Mambo 4 ya kufanya mwanamke akupende

Mambo 4 ya kufanya mwanamke akupende

halafu kuna kitu lazima tutambue.Nilichokia-ndika mimi ni mambo ambayo yanaweza kukusaidida yeye mwanamke awe nakupenda mwenyewe.Na sio kum-badilisha mtu awe anakupenda.Hata ukikutana na mtu anaehitaji brazilian hair e.t.c.
ujue yeye hakupendi ila wewe unalazimisha mapenzi
 
habari Wana wa JF.Natumai muko sawa.
Leo Nashukuru mungu kuchukua fursa hii kwa mara nyengine tena kuwaelezea kile ninachokifahamu katika maisha.Nimekuja na mambo manne ukiwa nayo mwanamke atakupenda na utamfanya mkeo awe na furaha

1.KUWA NA HESHIMA.
Heshima inasababisha mwanamke kukupenda kwasababu utapokuwa na heshima una-epukana na dhararu na wanawake karibuni wote hawapendi kudharauliwa.Heshima ni miongoni mwa kumsikiliza mtu,kutoongea nae kwa maneno machafu,kutompiga pasi na sababu,kutofanya vitu ambavyo yeye havipendi,kuonesha unajali kwake n.k.

2.KUDHIHIRISHA UPENDO
Unapoishi onesha kwamba una upendo na kila mtu,kwasababu mwanamke anahitaji amani na maelewano.Unapokuwa na sura pamoja na moyo wa upendo kila mtu anavutika nawe na anakupenda sio mwanamke tu peke yake, na wala watu hawatokuchoka.

3.KUWA MWEREVU
Hutakiwi kuwa mjinga mbele ya jamii.Unatakiwa kuishi ki-professional.Kwa sababu mwanamke anajivunia sana anapokuwa na mwanamume mwenye busara,anahisi ni wato-fauti.Jaribu kuwa mkimya usiwe unaongea ovyo,kuwa mtaratibu na usiwe unakimbilia kutoa hukumu kabla ya kufikiri.
Fikiria kwanza,Ongea maneno madhubuti. Mimi binafsi, kwenye miaka kama 5 iliyopita kuna mtu alikuwa anapenda sana kuniambia maneno haya "I like the way you are".

4.KUWA NA UVUMILIVU
Wanawake ni watu wenye vituko sana.Na muda mwengine huwa ni kama tabia kwao wanapokuwa wanaumwa ama wana stress zao tu ki-kawaida.Sasa unatakiwa ufahamu kwamba wewe ni mwanamume unatakiwa kuvumilia na hivyo vituko na maudhi yote hayo.Unatakiwa kuwa mkimya na uweze kudhibiti hasira zako.Mwachie mtu mpaka ajitambue mwenyewe kama ana makosa.

Kujifunza tabia hizi utakuwa umeuteka moyo wa mwanamke
hayo yote pumba kama huna mtonyo aka ngawila
 
Matatizo yanawafanya watu wawe wana falsafa...Tafuteni pesa vijana, pesa, pesa, fedha, tafuteni hela kwa nguvu na maarifa hayo mengine yatajiseti yenyewe kwenye mfumo.
 
Wewe haujasema, hawa viumbe nawajua, ukiwa mpole watakufanya kanyagio..

Mim wananiita mwanajeshi..
 
Unazungumzia wanawake wa sayari ipi mkuu? Wanawake ni viumbe wasiotabirika.
Unaweza kuwa na sifa zote hizo ila akakuacha sabb huna chapa.
 
Matatizo yanawafanya watu wawe wana falsafa...Tafuteni pesa vijana, pesa, pesa, fedha, tafuteni hela kwa nguvu na maarifa hayo mengine yatajiseti yenyewe kwenye mfumo.
Uko right bro, vijana wafanye kazi.
lakini tukizungumzia mapenzi hayataki fedha.
na kama ikiwa unahonga ujue hujawahi kupendwa
 
Think first then talk smart, bro.
Unajua fedha baadhi ya sehemu haifanyi kazi na utakuja amini haya
siku ukisha-ipata.Nasema hiyvo kwasababu naijua hela na nimetumia vya kutosha so kuna baadhi ya sehemu hazitaki hela
Mzee mwenzangu,

Hela tunayoiongelea hapa ni ya kukidhi mahitaji muhimu ya kwako na ya kwake au familia yako.
Haina maana uwe na mahela kama Bakhresa.

