Mambo ya ajabu niliyoshuhudia msibani

Wewe mleta mada ndio nakushangaa, tatizo lako umeishi kwa kukariri sasa umeona kitu tofauti unaona ni kosa, guu kwako ni ushamba, tembea maeneo tofauti uone mambo yanavyokwenda.

Suala la wahudhuriaji msibani kuwa wengi au wachache nalo kwangu halina maana, na zaidi hata hilo suala la kusema kwasababu walikuwa hawadhurii kanisani ndio maana wakakosa mchungaji sijui padre wa kuwazika nalo kwangu pia halina maana, hizo ni sheria za kanisa sio za Mungu, kama unaamini hizo sheria zina maana basi tuambie hapa Yesu alikuwa dhehebu gani?

Huyo mchungaji hawezi kumuondolea dhambi baba yake na rafikiyo hata kama akiendesha misa ya maziko, hilo walilofanya hao wachungaji sijui padre ni kuwahukumu hiyo familia ya rafiki yako wakati tumeambiwa tusihukumu tusije hukumiwa, hukumu ya haki iko mbinguni pekee.

Hao wachungaji wanajiona wako vizuri wakati nao siku ya mwisho wanaweza chomwa moto tu, kwani imeandikwa sio kila anaesema Bwana Bwana atauona ufalme wa Mungu, wachungaji/ mapadre kukataa kuzika ni siasa tu zimeingia makanisani, tumeona "wazito" wengi wanazikwa hata km walikuwa hawaendi makanisani.

Masuala ya kuzikwa na mchungaji, kuhudhuriwa mazishi yako na watu milioni mbili nk ni mbwembwe za ulimwenguni tu, haziisaidii chochote roho inayosubiri hukumu, tusidanganyike na vya ulimwengu huu.

Mwisho, huyo rafiki yako ana haki ya kumkataa huyo kaka yake kwasababu baba yake hakuwai kumwambia kama ana kaka, hilo sio kosa la binti ni kosa la mzazi baba, angempanga mapema huyo rafiki yenu hilo la kumkataa kaka yake lisingetokea.
 
Duh polen saana
 
Kuna mambo ya kijamii sio ya kujitenga kabisa,hata kwetu wako hivo ikiwa wewe unajitenga kwenye shughuli siku likikupata utaelewa
 
Kuna mambo ya kijamii sio ya kujitenga kabisa,hata kwetu wako hivo ikiwa wewe unajitenga kwenye shughuli siku likikupata utaelewa
Huu ni mtazamo hasi, huwezi kumtenga mtu hivyo ni kukosea, baya halilipwi kwa baya, baya hulipwa kwa jema ili umfundishe mkosaji aone alipokosea na ajifunze, hii sera ya jino kwa jino kufanywa na viongozi wa makanisa ni jambo la kushangaza sana.
 
Itoshe kusema tu ,hao mabinti watafunzwa na walimwengu ,hakuna MTU anayeumwa kama mzazi jamn ,ujasiri wa kufanya hayo yote unautoa wapi ? Mm nilipofiwa na wazaz wangu yaan unapata uchungu fulan machozi yanashuka yenyew tu ,una feel ile deep pain mpaka unakuta unaumia mnoooo ....lakn hawa wa kuchati na madoido mbali mbali sijui wanapata wapi huo ujasiri jaman ,kweli watu tunatofautiana

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 

vidy_tz
 
Pumba izi afu lazima utakuwa unahudhuria msosi wa foleni.
 
Kwa kweli sijasoma yote nitarudi kumalizia
 
mtoa mada ni chawa wa hao watoto wa kishua kifupi ni mtoto wa mbwa ndio mana aliweza kuvumilia izo shida zote

Sio kweli, yule ni rafiki yetu wa karibu sana ndio maana tumekua naye mwanzo mwisho, alafu hata sio wa kishua ni kawaida sana. Nimaona kwakua ishu imetokea karibia na weekend isingeathiri sana ratiba zangu za masomo.
 
Hao wameachiwa Mali/vitega uchumi kwa hiyo maisha yao hayatayumba baada ya kifo.

Moja ya sababu kwanini watu hulia sana msibani ni kufikiria uchumi baada ya kifo
 
Kwa ushuhuda wa humu kama umewalenga watu wa nyanda za juu kaskazini wasee wa kulewa Sana msibanii
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…