nobodylikedme
JF-Expert Member
- Apr 5, 2018
- 741
- 769
Kipindi flani hivi wakati bado nasoma nilikuwaga naishi karibu na kota za polisi kwenye geto la mchizi wangu ambae nilikuwa namuita bro! Huyo bro alikuwa ni dereva tax tena day worker tu.Kuna wanawake wanaume zao wa ndoa wanahela nyingi lakini hawana amani, mwanaume mwingine Malaya mbwa (money source of Evil)!
Mungu azidi kutunusuru na mabaya!
Bora kuwa na kiasi !
Alitokea kuzoeana sana na mother mmoja hivi ambae alikuwa ameolewa na inspector wa polisi, kutokana na mazoea yao yaliyokuwa yanatia shaka nilimuuliza bro kama wana uhusiano wowote, ila yeye alinificha akakataa kuniambia ukweli akiofia kwamba mimi ni dogo sina siri nitaenda kumtangaza kwa watu.
Nikashangaa siku moja akapotea ghafla na ikapita wiki nzima aonekani geto bila taarifa yoyote, ikabidi niende kijiweni kwake kumuulizia kwa madereva tax wenzie. Kumbe bana yule bro alikuwa anatafutwa na polisi tena kwa kesi ya uvamizi wa kutumia siraha, kwa baadae nikaja kupata stori kamili kumbe bro alikuwa ana tembea na yule mke wa inspector na inspector aliamua kumsakizia kesi ya ujambazi baada ya kubaini anatembea na mke wake.
Nikikumbuka tulivyokuwa tunaishi huyo bro wangu alikuwa ni mpuuzi tu fulani hana hela lakini alikuwa ana mvua chupi mke wa inspector. Sasa nikionaga comments za watu humu eti mwanamke anatulizwa na pesa huwa naishia kucheka tu na kusikitika.