ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,417
- 9,603
1.Utengenezwaji wake ulikua ni wa Siri
Utengenezwaji wake ulikua ni wa siri sana na ni watu wachache sana ndani ya serikali walijua uwepo wa mpango wa uundwaji wake.Mradi wa utengenezwaji wake ulipewa jina la Gray project na wote waliohusika katika project hiyo ilibidi kuchunguzwa sana na serikali mpaka historia zao na mahali walipotoka ili kulinda kuvuja siri ya projekti hiyo.
2.Ni ndege ya gharama sana ndani ya jeshi la Marekani na Duniani kwa ujumla
B2 stealth bomber ni ndege ya gharama sana kuwahi kutengenezwa katika historia ya jeshi la Marekani na Duniani kiujumla.Hii ni kutokana na teknolojia iliyotumika pamoja na malighafi sake kua za gharama kubwa sana.Kila ndege moja iligharimu zaidi ya dola milioni 737(In 1997 dollars) ambao ununuzi wake ulifikia hadi dola milioni 929 hii ni ukijuisha na spare parts, software support pamoja na vifaa vingine.Mradi mzima uligharimu zaidi ya dola bilioni 2.1(in 1997 dollars) za kimarekani kwa ndege moja hii ikijumuisha uundwaji, utafiti pamoja na majaribio yake.Kutokana na gharama zake kuwa kubwa na kuvunjika kwa Umoja wa kisovieti hii ilifanya jeshi la Marekani kupunguza idadi ya utengezaji wake kutoka ndege 132 mpaka 21 tu.
3.Inagharimu dola 135,000 kuindesha kwa lisaa limoja
B2 bomber inagharimu zaidi ya dola 135,000 kuindesha kwa lisaa moja tu hii inafanya kuwa na gharama Mara mbili kuiendesha ukilinganisha na B1 na B52 bomber.
4.Ina uwezo wa kuruka zaidi ya kilometa 11,000 bila kutua popote
B2 bomber ina uwezo wa kuruka kwa zaidi ya kilometa 11,000 bila kupumzika na zaidi ya kilometa 19,000 pale inapoongezwa mafuta.
5.Kwa Mara ya kwanza ilitumika kwenye vita ya Kosovo mwaka 1999.
Baada kuanza kazi kwenye jeshi la Marekani B2 ilifanya mashambulizi yake ya kwanza dhidi ya adui mwaka 1999 kwenye vita ya Kosovo.Inaarifiwa kwamba ingawa B2 bomber iliruka Mara 50 kufanya mashambilizi lakini ilifanya mashumbulizi ya asilimia 11(11%) ya mabomu yote yaliyotumika kwenye vita hivyo.Pia imefanya mashambulizi nchini Iraq,Afghanistan na Libya kwenye operasheni ya kumuondoa kiongozi wa Libya Muamar Gaddafi.
6.Ina uwezo wa kubeba mzigo wa mabomu wa zaidi ya kilogramu 18000
B2 ina uwezo wa kubeba mzigo wa mabomu wa zaidi ya kilogramu 18000 hii ikijumuisha yale ya nyuklia kama vile B83,B61.Pia ina uwezo wa kubeba makombora mbali mbali kama vile AGM-129 ACM na hata yale nyuklia.Mwaka 2009 iliongezewa uwezo mwingine wa kubeba mabomu makubwa ya kuharibu mahandaki au ngome za kijeshi zilizo chini ya ardhi maarufu kama Massive Ordinance Penetrator(MOP) yenye uzito wa 14000kg.
7.Ina Radar Cross Section yenye ukubwa wa 0.0001m^2
Inaarifiwa kwamba B2 ina Radar Cross Section yenye ukubwa wa 0.0001m^2,hii ina maanisha kwamba B2 ni ngumu kuonekana kwenye rada ya adui.Japokua kuna taarifa nyingine zinasema kwamba B2 ina Radar Cross section ya 0.1m^2 ambayo ni sawa na ukubwa wa njiwa mdogo.
8.Ni vigumu kuonekana kwenye Rada ya adui
Moja ya vitu vinavyofanya B2 kufikia lengo hili ni pamoja na umbile lake ambalo haliakisi mawimbi ya rada na kurudi kwenye rada.Pia uwepo wa Radar Absorbing Materials(RAM) ambazo husaidia kufyonza mawimbi ya rada, hii inazuia kutorudi kwa mawimbi hayo kutoa taarifa ya uwepo wake. Pia injini zake zimefunikwa ndani kwa ndani kuzuia uwezekano wa kuonekana kwenye rada.
9.Ina mahitaji yote kwa ajili ya marubani kuanzia malazi,sehemu ya kuandaa chakula na choo
Kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutembea umbali mrefu ikiwemo kutoka bara moja hadi jingine Ndege hii iliwekwa mahitaji yote muhimu kwa ajili ya marubani ikiwemo vitanda vya kupumzika, sehemu ya kuandaa chakula pamoja na choo.Rubani mmoja anaweza kupumzika wakati mwingine akiendelea kuongoza ndege,hii ni ili kusaidia kupunhuza uchovu.
10.Ndio ndege ya pekee aina ya Bomber ambayo ni Stealth
B2 stealth ndio pekee aina ya Bomber ambayo ina teknolojia ya stealth yenye uwezo wa mashambulizi ya nyuklia.