Kuna Mambo manne muhimu kwa miezi ya karibuni ambayo yataleta mwelekeo wa taifa letu kisiasa katika mambo haya manne matatu ni ya Chadema na mmoja ni la CCM.
Chedema inatakiwa kufanya maamuzi magumu kwenye haya mambo matatu
1. Bila katiba na tume huru ya uchaguzi wajitoe kabisa kwenye chaguzi lakini wasifanye kampeni za mgomo nchi nzima
2. Bila katiba mpya na tume huru washiriki chaguzi na kuombee walau chaguzi ziwe bora kuliko 2020
3. Bila katiba mpya na tume huru wagomee chaguzi ikiwa ni pamoja na kupiga kampeni za watu kutokushiriki chaguzi nchi nzima. Hii ni mgomo
4. Raisi samia je anataka kushinda kinyemela kwa 80% au kihalali kwa 51%-55%. Lanini hii 51%-55% inakuja na historia nzuri ya katiba mpya ambayo ni msingi mkubwa sana kwa maendeleo.
Kwa CCM na Raisi Samia anatakiwa kuelewa kutokuwa na tume huru na katiba mpya maana yake ni kuimarisha ngome ya Tindu Lissu na Lema ambayo haiamini hata kidogo serikali. Sababu ni kwamba Raisi Samia ndani ya Chadema ataonekana alikuwa anamtapeli Mbowe na kupunguza nguvu zake na ushawishi kwamba maridhiano yalikuwa na tija. Viongozi wenye msimamo mkali ndali ya Chadema wakiongozwa na Lissu sio kitu cha kupuuzwa kwa nchi. Hiki kikundi kina kipaji kuliko wanasiasa wowote Tanzania kwenye uchambuaji wa ajenda. Kikundi hiki kinajua kujenga hoja kuliko wengine wote mfano DP World tumeona. Lakini kikundi hiki kimataifa kinajulikana na wanajua siasa za kimataifa hasa ukizingatia Lissu na Lema wote wamekaa nje. Hii itadumisha sana upande ambao unampenda Samia wa Mboe, Sugu na Msigwa na kupaisha wanasiasa machachari ambao ni Lissu, Lema na Heche.
Geti la mbwa wakati Chadema kwasasa mwenye funguo ni Mbowe lakini kwa sasa kapoteza funguo na kama Raisi Samia asipojirudi na kuweka vizuri swala la tume na katiba mpya kudi la siasa kali ndani ya Chadema litachukuwa funguo na nchi hii haitakalika. Kwasasa wanaonyesha siasa za kipole kwasababu wanaendelea kwenda vijijini na kuandikisha watu hadi vijijini na zoezi la ziara likiisha tayari kundi hili litakuwa linajua watu wao ni wangapi, wako wapi na watakuwa na hadi simu za wafuasi wote!. Lakini Lissu ameshakutana na viongozi wote wa kimataifa wanao ongoza mashirika ya kimataifa ya demokrasia na wale wanaotupa pesa hasa nchi za magharibi. Raisi Samia asipo mpa Mbowe nguvu kwa kuweka Maridhiano na kuwasikiliza wakina Kinana ambao niwafanyabiashara na wanao angalia maslahi yao nchi hii itaingia kwenye wakati mgumu sana.
Tatizo kubwa litakuwa Raisi ataanza kuongozwa na wanasiasa wenye siasa kali ndani ya CCM wasiotaka mabadiliko na Chadema itaongozwa na wanasiasa wenye siasa kali ambao wanataka mabadiliko kwa njia yeyote ile! hii italeta mtafaruku mkubwa.
Hivyo maamuzi ya Raisi Samia kwenye maridhiano ya Chadema bila kujua yanaweza kuleta mapinduzi kwenye nchi hii.