Mambo wafanyayo wanaume yanayokera

Mambo wafanyayo wanaume yanayokera

Nitamchukulia ana matumizi mabaya kwa hiyo nitamfundisha kubana bajeti... ila na wewe uwe unampa hela ya shoping
yani laki tano kwa mwez ni mpe na hela ya shopping tena huwezi kuwa serious miss chagga asee.....hiyo yote anafanyia nini?kwa mwezi
 
Hahaha kwani we unaonaje?

Mie sioni chochote, sikujua una unyumba....na hata hivyo majibishano yetu na wewe hayana maudhui ya "kutakana" lol, Ntuzu na wivu wake tu.
 
Last edited by a moderator:
Mie sioni chochote, sikujua una unyumba....na hata hivyo majibishano yetu na wewe hayana maudhui ya "kutakana" lol, Ntuzu na wivu wake tu.

Hahahah...hana tatizo my husband sema alikuwa anakujulisha tu kuwa mi muke ya mutu so that u dont go far teeh..!
 
Last edited by a moderator:
Habari wana JF

Katika pita pita zangu nimekutana na haya wanaume wengi wanalalamikiwa na wanawake au mabinti kuwa tabia zifuatazo zinawakera kwa kuwa nina mapenzi na rafiki zangu JF hasa MMU kama unatatizo kati ya haya baadhi nitakayotaja jirekebishe ni upendo wangu tu kwenu.


  • Kutokubali majukumu , mwanaume umeamua kuwa na mpenzi kuwa responsible na take care of your famili kama ukibahatika kupata mtoto. kwa wadada ukiona mwanaume hayupo responsible ukiwa nae jua hadi kitandani ni mvivu wa kutupa ndio wa kwanza kulalama mmh ujui kukata kiuno. Kukiss ujui akilalamika hivyo kaa kimya uone kama anaweza kazi..... utasikia wanawake wanachuna tutaachaje kuchuna wakati kutoa kwa hiyari amtaki mjifunze.

  • Kujinunisha hovyo hovyo hivi mwanaume unasusa ili iweje ... he he susa wenzio wala.
  • Kuwa mchoyo.. unakuta mwanaume ni mchoyo kiasi kwamba hata kuhudumiana ni tatizo... mwanume pesa yako vitu vyako ni tatizo sasa maana ya mimi kuwa mpenzio au mwili mmoja ni ipi kama unaniwekea demacation kwenye vitu vyako... yani hawa hadi kutoa mawazo ni kazi anaona utafaidi...
  • Mwanume mbahili yani hadi anaumwa au unaumwa kutoa hela ya kutosheleza matibabu hato ... yani sasa huyu wimbo wake wa kila siku utasikia sina hela.. hivi kutokuwa na hela ni sifa au ni uvivu basi tuone unafanya jambo la maana upuuzi mtupu
  • Mwanume kuendekeza pombe na marafiki yani unatoa kipao mbele rafiki zako kuliko mpenzio ukiona hivyo ujue huna future nzuri.... baadhi ya maandiko yanasema "ajifanyie rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe though rafiki anweza kuwa kama ndugu" tafakari.
  • Wivu uliopitiliza hapa wengi ni 25 na 30 sana hawa ndio tatizo utasikia baby tuma picha ... tuma picha unatuma bado tena tuma picha ... hivi niwaulize mnatengenezea movie hizo picha ni nini tatizo?...

muhimu: jitahidini kutafuta pesa kwa bidii na kufanya mazoezi ya viungo. siku njema rafiki


Hayo yote ulivyosema ni sawa lakini tujue kama kwa girlfriend material inawezekana lakini sio kwa wife material,,,,maana kuna baadhi ya wasichana unaDate nae Mizinga kama nuclear utadhani ndio Mke sasa yaani anakugeuza baba yake wa hiari au mlezi!!


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
sasa miss chagga ni usawa gani mnaolilia nyie ? maana majukumu yote unayoyataja ni ya baba kwa mtoto sio kwa mwanamke yaani mwanamke hata afanye kazi bado atamtegemea mwanaume ili usawa uwepo kodi ya meza igawanywe kulingana na vipato kama kuna kodi ya nyumba vivo hivyo ada na mahitaji mengine yote yanayohitaji pesa sasa mwanamke hajulikani anafanya kazi au hafanyi hela zote kwwanaume tu ? labda mfumo dume unaopingwa urudishwe

Kaka mie na m/Mke wa dizaini hiyo lazima akae nyumbani tu sasa unafanya kazi ya nini kama mshahara ni wako peke yako, utaona walivyo kosa aibu mtoto anataka hata hela ya begi la shule atakuambia mwambie baba yako!

Mie nakuambia ubaki nyumbani ulee familia!


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom