri unayoyajua wewe ni wajibu wake serikali kuyafanya maana sio hisani ni kodi zetu lakini pale serikali inapofanya mambo ya hovyo hovyo hapo tunatakiwa kukemea maana hatujawatuma kufanya maamuzi ya ajabu ajabu.
 
Wewe ni mpumbavu kama wapumbavu wenzio sasa hao ma balozi wakusaidie nini pia hatuna mkoa unaitwa bariadi punda ww
Ndugu ilikuwa inatosha tu kumsahihisha mleta uzi pale ulipoona kuna kasoro fulani, lugha staha ndiyo jambo zuri kwa muungwana yeyote kujivunia.
 
Hivi karibuni kumekuwa na matukio mbalimbali yakikiuka au kuchochea ukiukaji wa haki za binadamu.

Mifano hai ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani kumlazimisha askari kuitikia salamu za chama chake. Halafu kumwambia mshahara wake unalipwa na serikali ya CCM. Sasa huyu kada wa CCM akitaka twende kwa kina zaidi ni kwamba serikali ya CCM imepewa dhamana tu ya hizo fedha lakini pato la serikali pia linatokana na kodi za Watanzania wote wakiwemo na wapinzani.

Halafu haikatazwi kutembelea taasisi za serikali na kufanya tathimini ya huduma zinazotolewa na kutoa maoni yake kwa kufuata ngazi za chama chake au mtu mwenye dhamana hiyo serikalini. Kuingilia moja kwa moja kwenye maamuzi na utendaji siyo sahihi. Sasa hivi inaonekana kila kada wa CCM ana uwezo wa kutembelea taasisi ya serikali na kutoa amri kitu gani kifanyike huku akipuuza watu wa ngazi za juu waliopewa dhamana ya kuongoza taasisi hizo.

Mfano mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi kushinikiza watumishi wa serikali kuchanga fedha zao binafsi kununua kifaa cha ultrasound.

Kama hiyo haitoshi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anasema watu wasiosifia mafanikio ya serikali ya awamu ya tano wachapwe viboko.

Kwa kuhitimisha nataka rai kwa wanaoguswa na upuuzi huu kusambaza hizi clips na tafsiri yake kwa Kiingereza kwa mabalozi wa nchi za nje na wadau wa haki za binadamu wa kimataifa ili wajionee wenyewe vioja vinavyoendelea.
Mshamba na limbukeni huzaa ushamba na ulimbukeni kila mahali.
Tunayoyashuhudia nchini kwa sasa ni matokeo ya watu wasioandaliwa kukabidhiwa dhamana ya uongozi.
 
Na hili ndio tatizo la watu wengi, hayo mazuri unayoyajua wewe ni wajibu wake serikali kuyafanya maana sio hisani ni kodi zetu lakini pale serikali inapofanya mambo ya hovyo hovyo hapo tunatakiwa kukemea maana hatujawatuma kufanya maamuzi ya ajabu ajabu.
Unaongelea mambo ya serikali jua haumwongelei mtu mmoja.

Serikali ni umma...ni vyema tukaepuka mihemko na mawazo binafsi...busara inahitajika unapowaza kwa ajili ya wengi.

Humo kwenye wengi kuna ambao wanafikiri tofauti na ufikiriavyo wewe. Kufikiria kwao tofauti haina maana wanakosea.

Kushukuru au kusifia zuri lilofanywa haimaanishi/haijalishi ni wajibu au hisani. Huhitaji akili ya chuo kikuu hapa ni busara tu.
 
Ingekuwa miaka ya 60 au 70 wangewasikiliza lakini sio miaka ya hivii sasa, hakuna nchi yoyote itakayo jingiza kwenye maswala ya ndani kama hawaoni manufaa kwao na kwenye uchumi wao. Leo hii hakuna nchi inathubutu kuweka mguu kwenye matatizo ya Hong Kong au Ukraine kwasababu hawaoni direct impact kwenye uchumi wao. Lakini jaribu kutia mguu Saudi Arabia au Israel uone nini kitakupata, mjaribu kutafita suluhisho la humu humu ndani maana hao mnao pigia tarumbeta hawaji.
 
Hivi karibuni kumekuwa na matukio mbalimbali yakikiuka au kuchochea ukiukaji wa haki za binadamu.

Mifano hai ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani kumlazimisha askari kuitikia salamu za chama chake. Halafu kumwambia mshahara wake unalipwa na serikali ya CCM. Sasa huyu kada wa CCM akitaka twende kwa kina zaidi ni kwamba serikali ya CCM imepewa dhamana tu ya hizo fedha lakini pato la serikali pia linatokana na kodi za Watanzania wote wakiwemo na wapinzani.

Halafu haikatazwi kutembelea taasisi za serikali na kufanya tathimini ya huduma zinazotolewa na kutoa maoni yake kwa kufuata ngazi za chama chake au mtu mwenye dhamana hiyo serikalini. Kuingilia moja kwa moja kwenye maamuzi na utendaji siyo sahihi. Sasa hivi inaonekana kila kada wa CCM ana uwezo wa kutembelea taasisi ya serikali na kutoa amri kitu gani kifanyike huku akipuuza watu wa ngazi za juu waliopewa dhamana ya kuongoza taasisi hizo.

Mfano mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi kushinikiza watumishi wa serikali kuchanga fedha zao binafsi kununua kifaa cha ultrasound.

Kama hiyo haitoshi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anasema watu wasiosifia mafanikio ya serikali ya awamu ya tano wachapwe viboko.

Kwa kuhitimisha nataka rai kwa wanaoguswa na upuuzi huu kusambaza hizi clips na tafsiri yake kwa Kiingereza kwa mabalozi wa nchi za nje na wadau wa haki za binadamu wa kimataifa ili wajionee wenyewe vioja vinavyoendelea.
Alafu mnataka kupewa nchi, kwahio mtakua mnawafuata wazungu kuwasaidia kuongoza nchi?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom