Mamaake ni Single Mother lakini kamkataza asioe Single Mother

Mamaake ni Single Mother lakini kamkataza asioe Single Mother

Hivi mama yake anaweza kumuonea wivu mtoto wake? Kuna jambo zito mama yake analo na hawezi kulisema..hivi anaweza kumwambia pamoja nikiwa kwenye ndoa na baba yako bado nilikuwa natoka na baba yake Davie?

Mama sio Mungu Mkuu😆
Kama hana hoja atapingwa tuu.
Lakini kimsingi lazima awe na hoja. Kijana Mdogo miaka 35 hujawahi kuoa, hujawahi kuwa na mtoto. Unawezaje kuoa mwanamke mwenye mtoto? Nafikiri hilo wazazi wengi huliona kama kijana kujibebesha mizigo isiyoyake bila sababu na ambayo haina tija kwake wala future yake
 
Robert ulimkwepa jamaa na bahati nzuri anaifahamu misimamo yako.

Kumbe wewe ni muoga ukiwa face to face na mtu, ni jasiri sana kwenye kuandika nimeshakujua.

Kama unaamini single mothers ni wabovu, basi ni wabovu wote kwa vijana wote bila kujali hali zao kiuchumi.

Kusema huyu anaweza kuwa mzuri jaribisha, simply because jamaa yuko vizuri kiuchumi, naona haukumpa ushauri mzuri, na mbaya zaidi uliyumba kimsimamo wako.

Kijana ningemshauri aoe tu, mama sio malaika kila anachosema mtoto akifuate.
 
kama bado anasubiri kila mtu aridhike… basi hata akioa leo, bado hatakuwa ameoa ,ataendelea kuidhinishwa kila hatua ya maisha yake.
Zamani nilikuwa na mawazo au mtazamo kama wako kwamba wazazi hawana nafasi ya kuzuia usimuoe mwanamke fulani. Au mwanamke asiolewe na mwanaume fulani.
Amini nakuambia ile kitu inaitwa radhi au laana (family curse) ya wazazi ipo kwenye suala hili la ndoa.
Ukilazimisha ukaoa/kuolewa na mzazi wako akakomaa na kinyongo na katazo lake.
Utakutana na mambo mazito sana kwenye hiyo ndoa, kibaya zaidi hii curse inawaathiri hadi watoto wako uliozaa na huyo mwenza aliyekataliwa na mzazi wako.
Trust me, I have seen it sereval times, different victims.
 
Robert ulimkwepa jamaa na bahati nzuri anaifahamu misimamo yako.
Sijamkwepa jamaa. Nilimpa kile ambacho kinahitajika.

Kumbe wewe ni muoga ukiwa face to face na mtu, ni jasiri sana kwenye kuandika nimeshakujua.

😄😄
Unapomshauri mtu jambo lolote hasa sensitive kuna mambo ya kuzingatia.
Sio kwamba ninaandika vile basi nimmwage moja Kwa moja.
Mpaka ananitafuta ni kwamba anahitaji msaada.

Siwezi kumwambia single mother ni mbaya moja kwa moja wakati tayari amenipa CV yake njema.
Nilichofanya ni kumpa ushauri wa kumpa mtihani wa Subira ili kumpima huyo mfamasia kama ni msikivu, anamuamini, na anasubira(uvumilivu) huku muda huo akijaribu kuona kile ambacho haoni wakati mamaake anakiona. Pia Mamaake kuona kile ambacho kijana anakiona.

Mwisho, muda ndio utampa majibu sahihi.

Kama unaamini single mothers ni wabovu, basi ni wabovu wote kwa vijana wote bila kujali hali zao kiuchumi.

Single mother wote sio wabovu ingawaje tunatumia neno general ili kuwahamasisha vijana wawe makini lakini pia Kwa wadada wasio single mother wajihami.

Kingine wakati mwingine changamoto za single mother sio tabia mbaya walizonazo. Isipokuwa udhaifu na wanaume kutokuwa na uwezo naa uchumi thabiti kutunza mwanamke na mtoto. Hali inayopelekea migogoro.

So tunaposema sema vijana wasioe single mother wengi wanafikiri ni matatizo ya single mother Pekee bali tunazungumzia pia uwezo wa vijana wadogo kubeba majukumu ya kutunza familia mbili ni Jambo gumu.
Kusema huyu anaweza kuwa mzuri jaribisha, simply because jamaa yuko vizuri kiuchumi, naona haukumpa ushauri mzuri, na mbaya zaidi uliyumba kimsimamo wako.

Sijamwambia ajaribishe. Soma vizuri.

Mimi kama Mtibeli na Watibeli wengine hatuingilii mipaka ya watu wengine. Ikiwemo Uhuru WA mawazo na maamuzi.

Anganiuliza ingekuwa wewe ungefanyaje jibu lingekuwa rahisi, naye anajua jibu.
Lakini yeye na watu aina yake hawaoni shida kuoa single mother

Mwisho, msingi mkuu wa tatizo lake sio kuoa single mother kama ukifuatilia mazungumzo yetu. Na Mimi kama mwanasaikolojia na sosholojia. Nikamshauri kulingana na msingi wa tatizo lake linalomsibu.

Ambalo ni Mama kumzuia yeye asioe Single mothers.
So tatizo lake halipo kwa eye kuoa single mothers Bali kuzuiwa kuoa single mother.

Ndio maana nikamshauri ajipe muda ili aone kile ambacho Mamaake anakiona ambacho yeye hakioni.
Pia asiharakishwe na huyo binti kwani mambo mengine ya mahusiano yanaweza kuendelea huku ndoa ikisubiri
 
Zamani nilikuwa na mawazo au mtazamo kama wako kwamba wazazi hawana nafasi ya kuzuia usimuoe mwanamke fulani. Au mwanamke asiolewe na mwanaume fulani.
Amini nakuambia ile kitu inaitwa radhi au laana (family curse) ya wazazi ipo kwenye suala hili la ndoa.
Ukilazimisha ukaoa/kuolewa na mzazi wako akakomaa na kinyongo na katazo lake.
Utakutana na mambo mazito sana kwenye hiyo ndoa, kibaya zaidi hii curse inawaathiri hadi watoto wako uliozaa na huyo mwenza aliyekataliwa na mzazi wako.
Trust me, I have seen it sereval times, different victims.
Ndoa nyingi zinazopingwa na wazazi tayari huwa na migogoro kabla hata ya ndoa utakuta ni tofauti za tabia, malezi, dini, au hali ya maisha.

Wazazi wanapokataa, mara nyingi wanakuwa wameona viashiria fulani, sasa ndoa ikija kupata matatizo, watu wanaona ni laana wakati kiuhalisia matatizo yalikuwepo tayari.


Ukiingia kwenye ndoa ukiwa na hofu kuwa “nimekosa radhi ya wazazi, mambo lazima yataharibika” hiyo hofu inakuwa kama mbegu ya kujiharibia. Unaanza kuona kila tatizo kama uthibitisho wa laana, unakuwa na stress, mawasiliano yanaharibika, na ndoa inaanza kuyumba.

Una uelewa na self-fulfilling prophecy?

Ile hali ya kuamini kitu kitatokea, halafu matendo yako yanakifanya kitokee, ndo kitu kinachowatokea wengi.
 
Wazazi wanapokataa, mara nyingi wanakuwa wameona viashiria fulani, sasa ndoa ikija kupata matatizo, watu wanaona ni laana wakati kiuhalisia matatizo yalikuwepo tayari.
Na watoto wanapopata majanga unaizungumziaje?
Mkuu mimi mgumu kuamini mambo ya uchawi, Imani za kufikirika, na mengi ya muundo huo.
Lakini kwenye hili nakuhakikishia nimeona mengi kupitia ndugu na wabaki.
Nimeona mengi sana, umri wangu mkubwa kidogo najiweka kundi la wazee sasa japo sijafikisha 50.
 
Sio kwamba Mama anahofu inayotokana na historia ya dunia?

Kwa tabia ya jamaa sijui. Maana ni wale wasio na maamuzi hasa maamuzi yenye tija
Hakuna cha historia ya dunia anayajua kiundani zaidi ndio maana... aidha kupitia kwake ama kwa wenzake, mwanamke anamjua vizuri mwanamke mwenzie..
Hapo habahatishi anamueleza anachokijua
 
Sijamkwepa jamaa. Nilimpa kile ambacho kinahitajika.



😄😄
Unapomshauri mtu jambo lolote hasa sensitive kuna mambo ya kuzingatia.
Sio kwamba ninaandika vile basi nimmwage moja Kwa moja.
Mpaka ananitafuta ni kwamba anahitaji msaada.

Siwezi kumwambia single mother ni mbaya moja kwa moja wakati tayari amenipa CV yake njema.
Nilichofanya ni kumpa ushauri wa kumpa mtihani wa Subira ili kumpima huyo mfamasia kama ni msikivu, anamuamini, na anasubira(uvumilivu) huku muda huo akijaribu kuona kile ambacho haoni wakati mamaake anakiona. Pia Mamaake kuona kile ambacho kijana anakiona.

Mwisho, muda ndio utampa majibu sahihi.



Single mother wote sio wabovu ingawaje tunatumia neno general ili kuwahamasisha vijana wawe makini lakini pia Kwa wadada wasio single mother wajihami.

Kingine wakati mwingine changamoto za single mother sio tabia mbaya walizonazo. Isipokuwa udhaifu na wanaume kutokuwa na uwezo naa uchumi thabiti kutunza mwanamke na mtoto. Hali inayopelekea migogoro.

So tunaposema sema vijana wasioe single mother wengi wanafikiri ni matatizo ya single mother Pekee bali tunazungumzia pia uwezo wa vijana wadogo kubeba majukumu ya kutunza familia mbili ni Jambo gumu.


Sijamwambia ajaribishe. Soma vizuri.

Mimi kama Mtibeli na Watibeli wengine hatuingilii mipaka ya watu wengine. Ikiwemo Uhuru WA mawazo na maamuzi.

Anganiuliza ingekuwa wewe ungefanyaje jibu lingekuwa rahisi, naye anajua jibu.
Lakini yeye na watu aina yake hawaoni shida kuoa single mother

Mwisho, msingi mkuu wa tatizo lake sio kuoa single mother kama ukifuatilia mazungumzo yetu. Na Mimi kama mwanasaikolojia na sosholojia. Nikamshauri kulingana na msingi wa tatizo lake linalomsibu.

Ambalo ni Mama kumzuia yeye asioe Single mothers.
So tatizo lake halipo kwa eye kuoa single mothers Bali kuzuiwa kuoa single mother.

Ndio maana nikamshauri ajipe muda ili aone kile ambacho Mamaake anakiona ambacho yeye hakioni.
Pia asiharakishwe na huyo binti kwani mambo mengine ya mahusiano yanaweza kuendelea huku ndoa ikisubiri
Naamini sensitivity ipo kwenye makala zako unazoandika humu, so ningetegenea kuona msimamo wako humu kwenye makala zako unaupeleka kwa huyo jamaa kama ulivyo.

Sio kuanza kumtazama kwanza usoni, ili umuone kama anatia huruma kisha ulegeze msimamo wako kwa ajili ya jambo lake.

Kwangu mambo ya kujipa muda amuangalie single mother wake kitabia naona ni kulegeza msimamo wako, hawa watu wote wana tabia zao, na binadamu wote tuna mapungufu yetu.

Kama tukianza kuchunguzuna sana hakuna yeyote kati yetu atakayetoka salama kwa mwenzake, ujue tu huyo jamaa mpaka anakuja kwako kutaka ushauri wako, basi yeye tayari ameshamuelewa sinhle maother wake.

Kwako alikuja kutafuta tu sifa za nyongeza kwa ajili baby wake, na bahati nzuri alivyokuonesha pia ukamimina sifa za kutosha!.
 
Hiyo hata mimi ningekataa. 😹😹
Single maza hapana waoane na single daddy walee magoli yao ya mechi za nje..!!

Kukubali mjukuu sio wako kazi sana 🤣
 
Mzazi mwizi hawezi kufurahi mwanaye kuwa kibaka.

Hakuna mzazi anayependa mwanaye apitie njia 'mbofu mbofu' pamwe changamoto kama alizopita yeye.

Kwa hiyo huyo single mama, yupo sahihi katika kumtakia heri mwanaye katika njia zilizo bora za kuishi.
😹😹😹 Hakuna mwanamke atakubali kijana wake aoe single maza hata kwa fimbo labda kijana alazimishe..!!

Sema wanaume muwe mnaoa hao wanawake mnaowapa mimba kupunguza single maza nchini..!!
 
Mama sio Mungu Mkuu😆
Kama hana hoja atapingwa tuu.
Lakini kimsingi lazima awe na hoja. Kijana Mdogo miaka 35 hujawahi kuoa, hujawahi kuwa na mtoto. Unawezaje kuoa mwanamke mwenye mtoto? Nafikiri hilo wazazi wengi huliona kama kijana kujibebesha mizigo isiyoyake bila sababu na ambayo haina tija kwake wala future yake
Ni zaidi ya hilo la kujibebesha mzigo kuna mengine mengi zaidi mama anayajua
 
Huyu anakosa sifa za kumiliki mke, atasokotwa akamlilie mama yake. Mshauri asioe kwanza, avute vute subira.
 
MAMAAKE NI SINGLE MOTHER LAKINI KAMKATAZA ASIOE SINGLE MOTHER.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Rafiki Yangu wa shule(A'Level) na chuo kikuu amenipigia akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa.

2. Kitabia ni Mpole, sio mtu wa maneno mengi. Mtu wa Amani, asiyetaka vuruguvurugu. Sio mtu wa Principles na makanuni kanuni kama Mimi.
Wengi humuita mtu piece. Kwa Sisi wataalam tunamtambua kama Niceman.

3. Wakati tukiwa chuo alikuwa anadhulumiwa kutokana na huruma zake. Boom likitoka washkaji wanamkopesha kwa ahadi ya kumrejeshea. Lakini hakuna aliyewahi kurudisha.
Basi jamaa Kila mara alikuwa akinilalamikia. Nikamwambia wakikutaka wakikope walete kwangu.

4. Basi tukiwa vimbwetani tulikuwa tunataniani na bahati nzuri unavyojitambulisha ndivyo unavyochukuliwa. Fikiria MTU akukope laki moja, asirudishe, alafu aje tena miezi kadhaa mbele akukope elfu hamsini, asirudishe, achukue PC yako aseme imeibiwa ubaki umeng'aa. Basi ndivyo tabia ya Rafiki Yangu hiyo.

5. Mwenyewe nilipomuuliza why yupo hivyo. Anasema hapendi migogoro, Sijui vurugu. Lakini niligundua anatabia ya Uoga, kutojiamini na MTU wakuigulia ndani kwa ndani.

6. Miaka zaidi ya kumi imepita tangu tumalize chuo kikuu. Hatujaonana zaidi ya mitandaoni huko na mara mojamoja kuwasiliana kwenye WhatsApp

7. Hivi karibuni alinipa wito tuonane. Tukaonana maeneo ya Shoppers pale Mbezi Beach.

8. Baada ya kuzungumzia kuhusu mambo mengine y maisha hasa tukikumbushia Stori za chuoni. Tukafika kwenye lengo la kukutana Siku Ile.

