Mambo usiyoyajua kuhusu B-2 stealth bomber

Mambo usiyoyajua kuhusu B-2 stealth bomber

Ikitokea vita kati ya China na US au Russia kitu cha kwanza kuharibiwa zitakua ni hizo satellites Ili kuharibu upataji taarifa. Sasa hpo na mchezo unaponoga km Bashite Vs Gwajima.Half sasa hv tangu Vietnam war US bomber zake zinapienda kushambulia huwa zinasindikiswa na Fighters km vile F22 raptor ambazo nazo ni stealth. Half kumbuka B2 sio completely invincible kwenye advanced radar km S400 au THAAD ila inapunguza uonekani wake kwenye radar.Kama s400 inaweza kuiona B52 400km away bhas B2 inaweza sogea had mpk 50km from enemy radars na kuzishambulia.
kumbe mpo,,maana wengine wameanza kuponda wasichokijua..
 
Kati ya B2 na F 16 ipi ndege yenye teknolojia kubwa?
B2 Bomber. Half hzo mbili zote ni ndege tofauti na zipo kwa ajili ya matumiz tofaut. F16 ni multi role fighter yaaani ni maalum kwa mashambulizi ya anga(kushambulia ndege nyingine), pia kwa mashambulizi ya ardhini pia haibebi mzgo mkubwa wa silaha Huku B2 ni ndege aina ya Bomber ambayo kaz yake ni kubeba mzgo mkubwa wa silaha wakt mwingine hata kwa mashambulizi ya Nyuklia. Pia B2 imebuniwa kuwa na uwezo wa kwenda umbali mrefu mfano inaweza toka Marekani na kuja kushambulia Tanzania bila kutua popote na kurud tena Marekan.Pia B2 ni stealth wakati F16 sio stealth.
ken-judt-RoG-f-16c-cover.jpg
cbf6a83bc0f99ef4b9ef5603dd73d3bb.jpg
images.jpg
download.jpg
download+%281%29.jpg
 
