Hashpower7113
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 1,353
- 2,137
Jina lake halisi anaitwa Shawn Carter ingawa anafahamika zaidi na mashabiki wake kwa jina la Jay Z. Ni mwanamuziki mkubwa wa Hip Hop duniani, prodyuza na mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa. Yafuatayo ni mambo 10 kumhusu mchizi huyu ambaye ni mume halali wa Beyonce Knowles:
1. Alizaliwa na kukulia uswazi kwenye mtaa wa watu weusi uitwao Marcy, Bedford nje kidogo ya Brooklyn jijini New York.
2. Katika familia yao, wamezaliwa wanne na walilelewa na mama yao, Gloria Carter baada ya baba yao kuitelekeza familia tangu wakiwa wadogo.
3. Akiwa na umri wa miaka 12, alimpiga risasi ya bega kaka yao mkubwa kwa madai kwamba alimuibia mkufu wake.
4. Jay Z alisoma shule moja (George Westinghouse) na marapa wengine wakubwa, Notorious B.I.G. na Busta Rhymes.
5. Licha ya kufanikiwa kufika Chuo Kikuu cha Trenton Central, New Jersey, Jay Z hakumaliza masomo yake kutokana na utukutu, akaacha chuo.
6. Baada ya kuacha chuo, amewahi kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya (Cocaine) hadi alipoingia kwenye muziki.
7. Mpaka sasa, Jay Z anatajwa kuwa bado anaendelea kuvuta bangi na kutumia Cocaine.
8. Kutokana na utukutu wake na biashara ya madawa ya kulevya, Jay Z amewahi kupigwa risasi mara tatu lakini mara zote aliponea tundu la sindano.
9. Amewahi kukamatwa na kutupwa nyuma ya nondo baada ya kuanzisha fujo klabu na kumchoma kisu cha tumbo mtu mmoja aitwaye Lance Rivera.
10. Amewahi kutua Bongo kimyakimya na kwenda mpaka Mwananyamala, akiwa na mkewe, Beyonce kwenye uzinduzi wa mradi mkubwa wa visima vya maji.
Kama unayajua mengine, tupia!