9. Alikuwa anamabadiliko kiasi, kidevu na mashavu vikiwa vimefunikwa na ndevu tofauti na alivyokuwa chuo. Kitambia kiasi. Mambo yake hayakuonekana kwamba ni mabaya. Hata yeye mwenyewe alikiri hela ya kubadilisha mboga haimsumbui.

10. Akaniambia, anataka kuoa. Sasa nikajua anataka niwe bestman wake. Akamsifia Sana huyo mchumba wake. Huku akitumia simu kunionyesha picha za huyo mwanamke.

11. Ni mwanamke mzuri. Mweupe. Mwenye uso mzuri kutokana na macho na pua mchongoko aliyonayo.
Shape yake size ya kati. Nikamsifu huku nikimhakikishia binti ni chombo kwelikweli.

12. Hakuishia hapo, kusindilia CV, akasema mwanamke wake ni Mfamasia katika Moja ya hospital za private hapa jijini Dar es salaam. Nikamwambia hiyo kwako ni bahati Mzee huku tukicheka wote.

13. Uso wake ulikuwa na furaha Sana aliponisikia nikimpongeza. Ni kama alikuwa akiniamini hivi au kunikubali kwa namna Fulani. Na nili meet mahitaji yake.

14. Nikamuuliza kwa hiyo ndoa lini? Au ndio Ile ya kusogea tuishi? Kabla hajajibu nikamwambia yeye ni MTU wa kufuata protocol na mambo ya Mila na taratibu.

15. Hapo akatulia. Ni kama alikuwa amesafirisha mawazo Yake sehemu. Nami nikamuacha kwa sekunde huku nikimtazama.

16. Akaniambia, Lakini anamtoto.

17. Aliongea hivyo huku akiniangalia kama MTU aliyehisi neno baya limemponyoka mbele ya Mtu anayeheshima. So macho yake ni kama yalikuwa yanategemea kuona mshtuko, au badiliko hasi, au namna yoyote mbaya.

18. Nikamwambia Mtoto sio tatizo.
19. Akaniambia lakini nasomaga Makala zako. Unasemaga vijana wasioe Single Mother.

20. Nikatabasamu. Nikasema vijana ambao hawajaamua, vijana ambao hawana upendo wote. Vijana wasiojiweza na wanaojitafuta kiuchumi wasioe single mother. Lakini haimaanishi single mother wote wanamatatizo. Ila asilimia kubwa wanashida kubwa.

21. Akaniambia ananielewa ninamaanisha nini. Nikamwambia sasa tatizo nini. Kama vigezo vingine vimekaa vizuri na amethibitisha anampenda, na yupo tayari kukabiliana na changamoto zozote why not.

22. Akapumua. Akawa kama anapitisha mawazo yake mbele ya kioo huku akiyaangalia. Nikameambia OA. Hata hivyo wewe sio mtu wa Principles ngumu. Utaweza na mtafurahia.

23. Akaongea polepole, tatizo Bi.mkubwa akimaanisha Mamaake. Anasema Mamaake anamzuia asimuoe huyo mwanamke. Kisa na mkasa huyo mwanamke anamtoto.

24. Amejaribu kumshawishi mamaake lakini bi. Mkubwa amegoma. Anasema kama yeye sio mtoto wake amuoe huyo mfamasia.

25. Hivyo amekuja kwangu kuomba ushauri akitegemea Mimi nitampa suluhu Bora kabisa katika mtihani wake huo.

26. Wewe ungekuwa Mimi ungemshauri vipi?

27. Hataki kugombana na Mama Yake kwani anampenda.
28. Hataki kumpoteza mfamasia kwani naye anampenda na anamuona kama mkewe mtarajiwa.