1.Utengenezwaji wake ulikua ni wa Siri
Utengenezwaji wake ulikua ni wa siri sana na ni watu wachache sana ndani ya serikali walijua uwepo wa mpango wa uundwaji wake.Mradi wa utengenezwaji wake ulipewa jina la Gray project na wote waliohusika katika project hiyo ilibidi kuchunguzwa sana na serikali mpaka historia zao na mahali walipotoka ili kulinda kuvuja siri ya projekti hiyo.
2.Ni ndege ya gharama sana ndani ya jeshi la Marekani na Duniani kwa ujumla
B2 stealth bomber ni ndege ya gharama sana kuwahi kutengenezwa katika historia ya jeshi la Marekani na Duniani kiujumla.Hii ni kutokana na teknolojia iliyotumika pamoja na malighafi sake kua za gharama kubwa sana.Kila ndege moja iligharimu zaidi ya dola milioni 737(In 1997 dollars) ambao ununuzi wake ulifikia hadi dola milioni 929 hii ni ukijuisha na spare parts, software support pamoja na vifaa vingine.Mradi mzima uligharimu zaidi ya dola bilioni 2.1(in 1997 dollars) za kimarekani kwa ndege moja hii ikijumuisha uundwaji, utafiti pamoja na majaribio yake.Kutokana na gharama zake kuwa kubwa na kuvunjika kwa Umoja wa kisovieti hii ilifanya jeshi la Marekani kupunguza idadi ya utengezaji wake kutoka ndege 132 mpaka 21 tu.
3.Inagharimu dola 135,000 kuindesha kwa lisaa limoja
B2 bomber inagharimu zaidi ya dola 135,000 kuindesha kwa lisaa moja tu hii inafanya kuwa na gharama Mara mbili kuiendesha ukilinganisha na B1 na B52 bomber.
4.Ina uwezo wa kuruka zaidi ya kilometa 11,000 bila kutua popote
B2 bomber ina uwezo wa kuruka kwa zaidi ya kilometa 11,000 bila kupumzika na zaidi ya kilometa 19,000 pale inapoongezwa mafuta.
5.Kwa Mara ya kwanza ilitumika kwenye vita ya Kosovo mwaka 1999.
Baada kuanza kazi kwenye jeshi la Marekani B2 ilifanya mashambulizi yake ya kwanza dhidi ya adui mwaka 1999 kwenye vita ya Kosovo.Inaarifiwa kwamba ingawa B2 bomber iliruka Mara 50 kufanya mashambilizi lakini ilifanya mashumbulizi ya asilimia 11(11%) ya mabomu yote yaliyotumika kwenye vita hivyo.Pia imefanya mashambulizi nchini Iraq,Afghanistan na Libya kwenye operasheni ya kumuondoa kiongozi wa Libya Muamar Gaddafi.
6.Ina uwezo wa kubeba mzigo wa mabomu wa zaidi ya kilogramu 18000
B2 ina uwezo wa kubeba mzigo wa mabomu wa zaidi ya kilogramu 18000 hii ikijumuisha yale ya nyuklia kama vile B83,B61.Pia ina uwezo wa kubeba makombora mbali mbali kama vile AGM-129 ACM na hata yale nyuklia.Mwaka 2009 iliongezewa uwezo mwingine wa kubeba mabomu makubwa ya kuharibu mahandaki au ngome za kijeshi zilizo chini ya ardhi maarufu kama Massive Ordinance Penetrator(MOP) yenye uzito wa 14000kg.
7.Ina Radar Cross Section yenye ukubwa wa 0.0001m^2
Inaarifiwa kwamba B2 ina Radar Cross Section yenye ukubwa wa 0.0001m^2,hii ina maanisha kwamba B2 ni ngumu kuonekana kwenye rada ya adui.Japokua kuna taarifa nyingine zinasema kwamba B2 ina Radar Cross section ya 0.1m^2 ambayo ni sawa na ukubwa wa mbegu ya mbaazi.
8.Ni vigumu kuonekana kwenye Rada ya adui
Moja ya vitu vinavyofanya B2 kufikia lengo hili ni pamoja na umbile lake ambalo haliakisi mawimbi ya rada na kurudi kwenye rada.Pia uwepo wa Radar Absorbing Materials(RAM) ambazo husaidia kufyonza mawimbi ya rada, hii inazuia kutorudi kwa mawimbi hayo kutoa taarifa ya uwepo wake. Pia injini zake zimefunikwa ndani kwa ndani kuzuia uwezekano wa kuonekana kwenye rada.
9.Ina mahitaji yote kwa ajili ya marubani kuanzia malazi,sehemu ya kuandaa chakula na choo
Kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutembea umbali mrefu ikiwemo kutoka bara moja hadi jingine Ndege hii iliwekwa mahitaji yote muhimu kwa ajili ya marubani ikiwemo vitanda vya kupumzika, sehemu ya kuandaa chakula pamoja na choo.Rubani mmoja anaweza kupumzika wakati mwingine akiendelea kuongoza ndege,hii ni ili kusaidia kupunhuza uchovu.
10.Ndio ndege ya pekee aina ya Bomber ambayo ni Stealth
B2 stealth ndio pekee aina ya Bomber ambayo ina teknolojia ya stealth yenye uwezo wa mashambulizi ya nyuklia.
Oooshh!! du aisee!!! niivyoiona huu uzi niijua taya Bashite imeshatishwa kuhusu vyeti vyake!!!

Nlikua nshatoa oda ya jogooo kwa ajili ya mchele bete kesho mchana tusheherekee na masela wangu mitaa ya uswahilini kwetu ....... any way kitawaka tu anytime
 
Satellite navigation technology ni technologia ya mwaka 1970 technologia hii baadhi ya nchi tayali wameshakuwa na uwezo wa kubypass technologia hii mfano nchi ya Pakistan katika project yao ijulikanayo kama PROJECT 706[1974-1983] waliweza kubypass SNT za US,UK na Israel na kufanikiwa kutengeneza bomu la nuclear bila ya dunia kujua kilichokuwa kinafanyika ndani ya jiji la islamabad kuanzia mwaka 1974-1983

Jeshi kuna aina tatu za ndege ambazo zinaingia ndani ya uwanja wa mapambano front line
1 Ndege za mizigo{cargo}
2 Fighter jet
ndege hizi mara nying zinakuwa na vitu viwil moja supersonic speed na kuwa na uwezo wa kubeba smart bombs ambazo lazima zinakuwa na mfumo wa Precision Guided munition [PGM]
3 Ni ndege zijulikanazo kama Bomber
Bomber ni ndege zenye kuweza kubeba mzingo mkubwa [payload] wa vilipuzi mabomu lakini mabomu hayo yanakuwa hayana mfumo wa PGM

Ndege ambayo mkuu ze kokuyo anaizungumzia ni ndege aina ya Bomber lakini ndege za bomber zipo nying tu mfano B52 lakini kinachoifanya B2 spirit ambayo imetengezezwa na kampuni ya Northrop Grumman kuwa tofauti na zingine ni technologia yake ya[ STEALTH]