Na wanaume tumetofautiana uwezo, na huo uwezo ndio tunapata wadada wa saizi yetu.

Ndio maana utasikia mdada anasema mm siwez kuwa na yule atanipa nini, ila huyo mwanaume sio atakosa Mwanamke, atapata wa saizi yake na ambaye pia huyo mwanamke wa saizi yake anasema pia mm siwez kuwa na mtu kama yule atanipa nn, only coz hana.uwezo kama wa mme wake..

Nadhan hapa sasa itapendeza
 
Yote hayo kisa papuchi wakati wazuri na wabaya wote wanataka kitu kimoja kutoka kwangu...wacha tuu nisake pesa nitaenjoy nao nitakavyo
Mwanaume ajue kujiongeza ajue kujitoa, akuheshim, akupende, akuthamini, akujali, akupe muda wake (itaingia hukohuko kwenye kujali)ajue kuvumilia awe na upeo mkubwa wa kufikiri nadhani huyu kwangu ana kila sababu ya kumpenda
 
Mpe pesa..
Mpe helaa..
Mpe faranga.
Money ndio kila kitu..
 
Nahangaika kutafuta pesa maana ndio kila kitu, nitachukua mwanamke yoyote nimtamaie kupitia chambo pesa, fweza ndio mpango mzima haya mengine ni kujichosha tu akili na mwili, kuwa na mwanamke huku unamnyenyekea kama vile ndiye Mungu muumba wa mbingu na nchi ilihali yeye akikutana na mwenye pesa haangalii kuwa kwako na heshima, kudhihirisha upendo, kuwa mwerevu au sijui uvumilivu. Hichi unachokizungumza hakipatikani tena ulimwengu huu hasa maeneo ya mjini.
unajidanganya sana,pole
hio pesa utaitafuta mpaka unakufa
 
Habari Wana wa JF.Natumai muko sawa,

Leo nashukuru Mungu kuchukua fursa hii kwa mara nyengine tena kuwaelezea kile ninachokifahamu katika maisha.Nimekuja na mambo manne ukiwa nayo mwanamke atakupenda na utamfanya mkeo awe na furaha.

1.KUWA NA HESHIMA.
Heshima inasababisha mwanamke kukupenda kwasababu utapokuwa na heshima una-epukana na dhararu na wanawake karibuni wote hawapendi kudharauliwa.Heshima ni miongoni mwa kumsikiliza mtu,kutoongea nae kwa maneno machafu,kutompiga pasi na sababu,kutofanya vitu ambavyo yeye havipendi,kuonesha unajali kwake n.k.

2.KUDHIHIRISHA UPENDO
Unapoishi onesha kwamba una upendo na kila mtu,kwasababu mwanamke anahitaji amani na maelewano.Unapokuwa na sura pamoja na moyo wa upendo kila mtu anavutika nawe na anakupenda sio mwanamke tu peke yake, na wala watu hawatokuchoka.

3.KUWA MWEREVU
Hutakiwi kuwa mjinga mbele ya jamii.Unatakiwa kuishi ki-professional.Kwa sababu mwanamke anajivunia sana anapokuwa na mwanamume mwenye busara,anahisi ni wato-fauti.Jaribu kuwa mkimya usiwe unaongea ovyo,kuwa mtaratibu na usiwe unakimbilia kutoa hukumu kabla ya kufikiri.
Fikiria kwanza,Ongea maneno madhubuti. Mimi binafsi, kwenye miaka kama 5 iliyopita kuna mtu alikuwa anapenda sana kuniambia maneno haya "I like the way you are".

4.KUWA NA UVUMILIVU
Wanawake ni watu wenye vituko sana.Na muda mwengine huwa ni kama tabia kwao wanapokuwa wanaumwa ama wana stress zao tu ki-kawaida.Sasa unatakiwa ufahamu kwamba wewe ni mwanamume unatakiwa kuvumilia na hivyo vituko na maudhi yote hayo.Unatakiwa kuwa mkimya na uweze kudhibiti hasira zako.Mwachie mtu mpaka ajitambue mwenyewe kama ana makosa.

Kujifunza tabia hizi utakuwa umeuteka moyo wa mwanamke
Nadhani ungezifanya ziwe 5, hii ya 5 ingezungumzia kuwa mtu mtafutaji mwenye uwezo wa kuitunza familia. Hapa mwanamke atakuwa secure.
 
Back
Top Bottom