Ndugu yangu huwa nawashangaa hao maliasili,kwan wanyama wetu huwa wanauawa pasipo sababu tu, mara ngapi tumesikia mamba,simba,fisi,tembo na koboko kule tabora na nk kuuwawa badala ya kudhibitiwa na kurudishwa ktk maeneo yao ya asili wao uwauwa tu. Ifike mahali iwe mwisho kuuwawa kwa wanyama wetu,kwani kuna siku tutawaangamiza wenyewe.
Pia itolewe elimu ya kuwajali wanyama wetu.
Kuna kipindi kule Rorya waliuwawa tembo watatu pasipo sababu,baada ya hao wanyama kuoneka maeneo TOTO kule Rorya hao jamaa wa game walitoa amri wauwawe,kweli waliuwawa wao game wakachukua tu zile pembe tu,lakin ukiangalia pale hao game walikuwa na uwezo wa kuwapiga risasi za usingizi kisha kuwabeba na kuwarudisha kule serengeti.
Ipo siku wanyama wetu waangamia na moja wapo wa kuwaangamiza ni hao idara ya wanyama haswa game.