Mambo 4 ya kufanya Instagram kupata followers zaidi

frado

Member
Nov 26, 2020
8
23
Profile visits ni idadi ya watu wanaotembelea ukurasa wako wa Instagram

unaweza kuangalia kupitia insights kufahamu kuhusu profile visits kupima maendeleo ya ukurasa wako

Ili kuwa na profile visits kubwa unapaswa kufanya mambo yafuatayo

BIO OPTIMIZATION
Hiki ni kitendo cha kutumia maneno sahihi ili watu wanapoperuzi Instagram katika niche yako iwe rahisi kukufikia

Angalia jina unalotumia katika BIO yako

Angalia category uliyochagua, je inaendana na Description uliyoweka ?

Imagine unauuza Nguo halafu jina umeandika Genious gangster 😀 (Are You serious?)

PICHA
picha katika profile yako inatoa details ya biashara yako au brand yako

kuwa makini na kuweka picha ambazo hata mtu akikutana na post yako anapata uoga

imagine umeweka Zombi HALAFU biashara yako ni kuuza Nguo za watoto 😭 Wazazi hawatakuamini ndugu

SPONSORED ADS
Haya ni matangazo ya kulipia, unapofanya sponsored ads kuna malengo makubwa matatu

Moja ya lengo ni profile visits na unapolipia Instagram wanahakikisha wanasambaza ukurasa wako kwa watu wengi zaidi

Hii ni uhakika kabisa

KEYWORD
kila unapo post hakikisha unatumia KEYWORDS yaani maneno muhimu katika ukurasa wako

Haya ni maneno ambayo yanatambulisha biashara yako lakini pia yanatafutwa zaidi na watu

Hii itakusaidia watu kutembelea profile yako na hivyo kupata PROFILE VISITS za kutosha na hatimae followers na mauzo zaidi

unaweza pia kutumia keywords kama TAGS kuongeza profile visits

Kuna kitu kinaitwa Topic katika Instagram, nitaandaa siku maalumu kufundisha kuhusu feature hii mpya na namna ya kuitumia ili kufanya OPTIMIZATION

Umefurahi na kujifunza ?

20221123_192748.jpg
 
Back
Top Bottom