SoC02 Mambo 7 Yanayoweza kupunguza tatizo la Ajira Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Mr Suprize

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
832
856
Kumekuwa na Maoni mengi ya wadau wakishauri Mtaala wa Elimu ubadilishwe , huu uliopo kwa Sasa hauendani na mahitaji ya Taifa letu kwa Sasa . Umeshindwa kabisa kutatua Changamoto ya Ajira na kuwafanya watumiaji wa Mtaala huu kutegemea Zaidi ajira za serikali. Kwa Maoni yangu nafikiri Ni sahihi uandaliwe Mtaala mwingine ambao utaachana kabisa na Mambo ya kukaririsha badala yake tuwe na Mtaala ambao utaenda kufanya Elimu kwa Vitendo na kuondokana kabisa kuwa Tegemezi wa Ajira za serikali.

Kipindi ambacho tunasubiri Maoni yetu ya kubadilisha Mtaala wa Elimu yafanyiwe kazi na Serikali tukumbuke pia Mtaala ukishabadilishwa kuona matokeo au matunda yake inawezekana Ni baada ya miaka 20 labda Kama Mtaala utapunguza Muda wa kupata Elimu mfano Elimu ya msingi iwe miaka 4 , Elimu ya Sekondari iwe miaka miwili, hapo tunaweza kusubiri kwa Kipindi kifupi na kuanza kuona matunda yake.

Bahati Nzuri sana Serikali ya awamu ya 6 imeanza mchakato wa kubadilisha mtaala, Sasa Kipindi hiki Serikali imeanza kufanya mchakato wa kubadilisha Mtaala wa Elimu Kuna Mambo kadhaa ningeshauri yafanyike Kama mpango wa Muda mfupi ili kuweza kukabiliana na Tatizo la Ajira linaloikumba nchi kwa Sasa.

1. Kazi zote za Serikali Za Muda mfupi wapewe vijana wasio na Ajira Rasmi.

Kazi Kama Sensa, Usimamizi wa uchaguzi , Shughuli za Anuani na makazi , kusahihisha mitihani ya mwisho ya Elimu (Msingi na sekondari) kugawa chanjo pale magonjwa ya mlipuko yanapotokea , watu waliopo kwenye ajira Rasmi wasiruhusiwe kupata kazi hizi za Muda badala yake wapewe wasio na Ajira Rasmi , Yale malipo au posho ambazo zinatolewa zingekuwa Kama chanzo Cha mtaji na kuweza kujiajiri. Na kwa Sababu kazi yoyote ya Muda ya serikali lazima kuwepo na Semina naamini hakuna kitachoharibika watapewa maelekezo/mafunzo Maalumu ya utendaji wa kazi husika , kikubwa mwombaji awe na sifa zinazohitajika , mfano wanahitaji vijana wa kugawa chanjo ya polio Basi mwombaji awe amehitimu hayo mafunzo.

2. Makampuni au viwanda na wageni wanaokuja kuwekeza hapa nchini Serikali ihakikishe 95% ya wafanyakazi wawe Ni watanzania . Naamini hii sheria ipo Lakini utekelezaji wake umekuwa bado Ni hafifu ningependekeza Serikali ipitie upya kuhakikisha Kama inatekelezwa ipasavyo.

3.Umri wa kustaafu upunguzwe Hadi kufikia miaka 45.
Kwa mawazo yangu Miaka 60 kazini Ni mingi sana hata ule ufanisi wa utendaji kazi unakuwa chini Sana hauwezi kufanana na mtu mwenye miaka 40 , tukiweka umri wa kustaafu uwe miaka 45 kwanza tutatoa fursa kwa anayestaafu kufanya shughuli zake za kifamilia na majukumu mengine akiwa bado Ana nguvu , Lakini pia tutakuwa tumeongeza nafasi za Ajira , Kama kila sekta kwa mwaka watastaafu watumishi elfu20 , kwa sekta 10 tutakuwa na watumishi waliostaafu Laki mbili (200,000) kwa maana Hiyo kwa kila mwaka tunahukakika wa kuzalisha ajira za uhakika 200,000 (Laki mbili).

4. Asilimia 50 ya mikopo Ya Elimu ya Juu mnufaikaji apewe baada ya kuhitimu Chuo.

Kwa mawazo yangu hii mikopo ingeangaliwa upya mnufaikaji nusu ya mkopo apewe wakati anasoma , halafu nusu nyingine ya mkopo apewe baada ya kumaliza masomo ili ukamsaidie kuweza kujiajiri hata kuanzisha biashara au ujasiriamali Kama vile ufugaji na kilimo , hii itasaidia pia kuweza kulipa mkopo wake bila kusubiri serikali imuajiri , kwa maana rahisi tufanye Kama wanavyofanya watumishi katika kupokea mishahara Yao kiasi kadhaa kinatengwa na anapewa baada ya kustaafu kazi ili kikamsaidie kujikimu Lugha rahisi tunasema kiinua mgongo.

5. Vyuo vya ufundi stadi (VETA) Viwe chaguo la kwanza kwa mhitimu wa Elimu ya msingi na Sekondari.

Huku ndo kunapatikana Elimu kwa Vitendo bahati mbaya Sana Jamii inachukulia VETA Kama Ni sehemu ya mwisho ya kupata Elimu , tunaamini mtoto kumpeleka VETA Hana akili ya darasani , Uzoefu wangu mtu aliyepitia VETA huwezi kumkuta analalamika Kukosa Ajira au Hamna Ajira , Hawa ndo mafundi pikipiki, magari , mafundi umeme, mafundi ujenzi , halafu huku mtaani wanapata pesa sana na wako kimya hawasemi, na Ni vijana wadogo Sana kwa siku kulala na shilingi elfu25 Hadi Elfu 50 Ni jambo la kawaida Sana.
Serikali ifanye linalowezekana kuviboresha hivi vyuo na ikiwezeka asilimia 45 ya wahitimu wa Elimu ya msingi na Sekondari wapangiwe VETA.

6. Serikali iangalie upya Teuzi zinazofanywa .

Kuna zile nafasi ambazo Serikali inafanya uteuzi kuanzia ngazi ya Serikali za mtaa , Halmashauri , Mkoa , Hadi Taifa kama vile nafasi za Wakurugenzi, Makatibu, Wakuu wa Wilaya (DC) Wakuu wa Mikoa(RC) Mawaziri n.k
Mara nyingi zimekuwa nafasi ambazo zinaenda kwa Viongozi ambao tayari Wamestaafu , au Kumpa mtu ambaye tayari Ana jina kubwa kiuongozi , ningeshauri Serikali Asilimia 40 ya Teuzi zinazofanywa ziwaguse vijana wapya ambao wametoka chuo na wanasifa Stahiki , wapewe nafasi waweze kuonyesha uwezo wao.

7.Kigezo Cha UZOEFU kisiwepo kwenye kuajiri.

Serikali itoe muongozo kwa makampuni ya serikali na binafsi yanapotaka kuajiri kuondoa kigezo Cha UZOEFU , unakuta Tangazo linamtaka mwombaji awe na uzoefu wa miaka 2 na kuendelea , hapo unakuta una miezi miwili tu umehitimu chuo uzoefu ungeupata wapi? Na je Ni Nani atawaajiri Hawa wasio na uzoefu ili nao wapate huo uzoefu?: Vijana wengi wanabaki mtaani kwa kukosa Uzoefu .

Nimalize Kwa Kusema Kwamba Serikali na Jamii kwa ujumla itambue kwamba Mwajiriwa mmoja anategemewa na watu wanne , inamaana ukimpa Ajira mtu mmoja fahamu kwamba unakuwa umewasaidia watu wanne kuweza kujikimu na maisha . Mshahara atakaopata ataweza kusomesha wadogo zake , atawatumia wazazi nyumbani wanunue Chumvi , Sabuni na mahitaji mengine ya Msingi . Asanteni
 
Mkuuu hapo kwenye pwenti nambari 5 panahitaji maboresho yanayokidhi kada zote ili kuboresha pwenti nambari 7 iweze kuwa na mashiko.
 
Elimu ni nini ?
 
Elimu ya veta inategemea na akili ya mtu
Elimu ya nadharia ndo inahitaji Sana Akili ya mtu Sasa VETA Mara nyingi wanahusika na Elimu kwa vitendo ambayo ni rahisi Sana mtu kuelewa , chukulia jamii za wakulima na wafugaji , mtoto hajui kusoma Wala kuandika lakin ukimpa jembe akalime huwezi kumfikia ,
 
Back
Top Bottom