STEALTH si ndege kama watu wanavyojua stealth ni technologia ambayo inawekwa kwenye ndege ambapo huwezesha ndege kutoonekana kwenye rada

kumbuka Technology ya rada imegunduliwa kwenye miaka 1930 so kumekuwa na mabadiliko ya technologia hii miaka na miaka
hili rada iweze kuona ndege huwa inascan anga na kurudisha kitu kinachoitwa Electromagnetic pulse [EMP] ambazo zinakuwa translated kwenye radio waves kupitia hizo radio waves inaweza kugundua umbali ,sehemu na ukubwa wa kitu kama ndege ,meli na mabomu au makombora yanaweza kuwa detect na rada sasa technologia hii ya Stealth ndio inaweza kuidanganya rada au kuzuia hizo electromagnetic pulse ambazo zinatumwa kwenye rada station

Zipo aina mbili za stealth technology

1 Ni aina ya mikunjo au mikato ya ndege {Cutting Edge]
hii technology cutting Edge ndio inatumika sana kwenye ndege za fighter kama F-35 LIGHTING II yani kifupi zile ndege au jets wanazosema hazionekani kwenye rada hii cutting Edge inadanganya rada vitu viwili

[A) Rada haiwezi kujua ni kitu gani kinakuja {kumbuka kwenye rada ni vitu vyote vilivyo angani vinaonekana so watashindwa kujua aidha ni ndege ya raia ,jeshi au drone so inawachanganya wakuwa hawawezi kushambulia kitu wasichokuwa na 100% sure ni kitu gani

[B) Rada haiwezi kujua umbali halisi wa hicho wanachokiona {kumbuka rada inatoa umbali,sehemu kilipo na ukubwa wa kitu]


2 Ni mchanganyiko wa rangi na material mbalimbali {ambayo mpaka sasa ni top secret na mwenye technologia hii ni kampuni ya Northrop Grumman ambayo ndio watengenezaji wa hii B-2 Spirit na technology hii ya kuchanganya rangi na material ni tofauti na technology ya Cutting Edge ambayo inafanya vitu nilivyovitaja hapo juu hii ni NOTHING TO DISPLAY kwenye rada yani kifupi uwezi kuona kitu kwenye rada



Tuje kwenye B-2 Spirit ndege hii inazo technologia zote mbili za stealth ikiwamo technologia ya Cutting Edge na hii ya kuchanganya rangi na material mbalimbali ambayo ndio inaifanya dege hili kutokuonekana kwenye rada na limeshakwenda sehemu mbalimbali duniani kufanya mission ikiwamo Russia bila ya kuonekana na kurudi salama US

MALCOM LUMUMBA

Mkuu watu wengi wanabisha kiushabiki na sio kitaalamu, siku zote ukiwa unajua mambo ni rahis kupanga hoja na sio kubase kwenye ushabiki tuuu
Maana mchango watu umetoa elimu kubwa na base ya wengine kufatilia na kusoma zaid tujue technology inavyo kuwa
Asante sana mkuuu
 
Oooshh!! du aisee!!! niivyoiona huu uzi niijua taya Bashite imeshatishwa kuhusu vyeti vyake!!!

Nlikua nshatoa oda ya jogooo kwa ajili ya mchele bete kesho mchana tusheherekee na masela wangu mitaa ya uswahilini kwetu ....... any way kitawaka tu anytime
Bashite yupo bondeni anakula bata anatuchora tu. Hio oda ya jogoo kaifute tu Mkuu.
 
Hiyo b2 itafanya mashambulizi kwa nchi kama pakistan;Syria na nyingine lakini kwa nchi kama urusi sizani kama zitafua dafu maana mrusi ana kila teknolojia ambayo marekani anaifanya
 
Half ingekua kweli Marekani wameogopa au hyo meli ilikua imezimwa kamwe isingerudi tena eneo hill lkn 2yrs later ilirud tena kupatrol km kawaida.Na mpk Leo Marekan anapeleka Aegis destroyer Black Sea na Russia anachokifanya ni kurusha tu ndege vita zake kuzimonitor tu zisivuke International waters.Hyo ilikua 2016 ikarud tena tena Su-24 zikarushwa na US Navy wakatoa tena hadi video kukata mziz wa fitina. View attachment 479006View attachment 479007
 
Hiyo b2 itafanya mashambulizi kwa nchi kama pakistan;Syria na nyingine lakini kwa nchi kama urusi sizani kama zitafua dafu maana mrusi ana kila teknolojia ambayo marekani anaifanya
Sasa hv wana kitu kipya kinatarajiwa kuanza kaz 2020.Kinaitwa B-21 Raider.
images.jpg
 
Back
Top Bottom