Mambo kumi niliyoyaona mechi ya leo Simba na Yanga

venance7

Senior Member
Joined
May 15, 2019
Messages
182
Points
1,000

venance7

Senior Member
Joined May 15, 2019
182 1,000
1. Goli la penati halikuwa sahihi Meddie Kagere alivutwa nje boksi akadondokea ndani ya boksi,hapa refa aliyumba.

2. Yondani alistahili kadi nyekundu kwa kosa la kumvuta Meddie Kagere nje ya boksi,kadi nyekundu kwasababu Yondani ndiye aliyekuwa mtu wa mwisho.

3. Goli la Mapinduzi Balama ni moja kati ya magoli bora hadi sasa,kama kuna tuzo ya goli la mwezi basi hili linastahili kushinda.

4. Refa alizidiwa na presha ya mechi,alijaribu kubalance ili aonekane hapendelei upande mmoja.

5. Wachambuzi wa Azam wapunguze ushabiki sawa haikuwa penati lakini walionekana wote wapo upande wa kumlaumu refa na sio kutoa uchambuzi yakinifu wote walikuwa na jazba.

6. Simba walitawala mchezo kipindi cha kwanza na Yanga walibadilika kipindi cha pili. Pongezi kwao maana ni ngumu kufungwa bao mbili na kurudi kwa kasi ile.

7. Aishi Manula ajitathmini aina ya magoli anayofungwa ni yaleyale siku zote.

8. Kutoka kwa Deo Kanda na Meddie Kagere kumeigharimu Simba.

9. Faruk Shikalo anastahili kuwa man of the match aliokoa saves nyingi sana kwa game ya presha namna ile pongezi kwake.

10. Uchawi upo katika hizi derby,mashabiki tuache kuingia na matokeo mfukoni.

Nb: Haya ni maoni yangu yanastahili kupingwa kwa hoja.
 

Zesh

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2017
Messages
14,206
Points
2,000

Zesh

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2017
14,206 2,000

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Messages
17,983
Points
2,000

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2016
17,983 2,000

Forum statistics

Threads 1,392,180
Members 528,565
Posts 34,100,840
Top