ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,087
- 61,456
Mimi ni mkristo wa dhehebu la Lutheran Church na nimekuwa nikipenda Sana kujifunza habari za Mambo ya Mungu na niliamua kuanza kusoma vitabu vyote kuanzia vitabu vya wayahudi biblia yao ya tanakh,kisha nikasoma Cha wahindi Cha bhaghavad Gita Kisha nikamalizia na Quran.katika usomaji wangu nikagundua vitabu vyote vina mapungufu fulani fulani lakini biblia ya kikristu ndiye nikagundua Ina makosa mengi Kuliko vitabu vyingine.hitimisho nikaona kabisa Quran ndio dini ya kisasa yenye miongozo yake na SHERIA nzuri kabisa na pia UISLAM umekuja baada ya ukristo ili kuboresha ukristo..zote Ni dini zinazo mcha mwenyeziMungu tumekubali lakini ukitaka utambuzi wa Hali ya juu Ni lazima utoke kwenye ukristo Kisha uende kwenye UISLAM Kisha umalizie kwenye science..yaani zote hizo tunaziita Ni partial Truth dini zote Ni partial Truth kiukweli watu wa zamani walijitahidi Sana hatuwezi kubeza waliyofanya sisi tunapaswa tuboreshe Zaid walipoishia.ndo maana tunasema Islam Ni dini ya kisasa Zaid kwanza sala zake kipindi unafanya tahajudi unaufanya mwili ukae vizuri zile stretches na pose mbali mbali unapopiga rakat zako Ni mazoezi tosha, kuchukuliwa udhu inakufanya unisikie refreshments kidogo kifupi Ni dini nzuri tofauti kabisa na ukristo ambao unaenda kanisani mchungaji anasema toka mapepo toka kwa jina la yesu toka mapepo toka toka...halafu Akimaliza kusema mnatoa mchango kisa mnarudi nyumbani