Mama yangu ni Bonge la mpambanaji

Soyuncu

Senior Member
Nov 20, 2019
193
224
Acha tu niseme bi mkubwa wangu ni bonge la fighter. Licha ya kazi anayofanya kua na maslahi madogo lakini mambo anayoyafanya ni makubwa. Mama yangu ni mwalimu wa shule ya msingi ila mungu kamjalia akili ya MAISHA..

Maisha ya walimu wa S/M wengi mnayajua ni mwendo wa madeni tu mwanzo mwisho Deni linaisha uku linakuja uku. Mpka muda mwingine unataman kuacha kazi. Kuna kipind mama alishawai kunitamkia ivo nikiwa form 2. Nikamwambia pambana. Lakini kwa msoto wote uo bado bi mkubwa. Kasimama.. Anawasaidia sana ndugu zake, anatusomesha sisi wanae mpka ndugu zake, anawahudumia wazazi wake kadri awezavyo.

Kwenye family tupo wa 3.. Mimi kama first born na wenzangu wa 2 (wote wa kike).. Kingine ninachoshukulu kwa bi mkubwa ametupanga vizuli, Imagine mimi kama mtoto wa kwanza nipo chuo kikuu kimoja cha AFYA hapa nchini nimebakiza semester moja nimalize tunaisubil COVID-19. ila anaenifatia yupo form 3.. Na anaefata Ndio ameanza darasa la kwanza mwaka huu ( 2020). Naisi hii imempa muda mzuri

Kama first born najitahid ku play part yangu vizuri sana ikiwemo kujenga uaminifu. Mkubwa sana kuna kipindi nikiwa likizo alinipa pesa nisimamie ujenzi wa nyumba.. Basi mjengo unaanza mpka unakamilika sijaichukua hata. TSh.100. Expenditure zote nilizofanya nilikua nazinote kwenye notebook. Baada ya ujenzi kuisha nikamkabidhi zile kalatasi nikamwambia matumizi Ndio kama hayo na pesa full ulizonikabidhi zilikua hizi na zilizobaki hizi.. Daah kiukwel hakuamini naisi alidhani pesa yote ingeisha.. Akamega kias. flan cha pesa akanipa.. Guys hakuna jambo zuli kwenye kazi za watu kama UAMINIFU.. Ukiwekwa sehemu acha Tamaa.. Toka siku hiyo hakuna password yake nisiyoijua kuanzia BANK mpka miamala ya kwnye simu.. Kila jambo la maendeleo analotaka kufanya lazima anishilikishe.

Honestly bi mkubwa ni mtu wa kubana sana SAVING zinamtoa sana na miradi yake mengine.. Kuna siku aliniambia mwanangu ukianza kujitegemea jalibu kuweka walau 10% ya Pato lako kwa mwezi.... Kulingana na kipato chako.. Akanimbia usiwe mtu wa kumaliza elfu 20 Au 15 kwa siku kwnye kula tu.. Hahaha mwenyewe ana msemo wake anasemaga "TUMBO HALINA SHUKRAN" ila siku moja moja sio mbaya Una enjoy vitu vizul.. Daaaah Mungu niwekee mama yangu Nami nije kumlea... Inshaallah

Mungu awape nguvu wakina mama + wakinadada wapambanaji wote na kuendeleza hizi race.. Uwe umeajiliwa, umejiajili, Au umeajiliwa + kujiajili) mwenyezimungu awazidishie..

Kama hii thread imekuja sehemu sio mniwie radhi wakuu maana hili Ndio jukwaa langu pendwa Humu JF . na linalotembelewa na watu wengi.. Finally tujikinge na COVID-19..

Nawasilisha
From Caglar SOYUNCU
 
Kingine nilichogundua kwnye mambo ya kuajiliwa mshahara sio inshu sana wa ww kutoboa kimaisha japo sometimes.. Vice versa is true kama Utatuliza kichwa. maana kuna siku nakaa nafikilia iv ingekuaje bi mkubwa angekua apokea mamilioni ya pesa

Maana kichwa yake imetulia si mchezo ana business idea za kibabe sana.... Angekua anapokea mamilioni angefanya wonders( maajabu) kuna siku alishawai kuniambia

Mwanangu mim mama yako Ata kama ingekua sina hii kazi ya ualimu ila ningetoboa tu kimaisha na mngeish vizul

Nakupenda mama.. Live long..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itakuwa BOMBA nawe ukiwa mpambanaji kama mama yako na siyo kuishia kumsifia tu. Hongera kwa kuwa muaminifu 🙏🏽
 
Hahahha chief siunajua idea zinauzwa kwnye somo la entrepreneur tulisoma IDEA vs CAPITAL... inaanza IDEA kwanza Ndio mana kuna watu wanauza business idea.. Aaah sema watu wa COMMERCE wanafahamu zaid

Ila kwa uchache tu wa idea misimu ya mavumo ikifika kuna kias cha pesa anatoa na kwnda kuzungusha uko kwa wakulima.. So kama soko linakua vizul kwnye mnada.. Mambo yanakua vizul
naomba uniibie idea moja tu ya business mojawapo anayofanya

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom