Mambo ya hovyo yafaa kuripotiwa kwa mataifa makubwa na wadau wa haki za binadamu

Alafu mnataka kupewa nchi, kwahio mtakua mnawafuata wazungu kuwasaidia kuongoza nchi?

Kwanza mimi sina chama chochote. Huyu Magufuli alivyochukua nchi mimi nilikuwa mtetezi wake mkubwa lakini alivyoanza kubadilika na mimi nikabadilka.

Kuhusu kuwatafuta wazungu wa kusaidia kuongoza, hilo waulize CCM. Zaidi ya nusu karne toka tupate uhuru karibu nusu ya bajeti yetu inategemea hao wazungu.
 
Wachekesha sana wewe. Suluhisho LA ndani? na nani? Na yule yule JIWE aliyekataa hata maombi viongozi wa dini kukutana nae wakati wa UKUTA?
Ingekuwa miaka ya 60 au 70 wangewasikiliza lakini sio miaka ya hivii sasa, hakuna nchi yoyote itakayo jingiza kwenye maswala ya ndani kama hawaoni manufaa kwao na kwenye uchumi wao. Leo hii hakuna nchi inathubutu kuweka mguu kwenye matatizo ya Hong Kong au Ukraine kwasababu hawaoni direct impact kwenye uchumi wao. Lakini jaribu kutia mguu Saudi Arabia au Israel uone nini kitakupata, mjaribu kutafita suluhisho la humu humu ndani maana hao mnao pigia tarumbeta hawaji.
 
Tusisahau pia kusifia na wanayofanya mazuri ili tunaowataka wasikie yanayoendelea Tanzania wafanye tathimini nzuri.

Sina maana mabaya yasisemwe au kukemewa la hasha tuyakemee ila pia tuyasifie na mazuri wayafanyao.

Mazuri ni wajibu wa serikali, ila mabaya sio wajibu. Ukinunua chakula na kupeleka watoto wako shule hakuna ulazima wa kusifiwa popote na yoyote, lakini ukimlawiti mtoto wako mpaka mizimu ya babu zako lazima waambiwe.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK

Mimi sijaongelea kuwa wajibu au kutokuwa mkuu.

Nimeongelea mazuri yanayofanywa tuyaone pia. Wewe baba yako kama ulikuwa humshukuru na kumsifu kuwa baba bora pole/hongera ila wangu nimefanya hivyo.
 
Ni hivi kusifiwa kwa mazuri unayofanya ndani ya wajibu wako unaolipwa ni fadhila isiyodaiwa. Kama unajitolea hapo sawa.
 
Hivi karibuni kumekuwa na matukio mbalimbali yakikiuka au kuchochea ukiukaji wa haki za binadamu.

Mifano hai ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani kumlazimisha askari kuitikia salamu za chama chake. Halafu kumwambia mshahara wake unalipwa na serikali ya CCM. Sasa huyu kada wa CCM akitaka twende kwa kina zaidi ni kwamba serikali ya CCM imepewa dhamana tu ya hizo fedha lakini pato la serikali pia linatokana na kodi za Watanzania wote wakiwemo na wapinzani.

Halafu haikatazwi kutembelea taasisi za serikali na kufanya tathimini ya huduma zinazotolewa na kutoa maoni yake kwa kufuata ngazi za chama chake au mtu mwenye dhamana hiyo serikalini. Kuingilia moja kwa moja kwenye maamuzi na utendaji siyo sahihi. Sasa hivi inaonekana kila kada wa CCM ana uwezo wa kutembelea taasisi ya serikali na kutoa amri kitu gani kifanyike huku akipuuza watu wa ngazi za juu waliopewa dhamana ya kuongoza taasisi hizo.

Mfano mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi kushinikiza watumishi wa serikali kuchanga fedha zao binafsi kununua kifaa cha ultrasound.

Kama hiyo haitoshi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anasema watu wasiosifia mafanikio ya serikali ya awamu ya tano wachapwe viboko.

Kwa kuhitimisha nataka rai kwa wanaoguswa na upuuzi huu kusambaza hizi clips na tafsiri yake kwa Kiingereza kwa mabalozi wa nchi za nje na wadau wa haki za binadamu wa kimataifa ili wajionee wenyewe vioja vinavyoendelea.
Eti uwaripoti huko nje wanalialia eti unawachongea kwa mabeberu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
We nae naona ni pungu kama pungu mwenzio kasema mkoa Wa bariadi mat**ko ww
Amesema wilaya ya Bariadi sio mkoa. Acha kukimbilia mambo usioyaelewa. Ndio tusambaze kwa mabalozi ili waione ile kauri ya muuza bar Chalamila.
 
