Naona hili kama limefumbiwa macho vile.Kuna mtu ana picha yoyote ya ile Hirizi aliyokutwa nayo Kagere?
HahahahahahahBabe haya yashapita sasa. Najua nitakufungia wapi tena.
Namba5 wewe ndio umeleta mahaba, refa alikuwa na presha ya mechi na kuleta maamuzi ya hovyo yanga wanashambulia kagere anakaa chini refa anasimamisha mpira huu si uzwazwa1. Goli la penati halikuwa sahihi Meddie Kagere alivutwa nje boksi akadondokea ndani ya boksi,hapa refa aliyumba.
2. Yondani alistahili kadi nyekundu kwa kosa la kumvuta Meddie Kagere nje ya boksi,kadi nyekundu kwasababu Yondani ndiye aliyekuwa mtu wa mwisho.
3. Goli la Mapinduzi Balama ni moja kati ya magoli bora hadi sasa,kama kuna tuzo ya goli la mwezi basi hili linastahili kushinda.
4. Refa alizidiwa na presha ya mechi,alijaribu kubalance ili aonekane hapendelei upande mmoja.
5. Wachambuzi wa Azam wapunguze ushabiki sawa haikuwa penati lakini walionekana wote wapo upande wa kumlaumu refa na sio kutoa uchambuzi yakinifu wote walikuwa na jazba.
6. Simba walitawala mchezo kipindi cha kwanza na Yanga walibadilika kipindi cha pili. Pongezi kwao maana ni ngumu kufungwa bao mbili na kurudi kwa kasi ile.
7. Aishi Manula ajitathmini aina ya magoli anayofungwa ni yaleyale siku zote.
8. Kutoka kwa Deo Kanda na Meddie Kagere kumeigharimu Simba.
9. Faruk Shikalo anastahili kuwa man of the match aliokoa saves nyingi sana kwa game ya presha namna ile pongezi kwake.
10. Uchawi upo katika hizi derby,mashabiki tuache kuingia na matokeo mfukoni.
Nb: Haya ni maoni yangu yanastahili kupingwa kwa hoja.
Hirizi ya Kagere hukuiona?
Kwa mtazamo wangu mashabiki wa Simba huwa hawaangalii mapungufu ya timu yao hata pale inaposhinda goli 4-0. Wao wanashangilia tu.Hirizi ya Kagere hukuiona?
Ile niliyokushtukia kuwa ni mwanamke wangu, Kama vp fungua pm yko nikutumie ushahid, au niupandishe hapa hapa jukwaan
Wewe mimi sio mwanamke wako bwana na sina mtoto khaaaaIle niliyokushtukia kuwa ni mwanamke wangu, Kama vp fungua pm yko nikutumie ushahid, au niupandishe hapa hapa jukwaan
Goite
Ww ndiye
Kwako mwalimu kashashaNilichoona leo ni kwamba sisi wanaume tunatakiwa kuhakikisha mwanamke anafika kwanza kileleni then sisi ndio tunafuata yan tunakua wote tumefika.
Ndio uanaume. Ahsante Yanga kwa fundisho hili.
Sent using Jamii Forums mobile app
In kambalage voiceKwa mtazamo wangu mashabiki wa Simba huwa hawaangalii mapungufu ya timu yao hata pale inaposhinda goli 4-0. Wao wanashangilia tu.
Kama wangekuwa wanaifuatilia mapungufu yake wasingeingia na matokeo.
Wachezaji wanaocheza kwa jihadi na nguvu Simba ni wachache sana, wanapokutana na timu inayotumia nguvu na mbio wanapata taabu sana, mathalan Mkude sio mchezaji wa mpira wa kasi na nguvu, hivyo nyuma yake alitakiwa awepo Fraga, lakini kwa mshangao hata sub hakuwekwa. Kwa hili namlaumu sana Matola kwa sababu anawajua wachezaji kuliko Sven.
Namlaumu tena Matola kwa kumpanga Manula, hivi anafikiri Nderagije ni mjinga alipomuacha taifa! Kipa anayefungwa magoli ya kawaida sana hapaswi kupangwa kwenye Derby.
La mwisho, Simba watambue kuwa Yanga inayocheza na Biashara United sio itakayocheza na Simba, lazima watapandisha kiwango cha uchezaji, hasa wachezaji kibinafsi, kwa sababu na wao pia wangependa wasajiliwe na Simba.
Hakuna mchezaji bongo ambaye hataki kucheza Simba, kwa hiyo pale wanakuwa sokoni kama walivyofanya akina Beno, ndio maana mashabiki wa Simba wanatakiwa wajifunze kuwa Sportsmen na waache unazi kama wa Manara.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mtu ana picha yoyote ya ile Hirizi aliyokutwa nayo Kagere?