Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 473
- 1,682
1. Kama hukuangalia gemu ya jana baina ya Inter Milan vs Barcelona basi umekosa raha ya dunia, it was a real outstanding kama alivyokuwa akisema commentator.Gemu ya kasi sana, uwezo, ufundi, ujuzi na mbinu za hali ya juu zilizopelekea gemu kwenda extra time.
2.Nimejifunza kuwa timu hata ikifungwa mabao ya hovyo hailalamiki halalamiki kama Mashujaa au JKT au Yanga, inaweka mpira kati na inapambana kama walivyofanya Barxcelona.Barca wamethibitisha kuwa mpira ni mchezo unaoonekana uwanjani, kama refa kakosea kibinadamu we endelea kupambana hadi mwisho na ndivyo ilivyokuwa kwa Barcelona.
3.Mwamuzi kwa namna alivyokuwa akichezesha ukiangalia kwa jicho la washabiki wa Yanga au Mashujaa ungeweza kusema kuwa Inter walikuwa wanaandaliwa mazingira ya kwenda fainali lakini kumbe wapi, tuheshimu taaluma za watu.
4.VAR kuna wakati waamuzi wanasema ukweli na kuna wakati wanachemka hata wakiangalia VAR.
5.Barcelona wana vijana wana moto sana na sijui kama Madrid watatoka hiyo tarehe 11 kwenye ligi ya Spain, Inter Milan wanaubonda lakini wazee wengi.
6.Ni mchezo ambao haukuwa wa kupoteza muda kama wanavyofanya Mashujaa, mchezo umepigwa mwanzo mwisho na mgeni wa mechi hiyo Barcelona amekimbiza as if they were playing in their homeground.Ndivyo tutakavyowapelekea moto RS Berkane huko huko kwao Morocco.
7.Kuongezwa kwa dakika 5 ilikuwa ni discretion ya mwamuzi lakini kwa namna mchezo ulivyokuwa ukipigwa, dakika 5 naziona zilikuwa nyingi sana na wachambuzi wetu kama akina Ambokile kuongezea kwa dakika 5 na Inter kuchomoo bao angesema kulikuwa na nia ovu.
8.Mliona tukio la Inter Milan kusawazisha goli? Beki wake wa kulia alimchezea rafu mchezaji wa Barca refa akapeta na jamaa wakaenda kusawazisha, hili ni fundisho kwa wachambuzi wajinga wajinga kama Ambokile, kuwa wakati mwingine mambo kama yale yanatokea uwanjani na sio mapenzi ya mwamuzi.
9. Tuwe na adabu na mpira, mtanange wa jana umedhihirisha kuwa waamuzi wa Tanzania wanafuata sheria 17 za mchezo, mwamuzi wa Inter vs Barca hakuwa na tofauti na waamuzi wa Simba vs Mashujaa isipokuwa wajinga wajinga na malofa wengi kama akina Ambokile wako katika mpira wetu kutafuta manufaa, sifa na followers.Mtu kapelekwa Pemba tu kuangalia fainali ya Muungano anajidhalilisha utadhani amekwenda ulaya au Marekani.
10. Ndugu zangu wanasimba tusibweteke, Yanga wanawazuga kuwa hawachezi kumbe wanapanga mipango yao kimya kimya, andaeni timu, wataleta timu uwanjani, mkiwa mnafikiria kuwa hawateleta timu uwanjani mtakuwa mnajidanganya, hiyo ni mbinu yao ili nyie msifanye maandalizi kabambe na mikakati ya kufa mtu wao wakiendelea kufanya makafara makubwa makubwa, chukueni tahadhari, wameshapanga kucheza hiyo mechi ila wanawazubaisha nyie.