Mambo 10 yaliyofanyika katika Wizara ya Elimu ndani ya muda mfupi

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Tangu alipoingia madarakani juhudi za Rais Samia Suluhu katika kuboresha huduma kama vile Elimu, Afya na upatikanaji wa Maji safi na salama ni vipaumbele vilivyo wazi.

Baadhi ya jitihada muhimu zilizofanyika ndani ya muda mfupi katika sekta ya Elimu ni pamoja na;

1. Ujenzi wa Shule mpya za sekondari na shule ya msingi zipatazo 266.

2. Ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa ya shule za msingi, vituo shikizi, na shule za sekondari vipatavyo 18,219.

3. Ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa shule za msingi na sekondari vipatavyo 4,525.

4. Ukamilishaji ujenzi wa vyumba vya maabara vipatavyo 1,399.

5. Ujenzi wa matundu ya vyoo kwa shule za msingi na sekondari yapatayo 568.

6. Ujenzi wa mabweni kwa shule za msingi na sekondari yapatayo 170.

7. Ujenzi wa nyumba za walimu wa shule za msingi na sekondari zipatazo 42.

8. Kutolewa ajira za walimu wapatao 9800 wa kada tofauti tofauti.

9. Watumishi katika wizara ya Elimu kwa maana ya walimu, waratibu wa Elimu na Maafisa Elimu kulipwa malimbikizo na madai yao yote yaliyohakikiwa.

10. Kutolewa fedha za Mikopo ya Elimu ya juu na kuondolewa kwa tozo ya VRF kiasi cha asilimia 6 kwa wanufaika wa Bodi ya Mikopo.

Rais Samia Suluhu anachapa kazi na anastahili pongezi za dhati kutoka kwa watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi hii. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MMBARIKI RAIS WETU
 
Tatizo sio hayo uliyayaainisha kama mafanikio!

TATIZO ni end product ya Elimu yenyewe!!

YAANI mhitimu anatembea na Bahasha akitafuta ajira na ajira HAMNA na elimu haikumuandaa kujiajiri!

Tatizo Ndio hilo Hata kama ajenge madarasa kama utitiri kama Elimu HAINA tija HAINA TU!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"!
 
CCM nzima hamna mwenye akili ya kuwaza kama ulivyowaza.
 
Kwakweli hatutakaa tutoboe Kama nchi licha ya rasilimali tulizonazo lowasa alisema Elimu Elimu Elimu wale amabao hawajasoma na hawajui maana ya Elimu kina msukuma wakasema kazeeka vibaya amejinyea....kijani ndio tatizo lenyewe ambao hawana Elimu ndio wako kwenye usukani wa Mambo nyeti
 
Hakika yamefanyika na ni pongezi kubwa kwa rais na serikali yake.Nguvu ikiwezwa zaidi katika kuandaa elimu hasa ya uzalishaji kwa maana ya ufundi kwa aina zake,tutaiona Tanzania yenye wasomi wenye tija katika nyanja mbalimbali
 
SSH hajui propaganda ndio maana hata akifanya makubwa mangapi yanaonekana kama vile hakuna anachofanya.
 
Mkuu tupa shuka pembeni amka jinyooshe kumeshakucha. Upo afrika haupo ulaya au Marekani.
Rwanda wanarusha satellite yao na hawapo ulaya wala marekani. Licha ya vita vya muda mrefu, hawajivunii matundu ya choo bali kutengeneza simu zao, magari yao na sasa kurusha satellite yao. Kila mwanafunzi ana laptop yake na mtandao wazi tu... wana mengi ya kutufunda japo hawana bahari wala bandari kama sisi.
 
Mkuu nenda Rwanda kama unaona Tanzania imechelewa sana. Tazama ukubwa wa eneo analoongoza Kagame halafu linganisha na la Tanzania analoliongoza Samia, vitu viwili tofauti.

Rwanda kwa eneo inaweza kuwa ndogo kulinganisha na mkoa wa Kagera peke yake hapo hujaweka mikoa ya kanda ya ziwa kwa pamoja.
 
Tatizo sio hayo uliyayaainisha kama mafanikio!

TATIZO ni end product ya Elimu yenyewe!!

YAANI mhitimu anatembea na Bahasha akitafuta ajira na ajira HAMNA na elimu haikumuandaa kujiajiri!

Tatizo Ndio hilo Hata kama ajenge madarasa kama utitiri kama Elimu HAINA tija HAINA TU!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"!
Serikali ya awamu ya sita inamtengenezea mwanafunzi au kijana mazingira ya kujiajiri endapo asipoajiriwa inagawa mashamba kwa vijana ili vijana wajiajiri katika kilimo pia imejenga vyuo vya veta mikoa yote Tanzania ili wahitimu wa ufundi waweze kupata uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa kwaiyo mikakati ya ajira mingi sana
 
Wengine wanaenda sayari za juu hapa kwetu wakereketwa wanahesabu ujenzi wa matundu ya choo kama maendeleo ya kujivunia.
Serikali ya awamu ya sita imefanya maendeleo mengi sana ukiachana na hili la Elimu unaweza ukaangalia katika sekta ya afya saizi hospital mpaka vijijini huduma ya mama na mtoto imeboleshwa pia gharama ya kilimo imepungua
 
Kwakweli hatutakaa tutoboe Kama nchi licha ya rasilimali tulizonazo lowasa alisema Elimu Elimu Elimu wale amabao hawajasoma na hawajui maana ya Elimu kina msukuma wakasema kazeeka vibaya amejinyea....kijani ndio tatizo lenyewe ambao hawana Elimu ndio wako kwenye usukani wa Mambo nyeti
Ndio maana Rais Samia Suluhu amewezesha elimu bure ili kila mtanzania aondokane na ujinga,
inatakiwa kupambana sana na ujinga na umasikini nchi yetu itasimama kwaiyo sekta ya elimu ni sekta muhimu sana
 
SSH hajui propaganda ndio maana hata akifanya makubwa mangapi yanaonekana kama vile hakuna anachofanya.
Sure yeye kazi yake ni kuleta maendeleo Tanzania hana muda wa kujisiia na kutengeneza story ndio maana hajari hata watu wakisema nini yeye anajari kazi yake ya utekelezaji tu na wale wanaopinga wanapinga tu kwasababu wamezoea upinga lakini moyoni wanakubali mambo makubwa ya mama
 
Hakika yamefanyika na ni pongezi kubwa kwa rais na serikali yake.Nguvu ikiwezwa zaidi katika kuandaa elimu hasa ya uzalishaji kwa maana ya ufundi kwa aina zake,tutaiona Tanzania yenye wasomi wenye tija katika nyanja mbalimbali
kweli kabisa Rais Samia Suluhu ameamua kupambana na ujinga na umasikini hawa ndio adui zetu wakubwa katika kuleta maendeleo
 
Rwanda wanarusha satellite yao na hawapo ulaya wala marekani. Licha ya vita vya muda mrefu, hawajivunii matundu ya choo bali kutengeneza simu zao, magari yao na sasa kurusha satellite yao. Kila mwanafunzi ana laptop yake na mtandao wazi tu... wana mengi ya kutufunda japo hawana bahari wala bandari kama sisi.
Tulia kila kitu kitawezekana chini ya Rais Samia Suluhu sasa ameanza kwa kutoa ada mashuleni ili watoto wote wapate haki yao ya msingi ya kusoma na amebolesha mazingira ya kusomea amejenga vyumba vya madarasa, walimu wa kutosha pia madawati ya kutosha kwaiyo tunaenda step by step uko kwenye pc tutafika tu kwa kasi hii ya maendeleo
 
Mkuu nenda Rwanda kama unaona Tanzania imechelewa sana. Tazama ukubwa wa eneo analoongoza Kagame halafu linganisha na la Tanzania analoliongoza Samia, vitu viwili tofauti.

Rwanda kwa eneo inaweza kuwa ndogo kulinganisha na mkoa wa Kagera peke yake hapo hujaweka mikoa ya kanda ya ziwa kwa pamoja.
Kwani setilite,au uumdwaji wa magari unategemea ukubwa wa nchi au mipango?nilitegemea nchi kama Tz tufanye makubwa wewe unaongeleo eneo!
 
Rais Samia anajitaidi sana kuleta maendeleo lakini watu wengine wanataka kupinga kila kitu elimu ya Tanzania ya sasa japokua ni elimu bure lakini imeboleshwa sana saizi hakuna tofauti ya government school na private school
 
Tulia kila kitu kitawezekana chini ya Rais Samia Suluhu sasa ameanza kwa kutoa ada mashuleni ili watoto wote wapate haki yao ya msingi ya kusoma na amebolesha mazingira ya kusomea amejenga vyumba vya madarasa, walimu wa kutosha pia madawati ya kutosha kwaiyo tunaenda step by step uko kwenye pc tutafika tu kwa kasi hii ya maendeleo
Wewe jamaa ni mwongo sana sisi tumepeleka watoto Kishoju secondary Muleba tumelipishwa ada.wewe uko nchi gani?nenda hiyo shule ukaulize kama wazazi hawajalipa ada.acha siasa za mitandaoni tena wengine walirudishwa kwa kukosa ada halafu wewe unadanganya watu.fanya tafiti kabla ya kukurupuka bwashee
 
Kwani setilite,au uumdwaji wa magari unategemea ukubwa wa nchi au mipango?nilitegemea nchi kama Tz tufanye makubwa wewe unaongeleo eneo!
Punguza jazba kila kitu kinawezekana kwanza angalia maedeleo aliyoleta Rais Samia Suluhu ndani ya siku 535 sasa imagine mpaka kufikia 2025 atakua amefanya mamb mangapi
 
Back
Top Bottom