Mama yangu sio fighter lakini ni responsible na wa uhakika. Anafaa kuwa subordinate wa mtu na anaperform vizuri kabisa kazini wakati ana elimu si kubwa sana ya kutisha.
Nishaona hana uwezo mzuri wa kusimamia shughuli zake, labda kwakuwa experience hana.
Anatulea peke yake, mzee yuko bize na maisha yake na hataki 'mazoea' kabisa.
Hatuna pesa wala mali za aina yoyote. Tumebarikiwa amani na afya.
Bahati nzuri sisi hatusumbui wala hatuna historia ya utukutu, sio wakorofi wala wasumbufu. Mama haugui kabisa, mara ya mwisho kuumwa serious hatujui ni ugonjwa gani. Alipofukuzwa tu kazi kwa utoro ugonjwa ukaisha.
Naweza jitegemea kwa mambo mengine lakini si kwa ada. Niko chuo, dogo yuko form four.
Sent using
Jamii Forums mobile app