MKAKA HALISI
JF-Expert Member
- Dec 5, 2018
- 714
- 1,419
Tatizo linaanzia hapa mama anaweza kuwa bonge la fighter lkn watoto wanaweza kuwa boooonge la viazi lkn sikusemi wewe mpenzi uko wapi? Njoo in box mamaAcha tu niseme bi mkubwa wangu ni bonge la fighter.. Licha ya kaz anayofanya Kua na maslahi madogo lakini mambo anayoyafanya ni makubwa.. Mama yangu ni mwalimu wa shule ya msingi ila mungu kamjalia akili ya MAISHA..
Maisha ya walimu wa S/M wengi mnayajua ni mwendo wa madeni tu mwanzo mwisho Deni linaisha uku linakuja uku.... Mpka muda mwingine unataman kuacha kazi.. Kuna kipind mama alishawai kunitamkia ivo nikiwa form 2.. Nikamwambia pambana.. Lakin kwa msoto wote uo bado bi mkubwa.. Kasimama.. Anawasaidia sana ndugu zake, anatusomesha sisi wanae mpka ndugu zake.. , anawahudumia wazaz wake kadri awezavyo..
Kwnye family tupo wa 3.. Mim kama first born na wenzangu wa 2 (wote wa kike).. Kingine ninachoshukulu kwa bi mkubwa ametupanga vizul.. Imagine mim kama mtto wa kwanza nipo chuo kikuu kimoja cha AFYA hapa nchini nimebakiza semester moja nimalize tunaisubil COVID-19.. ila anaenifatia yupo form 3.. Na anaefata Ndio ameanza darasa la kwanza mwaka huu ( 2020).. Nais hii imempa muda mzul..
Kama first born najitahid Ku play part yangu vizul sana ikiwemo kujenga uaminifu. Mkubwa sana kuna kipind nikiwa likizo alinipa pesa nisimamie ujenz wa nyumba.. Bas mjengo unaanza mpka unakamilika sijaichukua hata.. TSh.100.. Expenditure zote nilizofanya nilikua nazinote kwnye notebook.. Baada ya ujenz kuisha nikamkabidh zile kalatasi nikamwambia matumiz Ndio kama hayo na pesa full ulizonikabidh zilikua hizi na zilizobaki hizi.. Daah kiukwel hakuamini nais alidhani pesa yote ingeisha.. Akamega kias. flan cha pesa akanipa.. Guys hakuna jambo zuli kwnye kazi za watu kama UAMINIFU.. Ukiwekwa sehemu acha Tamaa.. Toka siku hiyo hakuna password yake nisiyoijua kuanzia BANK mpka miamala ya kwnye simu.. Kila jambo la maendeleo analotaka kufanya lazima anishilikishe.
Honestly bi mkubwa ni mtu wa kubana sana SAVING zinamtoa sana na miradi yake mengine.. Kuna siku aliniambia mwanangu ukianza kujitegemea jalibu kuweka walau 10% ya Pato lako kwa mwezi.... Kulingana na kipato chako.. Akanimbia usiwe mtu wa kumaliza elfu 20 Au 15 kwa siku kwnye kula tu.. Hahaha mwenyewe ana msemo wake anasemaga "TUMBO HALINA SHUKRAN" ila siku moja moja sio mbaya Una enjoy vitu vizul.. Daaaah Mungu niwekee mama yangu Nami nije kumlea... Inshaallah
Mungu awape nguvu wakina mama + wakinadada wapambanaji wote na kuendeleza hizi race.. Uwe umeajiliwa, umejiajili, Au umeajiliwa + kujiajili) mwenyezimungu awazidishie..
Kama hii thread imekuja sehemu sio mniwie radhi wakuu maana hili Ndio jukwaa langu pendwa Humu JF . na linalotembelewa na watu wengi.. Finally tujikinge na COVID-19..
Nawasilisha
From Caglar SOYUNCU
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app