29. Mshikaji anasema, Mamaake mwenyewe aliolewa akiwa tayari na mtoto. Ingawaje baada ya miaka kupita Mzee wao alifariki. Ananiambia kuna Siku mamaake alimrushia maneno yasiyofaa kidogo amjibu kwamba mbona yeye aliolewa akiwa single mother. Lakini alijikuta akijizuia.

30. Binafsi nilimwambia Kwanza asitishe wazo la harusi ya hivi karibuni huku akiendelea na mahusiano na huyo mfamasia.

31. Ajipe muda zaidi, huku mamaake akiona mchango na faida ya mfamasia kwa kijana wake. Akigundua tabia za Mkamwana wake.
Tabia njema na upendo huyeyusha mitazamo potofu na chuki zisizo na sababu.

32. Then baadaye anaweza kumuoa. Lengo ni kutomuudhi Mama lakini pia kupima subira, uvumilivu na usikivu wa mwanamke, Mfamasia.

33. Mshikaji ananiambia mwanamke anahitaji hiyo ndoa kwa haraka kwa udi na uvumba. Kwamba umri kidogo umesogea kwani anamiaka 29. Mshikaji miaka 35.

34. Nikamwambia uamuzi wote uko mikononi mwake. Mimi ushauri wangu ndio huo.
Nilimuambia kama anania ya kumuoa huyo binti lazima ajue anatakiwa kuoa mwanamke ambaye aanasubira, mvumilivu na anayemsikiliza(mwamini).

Kama anahisi utampotezea muda huyo hakuamini. Hiyo ni red flag.

35. Nikamwambia, mambo mazuri kama ndoa hayahitaji haraka. Kuuziwa mbuzi kwenye gunia ni dakika.

36. Nikamwambia, ndoa ni halalalisho la kisheria lakini halizuii nyie kuendelea na mahusiano yenu.

37. Nikamwambia, Mamaake kuna hoja anazo na hatakiwi kuzipuuza. Jukumu lake ni kuzifuatilia kwa kujipa muda.

38. Nikamwambia, usifanye jambo hili kumridhisha au kumthibitishia yeyote unampenda. Bali Fanya. Jambo hili kwa kuonyesha wewe umekua mwanaume na unajua kufanya maamuzi sahihi.
Kwa kulinda heshima ya Kila mmoja wao bila kuathiri yake.

39. Basi tukamaliza. Alinishukuru lakini bado aliniambia amechanganyikiwa.

Je wewe ungemshauri Jambo gani?

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Mama yake hana uhuru wa kumpangia, mzee wa 35 yrs kuogopa kuamua mambo yake kisa eti kakatazwa na mama yake ni kwamba somehow hayuko sawa 'kiuanaume'.
Mwambie kuwa single mother si kwamba she is an automatic red flag lakini hiyo ya kulazimisha ndoa ifanywe haraka mwambie jamaa/rafiki/ndugu yako huyo akimbie fasta because that's an obvious red flag. 29 yrs plus kwamba tayari ameshazaa hana haja ya kuwa na haraka unless kama anaogopa kwamba yale anayotaficha jamaa akiyabaini kutakuwa hakuna tena ndoa.
 
Alafu kijana ambaye hana moyo mgumu na hajaamua kikamilifu sio wazo zuri Sana.
Kijana mwenye mawivu yasiyo na mbele wala nyuma pia sio wazo zuri
Sasa huyo mama singo maza yeye anatoa sababu gani za kumzuia? Mimi mama wadogo walitaka kuleta za kuletwa nikawafumua asubuhi tu na mapema hawakurudi tena! Niliwaukiza hivyo hivyo kwamba wao walienda kwa waume wakiwa singo maza walipungukiwa nini? Nikwaongezea, kama nyie mlikuwa mnawatoroka wazee mnaenda kwa wazazi wenzenu wa kwanza basi mlikuwa takataka! Hawakurudi tena!
 
Back
Top Bottom