Hii awamu ya maovu na vikwazo vya kiuchumi kwa Watanzania inashangaza sana. Halafu tukisema wanalalama eti tunaichafua nchi! 😳

Hata maana halisi ya kuichafua nchi hawaijui hawa wahuni. Wao watende maovu yao siye tunaoyapinga maovu hayo tukiyaweka hadharani tunaichafua nchi! Kwa ufinyu wa akili zao maovu yao ya kubambikia kesi, kuteka, kutesa, kuua na Watanzania kupotea wanataka tuyanyamazie tu!

Hivi karibuni kumekuwa na matukio mbalimbali yakikiuka au kuchochea ukiukaji wa haki za binadamu.

Mifano hai ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani kumlazimisha askari kuitikia salamu za chama chake. Halafu kumwambia mshahara wake unalipwa na serikali ya CCM. Sasa huyu kada wa CCM akitaka twende kwa kina zaidi ni kwamba serikali ya CCM imepewa dhamana tu ya hizo fedha lakini pato la serikali pia linatokana na kodi za Watanzania wote wakiwemo na wapinzani.

Halafu haikatazwi kutembelea taasisi za serikali na kufanya tathimini ya huduma zinazotolewa na kutoa maoni yake kwa kufuata ngazi za chama chake au mtu mwenye dhamana hiyo serikalini. Kuingilia moja kwa moja kwenye maamuzi na utendaji siyo sahihi. Sasa hivi inaonekana kila kada wa CCM ana uwezo wa kutembelea taasisi ya serikali na kutoa amri kitu gani kifanyike huku akipuuza watu wa ngazi za juu waliopewa dhamana ya kuongoza taasisi hizo.

Mfano mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi kushinikiza watumishi wa serikali kuchanga fedha zao binafsi kununua kifaa cha ultrasound.

Kama hiyo haitoshi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anasema watu wasiosifia mafanikio ya serikali ya awamu ya tano wachapwe viboko.

Kwa kuhitimisha nataka rai kwa wanaoguswa na upuuzi huu kusambaza hizi clips na tafsiri yake kwa Kiingereza kwa mabalozi wa nchi za nje na wadau wa haki za binadamu wa kimataifa ili wajionee wenyewe vioja vinavyoendelea.
 
Hivi karibuni kumekuwa na matukio mbalimbali yakikiuka au kuchochea ukiukaji wa haki za binadamu.

Mifano hai ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani kumlazimisha askari kuitikia salamu za chama chake. Halafu kumwambia mshahara wake unalipwa na serikali ya CCM. Sasa huyu kada wa CCM akitaka twende kwa kina zaidi ni kwamba serikali ya CCM imepewa dhamana tu ya hizo fedha lakini pato la serikali pia linatokana na kodi za Watanzania wote wakiwemo na wapinzani.

Halafu haikatazwi kutembelea taasisi za serikali na kufanya tathimini ya huduma zinazotolewa na kutoa maoni yake kwa kufuata ngazi za chama chake au mtu mwenye dhamana hiyo serikalini. Kuingilia moja kwa moja kwenye maamuzi na utendaji siyo sahihi. Sasa hivi inaonekana kila kada wa CCM ana uwezo wa kutembelea taasisi ya serikali na kutoa amri kitu gani kifanyike huku akipuuza watu wa ngazi za juu waliopewa dhamana ya kuongoza taasisi hizo.

Mfano mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi kushinikiza watumishi wa serikali kuchanga fedha zao binafsi kununua kifaa cha ultrasound.

Kama hiyo haitoshi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anasema watu wasiosifia mafanikio ya serikali ya awamu ya tano wachapwe viboko.

Kwa kuhitimisha nataka rai kwa wanaoguswa na upuuzi huu kusambaza hizi clips na tafsiri yake kwa Kiingereza kwa mabalozi wa nchi za nje na wadau wa haki za binadamu wa kimataifa ili wajionee wenyewe vioja vinavyoendelea.
Ume bakiza kidogotu uorewe na wazungu nyambafu
 
Wachekesha sana wewe. Suluhisho LA ndani? na nani? Na yule yule JIWE aliyekataa hata maombi viongozi wa dini kukutana nae wakati wa UKUTA?
Kwani kuna kiongozi hata mmoja amejitokeza kusaini matokeo ya uchaguzi 2015 na kumtambua rasmi kama JPM ni rais aliyechaguliwa na wananchi wa Tanzania???? Mjiridhishe kwanza kabla ya kulaumu, vikwazo vingine mnajiwekea wenyewe.
 
Back
Top Bottom