Duh aibu kwlkwl ,mie nilihudhuria msiba wa haya madhehebu ya kiroho baadhi ya masharti mi kutokulia unapofiwa,marehemu ameenda kupumzika halafu na wewe utake usitake utakufa tu ndio yalikuwa madai yao kwnn usilie,basi ulikuwa msiba wa wameru wakavumilia sana sana vijisheria visivyoeleweka ikiwemo kutokutamka marehemu amefariki unatakiwa useme ametwaliwa,
Mara gari wanaita punda,majina yao Mara waumini wanaitana kama kwa code unakuta MTU anaitwa Jiwe kuu,Upendo wa madhabahu Mara Adamu wa pili nk. Wameru wakatulia tuliii ikafika SAA ya mahubiri mchungaji akaiambia hadhira bila kupepesa macho hivi mnaolia mnalilia nn? Nashangaa SAA mkizini hamlii mnakuja kulia msiban' Duh Mimi binafsi nikajiuliza hivi haya ninayoyasikia kaongea kwl au?
Mara kukazuka vurugu Weee wameru walisimama ulitokea ugomvi katikati ya ibada mchungaji ma waumini wake woote wakatolewa nje wao waumini walikuwa wamevaa mavazi meupe duhhh kilichoendelea msiniulize Ila marehemu alizikwa .ni kwl mkuu mambo haya na visanga kama hivi vipo.