Mfanano wa magoli mechi ya Simba vs ASEC na ya leo ya Tanzania vs Togo

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,136
7,903
Wiki chache zilizopita nilileta uzi mmoja nikihoji kwa nini matukio katika mechi za Simba msimu iliyopita na msimu huu yamekuwa yanafanana sana na yale ya Yanga pale timu hizo zinapocheza siku moja au siku mbili zinazofuatana.

Leo tena katika mechi ya Tanzania vs Togo nimeshuhudia magoli mawili kati ya matatu yaliyofungwa katika mazingira yanayofanana na magoli mawili yaliyofungwa katika mechi ya Simba vs ASEC Mimosas.

Leo Tanzania walipata penati ya goli la kwanza iliyopatikana katika mazingira yanayofanana sana kama ile penati iliyopata Simba na goli kufungwa na Saidoo. Penati zote mbili zilifungwa ndani ya tofauti ya dakika 4.

Pia goli la tatu la Tanzania linafanana na goli la kusawazisha la ASEC. Katika goli hilo, Opah alipata mpira katikati ya uwanja akautuliza vizuri akapiga chenga moja, akampasia winga, winga akasogea kidogo akamrudishia Opah aliyekuwa amefika ndani ya box akamalizia kwa goli zuri. Goli la kusawazisha la ASEC nalo lilikuwa hivyo hivyo. Magoli yote mawili nayo yalifungwa ndani ya tofauti ya dakika 4.

Mechi za Jumamosi zitahitimisha uchunguzi wangu ili niwe mwekezaji rasmi kwenye sekta ya kubeti.
 
View: https://www.youtube.com/watch?v=-Ovbg1wnxSU

View: https://www.youtube.com/watch?v=6UUUT0Wglrg

Mechi za Jumamosi zitahitimisha uchunguzi wangu ili niwe mwekezaji rasmi kwenye kubeti.

Aahaahaa

Poa mkuu
 
Babu huwa unapiga cha Arusha au cha Malawi?
 
Kama nilivyoahidi, jana niliendelea na uchunguzi wangu na kusema kweli unaendelea kunishangaza.

Katika mechi ya Gwaneng Galaxy vs Simba ilipofika dakika ya 90, Chama alipata nafasi ya wazi akapiga shuti na mpira ukagonga mwamba. Katika mechi ya Yanga vs Al Ahly, Yanga walipata goli lao pekee na la kusawazisha dakika ya 90.

Hii inaweza isifanane sana na matukio mengine niliyoorodhesha huko nyuma ila unaona ukaribu wa matukio kwa kiasi fulani.

Nimeamua kuendelea zaidi na uchunguzi wangu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom