Mambo gani yanaweza kubatilisha WOSIA?

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,595
Endapo nitaandika wosia kuhusu jinsi gani Mali zangu zigawanywe kwa wategemezi wangu kama mke watoto na ndugu!

Mfano:
Nina watoto wanne kwa mke mmoja na katika wosia wangu nikaeleza kuwa Mali zangu zigawanywe kwa mke, watoto watatu na nikawataja kwa majina, pia nikaeleza mtoto mmoja asihusike kwenye urithi wa Mali zangu bila kuweka wazi sababu za kufanya hivyo! Je, wosia wangu utabaki kuwa halali endapo nikifariki?

Je, ni mambo gani au mazingira gani yanaufanya wosia kuwa batili?
 
Wosia wako utakuwa halali hata kama utaacha mtoto mmoja nje kwa kuwa ndio mapenzi ya marehemu japo nadhani zipo sifa maake kama mtoto unayetaka kumuacha nje alikuwa mtegemezi kwako na hajafikia umri wa utu uzima nadhani hawezi kuachwa kwenye beneficiaries wa marehemu.
 
kwa hiyo umri wa mtoto utabatilisha wosia endapo hahatimiza miaka 18!? bado utata tena!
 
Mkuu nawe labda ureason kidogo maake sheria hutengenezwa kulinda haki. Unapomuacha mtoto wa miaka mitatu ambae alikuwa anakutegemea kama baba labda nje ya wosia unataka nani akusaidie kulea kama mali zako ambazo zingelisaidia kumlea hutaki kumpatia naye share yake
 
Utabaki halali sababu wosia hata siku moja hauwezi kubadilishwa...u can not challenge nor change a will.So kama umeandika asipewe ni hapewi kitu hata kimoja.
 
Na wosia utakua batili kama,kuna wosia zaidi ya mmoja so wataangalia tarehe yn whch one is current,thn kama haujasainiwa, na vitu vingne ila hayo ndo makubwa nayokumbuka
 
Utabaki halali sababu wosia hata siku moja hauwezi kubadilishwa...u can not challenge nor change a will.So kama umeandika asipewe ni hapewi kitu hata kimoja.
Shukrani sana kwa mchango wako Beatrice! hapa lazima maamuzi ya marehemu yaheshimiwe kwa kuwa hana uwezo wa kutoa maamuzi nengine wala kijitetea!
 
Sijui kwa imani zngine, lkn kwa imani nnayofuata mimi, mke na watoto, iwe umewapa chao ktk wosia ama hukuwapa, bado watarithi na kwa hiyo wasia wako ni batili!

Lkn pia kama uluchogawa ktk wasia ni kikubwa kuliko mali iliobaki baada ya wasia, wasia wako ni batili
 
kama ni hivyo kuna haja gani ya kuandika wosia? maana maamuzi ya marehemu lazima yaheshimiwe kwa maana hawezi kuubadili!
 
Mkuu hiyo ni kulingana na Imani yako ila kumbuka Wosia uliosainiwa na mwanasheria uko Kwa mujibu wa sheria za nchi huwezi enda tofauti kwa kuwa nchi haina dini/Imani
 
Kwa kuanzia na swali lilopo kwenye heading yako baadhi ya majibu ni haya,
1. ikiwa wosia haujasainiwa na aliyeuandika basi wosia huo utakua batili,
Q. Kama hakuna sahihi ya waliotuliwa kuwa shahidi
3. Mtu aliandika huo wosia pia anaweza batilisha yeyemwenyewe kama bado hajafa
Nikija kwenye maelezo ulotoa kuhusu mtoto mmoja kutohusika kwenye Mali zako,endapo wosia wako ukawa umefata matakwa ya sheria basi pindi aliyeandika huo wosia atafariki hakuna atakaye weza kubatilisha huo wosia.
 
Kama hakulezea sababu ni lazima mtoto huyo atapata
Na mtu huez kum exclude mtoto wako bila kumwambia
Ni lazima umwambie na mtoto atakua ana haki ya kukata rufaa kwenye kikao cha ukoo ikiwa anaona bado ana haki
 
Kwanza kabisa wosia
Umetafsiriwa Kwenye Tangazo la serikali namba 436 la mwaka 1963
ORDER NAMBA 4
 
Wosia utakua batili kama

Kumeandikwa wosia mwingine mpya

2. Kama mashahidi wote wamekufa

3. Kama hukuwekwa saini eidha ya dole gumba au ya kawaida

Pia kama HUKU wosia huo hukushuhudiwa na watu japo wawili toka kwenye ukoo wako

Kama ni wosia wa maneno utabatilishwa kama utaandikwa wa maandishi

Pia kama wosia huo utafanyiwa marekebisho kwa maana ya kufuta baadhi ya maneno au kuongeza kutafanywa na mtu ambae si testator
 
Endapo nitaandika wosia kuhusu jinsi gani Mali zangu zigawanye kwa wategemezi wangu kama mke watoto na ndugu!
mfano! Nina watoto wanne kwa mke mmoja na katika wosia wangu nikaeleza kuwa Mali zangu zigawanywe kwa mke, watoto watatu na nikawataja kwa majina,pia nikaeleza mtoto moja asihusike kwenye urithi wa Mali zangu bila kuweka wazi sababu za kufanya hivyo! Je, wosia wangu utabaki kuwa halali endapo nikifariki?
Je, ni mambo gani au mazingira gani yanaufanya wosia kuwa batili?
Sasa huyo mtoto mmoja unataka kumwacha kakukosea nini jamani? Au unakuwa na wasiwasi kuwa ulibambikiwa au alikusea sana adabu? Ukiacha hivyo kisheria wosia wako ni halali. Concern yangu katika mfano wako ni jinsi huyo mtoto atakavyojisikia ikiwa wote pamoja na mama yake wanapata mgao halafu yeye anatengwa.
 
Back
Top Bottom